Do! Inasikitisha nakumbuka siku ambayo Tibaijuka anaambiwa akae Pembeni na Mkuu wa Kaya akiwahutubia Wazee wa Dar es salaam alisema zile hela siyo za serikali,Kama wenyenazo walishachukua hawa wametoka wapi kutudai tena,Watanzania wenzangu hii issue IPTL ni ya miaka mingi kwanini kila siku watu zaidi milion 50 tumeshindwa kulipatia ufumbuzi?Hilo ni dili watu serikalini na washirika wao,Mheshimiwa Rais itisha mjadala wa kitaifa kuhusu unyonyaji huu.Wanabodi nataka kujua hao majaji kuna waafrika?na wanapatikana vipi,Tusikurupuke kusaini Maazimio ya kimataifa kuanzisha vitu kama hivi,lazima tujiulize vina faida kwetu? Hii mbinu ninamna ya mabeberu kukwapua Mali yetu kwa mlango wa nyuma kwa kushirikiana na maprofesa(wasomi)wezi tuliowaamini.