Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Hakuna kuwalipa hao mafisadi la sivyo wakamatwe wote waliousaini huo mkataba wa kifisadi na kuisababishia nchi hasara si wote wapo na wanafahamika?
 
Walipwe pesa zao za ugali sababu awali tulishawapa za mboga.
 
Mwache Profesa wetu. Yeye aliletewa mwekezaji na wanasheria wakamthibitishia kuwa sheria zote zimefuatwa. Jaji akasema pesa zilipwe na zikalipwa kwa matapeli, majaji, mawaziri, wabunge na hata maaskofu. Mamlaka za juu zikasema pesa ni za wenyewe na wenyewe siyo TANESCO. Nina hakika profesa hakupewa hata za chai acha za mboga! Hapa tunataka kuona mamlaka mpya zitaita beleshi (spade) ni beleshi au ni kijiko kikubwa!!!!!!!!
The manner which Zile fedha zilitapanywa baada tu ya kugawiwa kwa huyo mtu anayejiita PAP inathibitisha kuwa ule ulikuwa utapeli uliofanywa na wabongo wenyewe. Kuna watu walikuwa eakisema eti mzungu (Yaani standard chartered) kkatapeliwa. Sasa tujifunze kuwa kutapeliana ni msamiati wa Kibongo. Hiyo fedha lazima ilipwe kwa Mwenye nayo. Hatimaye kina Ruge na wanasiasa wa Tanzania waligawana fedha za mlipa kodi wa Tanzania.

Tunasubiri sasa tuwaone kina Ruge na timu nzima ya wanufaika wa escrow account wakitinga mahakama ya mafisadi ambayo jaji Chande amesema iko tayari - hadi senti ya mwisho iliyochukuliwa lazima irudishwe!!
 
Dawa ya mwisho kwa hawa jamaa ni kutolipa tuone watafanya nini. Pesa ya walalahoi haiwezi kutumika kulipa deni hewa kama hili. Hakuna kulipa tuone watafanya nini. Hawawezi kufanya kitu hao. Hamasa za kulipa zipo kimaslahi zaidi kwa wahamasishaji. Ingekuwa kwa Mgabe wangethubutu kumdai? Je angelipa? TZ wameigeuza shamba la bibi. Napinga kabisa kulipwa kwa deni hilo fake. Kila siku wanakuja na style nyingine ya kupiga dili wakijua tutalipa. Afadhari kukosa wawekezaji kuliko kuwa na uwekezaji wa sura hii.
 
Huko tulishatoka sasa ni kujiuliza zitalipwa? Au hazilipwi kama zile za feki?
 
unapinga wewe kama nani?taratibu lazma zifuatwe kuanzia chanzo cha tatizo ndipo ifahamike nini kifanyike!
 
Mimi jicho langu limejikita katka paragraph hii hapa chini kuhusu serikali itachukua hatua gani:

By jerrytz,
"The funds held in the escrow account that should have been available to satisfy TANESCO's payment obligations to IPTL under the PPA (power purchase agreement) have therefore been paid to two Tanzanian parties - VIP and PAP - neither of whom made any financial contribution to the construction of the facility," it adds. Source: jerrytz Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

N.B
VIP Engineering Mkurugenzi wake James Rugemalira na PAP Mkurugenzi wake Harbinder Singh Sethi inaonekana kwa tafsiri yangu kuwa wamepokea pesa wasiyostahili na ndiyo maana wakawa wanazitoa kwa watu mbalimbali bila uchungu kuwa wamezifanyia kazi. Swali kuu, hatua gani zitakuchuliwa kwa kampuni hizi mbili zilizopokea fedha za ESCROW kwa ''makosa'' toka akaunti (ESCROW) maalum kwa ajili ya malipo ya mradi wa umeme PPA/IPTL/Tanesco Tanzania?

