Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Do! Inasikitisha nakumbuka siku ambayo Tibaijuka anaambiwa akae Pembeni na Mkuu wa Kaya akiwahutubia Wazee wa Dar es salaam alisema zile hela siyo za serikali,Kama wenyenazo walishachukua hawa wametoka wapi kutudai tena,Watanzania wenzangu hii issue IPTL ni ya miaka mingi kwanini kila siku watu zaidi milion 50 tumeshindwa kulipatia ufumbuzi?Hilo ni dili watu serikalini na washirika wao,Mheshimiwa Rais itisha mjadala wa kitaifa kuhusu unyonyaji huu.Wanabodi nataka kujua hao majaji kuna waafrika?na wanapatikana vipi,Tusikurupuke kusaini Maazimio ya kimataifa kuanzisha vitu kama hivi,lazima tujiulize vina faida kwetu? Hii mbinu ninamna ya mabeberu kukwapua Mali yetu kwa mlango wa nyuma kwa kushirikiana na maprofesa(wasomi)wezi tuliowaamini.
 
Viongoz wa serikali na ccm ndio wanaonufaika na hiyo iptl...

Haiwezekani iptl walipwe pasipo kutoa huduma yoyote...

Tanesco inakusanya mapato kwa raia na pesa hizo kulipa wajanja wachache ifike mwisho kwa kuvunja mkataba na iptl..
400m×30=12bilioni,makusanyo kwa mwezi=1.1trilion,hiyo pesa ndogo sana [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Sijui tutaendelea lini! Na likiisha hili kutakuja na mengine yenye utata zaidi na tutaendelea kulipa miaka yote
 
Hiyo ndo ccm wapiga dili wao nawao hao hao wanasema wanazui ufisadi maajabu
Tanzania ni nchi ya amani tuitunze amani yetu,yeyote atakayeleta fyokofyoko atashughulikiwa.
 
Hili gazeti linaleta uchochezi, ile hela ya Escrow ilikuwa siyo hela ya Uma, hii ya sasa ndo ya Uma.

Kwa hiyo tunailipa bila shaka, hela ipo msiwe na wasiwasi jamani, kila mwezi TRA wanavuka lengo la ukusanyaji kodi.
 
...bunge limekaa likapitisha maazimio....mojawapo ikiwa dhidi ya PAP na umiliki wa IPTL...utekelezaji wa maazimio ya bunge hadi leo hatujaona feedback yake bungeni....mambo yanafanyika kama vile nothing happened....ifike mahali hili suala la escrow lirudi lijadiliwe bungeni...kwamba pesa hizi walipe waliozichota....maana wanajulikana....namwona Kafulila akianza kukumbukwa kwa mchango wake kwa taifa hili...maana alipiga kelele saana wakati hela hizi zinataka kulipwa kwa PAP na VIP..lakini wao wakang'an'gana na amri yao ya kimagumashi ya jaji Utamwa...wakachota hela....
 
Tulipe tu.Hamna jinsi.Ni viongozi wetu wametufikisha hapo.
 
...bunge limekaa likapitisha maazimio....mojawapo ikiwa dhidi ya PAP na umiliki wa IPTL...utekelezaji wa maazimio ya bunge hadi leo hatujaona feedback yake bungeni....mambo yanafanyika kama vile nothing happened....ifike mahali hili suala la escrow lirudi lijadiliwe bungeni...kwamba pesa hizi walipe waliozichota....maana wanajulikana....namwona Kafulila akianza kukumbukwa kwa mchango wake kwa taifa hili...maana alipiga kelele saana wakati hela hizi zinataka kulipwa kwa PAP na VIP..lakini wao wakang'an'gana na amri yao ya kimagumashi ya jaji Utamwa...wakachota hela....
Ilifika mahali Kafulila aliitwa tumbili.Na ilibakia kidogo mwanasheria mkuu wa serikali amchape makonde Kafulila.Daima tutamkubuka Kafulila.
 
Rugemalira na wenzake waliochukua pesa warudishe na riba juu au wafilisiwe
 
Here is where we are now as a country!!!!!...so so heartbreaking!!!
 
Kikwete alilidanganya Taifa aliposema zile pesa si za umma, pesa ambazo CAG, BoT na TRA wote walisema ni za umma. Uthibitisho mwingine huu hapa. Kumbe yule mwizi na fisadi Rugemarila hakutoa hata senti moja katika hiyo 30% yake.

"SCB-HK understands that PAP used $75 million of the funds obtained from the escrow account to pay VIP Engineering and Marketing Limited (owned by Tanzanian businessman James Rugemalira) for its 30 per cent shareholding in IPTL," says part of the 100-page ruling.

"The funds held in the escrow account that should have been available to satisfy TANESCO's payment obligations to IPTL under the PPA (power purchase agreement) have therefore been paid to two Tanzanian parties - VIP and PAP - neither of whom made any financial contribution to the construction of the facility," it adds.
 
Pia wote waliohusika kudanganya Bunge na wananchi kwa ujumla washitakiwe na Sheria ichukue mkondo wake...walisema pesa sio ya serikali wala sio ya Tannesco kama nakumbuka vizuri
 
Imbeni tena ule wimbo wa ccm mbele kwa mbele, tutakamuliwa mpaka tubaki mbavu tuu ndoo tutafumbua macho kuwa hili lichama linahitaji kuondoka madarakani
 
Back
Top Bottom