Tego la usinga; uchawi uliotoweka

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Udanganyifu katika mahusiano ni kitu kikongwe na kinachopigwa vita duniani kote watu kwa maelfu wamepoteza maisha kutokana na ishu za Udanganyifu wivu na kufumaniwa au kufumaniana

Kwa wasambaa kulikuwa na tego moja maarufu sana TEGO LA USINGA tego hili ni baya na lenye nguvu sana ambalo lilitegwa kwenye mapaja ya mwanamke kwa kujulishwa au kwa kutojulishwa

Test yake kama tego linafanya kazi mwanamke angewekewa kipande cha chuma au kisu au panga na kuambiwa akiruke, ambapo kitu hicho kingekatika vipande viwili , kwahiyo hapa mwanamke hana ujanja na anajua fika kinachoendelea

Kwa wale wanawake ambao hawajulishwi ila wana mashaka basi huchukua panga au kitu chochote cha chuma na kukiruka!kikikatika tu anajua hali halisi anatulia. Bahati mbaya sana kuna baadhi ya wanaume huwa hawawaambii wake zao kile walichokifanya na wanawake nao wengine huwa hawana machale na hivyo kusababisha maafa.

Mwanamke mwenye tego la usinga akiingiliwa na mwanaume mwingine yule mwanaume hupigwa na kitu kama shoti na baada ya hapo huanza kuumwa tumbo ambapo hawezi kumaliza masaa sita hufariki huku uume ukiwa umesimama ndii

Usinga si kitu chema kwakuwa hauna dawa na mwanamke hatakiwi kuwa na mtoto mdogo wa kiume ambaye atambeba mara kwa mara
Huu ndio usinga tego baya kabisa enzi hizo usambaani...!

Bahati mbaya wataalam wake wamekufa na ujuzi huo bila kuurithisha kwa yeyote
 
duh hatari sana hiyo, hakuna mahali wameacha maandiko, ni ujuzi wa aina yake!!
 
Wanaume bana, we unagonga wanawake kama kumi huko nje, we kuonjewa tu na mtu mmoja unaua...... Nanyie tutaanza kuwaua hata kwa sumu ya panya!!!
Na hapa ndio linapokuja tatizo linalofanya kusiwe na ndoa siku hizi. Wanawake wanataka kulingana na wanaume kwa kila kitu. Kuna siku tutatakiwa tusaidie kubeba mimba. Lakini mbona hamuombi haki ya kuolewa na wanaume wawili?
 
Mambo hayo yapo sana na usinga upo wa aina nyingi na kwa matumizi tofauti, ninaufaham kidogo ule wa kule upareni hasa upare ya kaskazini naamini unaweza kuwa usinga wenye nguvu zaidi.

Duc In Altum.
 
Hahhahahaaaa MKWECHE
 
Mkweche ni noma
Jogoo litasinzia hadi kutoa udenda
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…