FLASHBACK: Decision on jurisdiction Date of dispatch to the Parties: February 12, 2014 Source: website link icsidworldbank.org : Request Rejected


In the arbitration proceeding between


STANDARD CHARTERED BANK (HONG KONG) LIMITED

Claimant

and

TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY LIMITED

(TANESCO)


c.c FRANCIS DA DON ; KipimaPembe ; Masiya ; No Shi niubi ; Hercule Poirot ; Ebale
 
Kwani Tane

Tanesco isipolipa hakuna shida. IPTL hawana uwezo wa kucheza na dola. Watafanya nini? Hakuna kitu. Dawa ni kutolipa tuone watakachofanya hao IPTL.
Hivi wewe unajua sheria na mikataba ya kimataifa kweli,Serikali isipolipa Mali zake zilizopo nje zitakamatwa na kulipa hilo deni.
 
Hahahaaa tukiwaita yule mnyama mmoja akenda huku na wengine hufata tunapigwa ban lakini ukweli unabaki ukweli. Escrow escrow escrow escrow na mliambiwa nini kuhusu hiyo escrow na Tanesco yenu? Hongera Pro. Muhongo sasa watu wanakula matapishi yao wenyewe. Mkome kipiga kelele escrow escrow
 
Kwani Tane

Tanesco isipolipa hakuna shida. IPTL hawana uwezo wa kucheza na dola. Watafanya nini? Hakuna kitu. Dawa ni kutolipa tuone watakachofanya hao IPTL.
iptl haipo kuna PAP na wanaendelea kuzalisha umeme na wanalipwa kama kawa.
 
Namuona Mheshiwa "wapigwe tu" kwa mbaaalii........AKITABASAMU BAADA YA KUTUMWA NA CCM NA KUFANIKIWA KUWADANGANYA WATZ ILI WAGAWANE PESA NA BAADAYE WATZ HAOHAO WABEBESHWE MZIGO WA KULIPA.....
Tanzania Shamba la bibi kizee
Mkuu Jile79,laiti ungekutana na huyu Mzee wa Wapigwe tu na akakuelezea mambo kadhaa,utajuta kuzaliwa Tanzania.
 
TZ ina vyanzo vingi vya mapato tunaweza lipa tena kwa mkupuo kama tulivyonunua ndege:
1. Kuongeza malipo ya mikopo ya wanachuo.
2. kufuta fao la kujitoa
3. Kufuta kiinua mgongo kwa wastaafu.
4. Kuongeza makato kwenye miamala ya benki
5. Kuongeza makato kwenye simu
6. Kutoongeza mshahara kabisa
7.kuacha kuajiri.
8.kulipia "simcard" elfu 10 kwa mwezi.
9.kila gari lenye tairi jeusi kulipa 20,000
10. Kuita wafanyabiashara wachangie.
11. Kukata kodi ya maalimu ya deni la iptl kwa kila mtumishi wa uma.
12. Sadaka za ijumaa, jumamosi na jumapili zipelekwe kwa serikali.
Hapo deni litakisha fasta sana........
 
Hakuna kuwalipa hao mafisadi la sivyo wakamatwe wote waliousaini huo mkataba wa kifisadi na kuisababishia nchi hasara si wote wapo na wanafahamika?

kwa lugha nyingine unasema ikamatwe serikari yote mkuu na taasisi za dini haiwezekani
 
Hivi wewe unajua sheria na mikataba ya kimataifa kweli,Serikali isipolipa Mali zake zilizopo nje zitakamatwa na kulipa hilo deni.
miaka ya 70 iran ilikuwa na mkataba na israel kuuziana mafuta,
hadi utawala wa shah unaondolewa iran ilikuwa ikiidai israel mabilioni ya dola,
israel waligoma kulipa licha ya iran kuwapeleka mahakama hiyohiyo,na hukumu ikatoka israel alipe,mpaka leo hajalipa na hajakamatiwa hata shilingi,ndo ujue hiyo bank uchwara haina mamlaka ya kuforce utekelezwaji wa hukumu zake fake
 
Back
Top Bottom