mwambadog
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 1,736
- 1,446
TANESCO imekamatika tena. Inapaswa kuwalipa Standard Chartered bilioni 320. Haina jinsi ya kufanya,zaidi ya kulipa. Kashfa inayokera ya Escrow imeibuka tena. Imekuja kivingine!
Wakati wa kashfa ya Escrow ambapo mabilioni yalichotwa,kubebwa na kulipwa kwa watu mbalimbali kulikuwa na malumbano ya hoja yasiyo na tija wala haja. Malumbano yalikuwa: ni fedha za umma au si za umma?
Watawala walisema si za umma. Watawaliwa wakasema ni za umma. Mjadala ukalala. Waliopata wakapata,waliokosa wakadata. Kwa deni hili jipya kwa TANESCO la bilioni 420,tuendelee na malumbano yetu?
Mimi nawakera tena,TANESCO haitalipa deni hili kwa fedha za umma!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
mkuu sasa nipo upande wako, mkuu akisimama jukwaani atasema kwa msisitizo wa kisukuma
""TANESCO haitalipa deni hili kwa fedha za umma!""