SoC01 Teknolojia ina nafasi kubwa kwa Mwanamke kipindi cha hedhi

SoC01 Teknolojia ina nafasi kubwa kwa Mwanamke kipindi cha hedhi

Stories of Change - 2021 Competition

GUAVA TECHNOLOGIES

New Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
2
Reaction score
2
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la "stories of change". Ni tumaini langu wote ni wazima.

Andiko hili litalenga zaidi uhusianishaji wa teknolojia katika kusaidia Maisha ya watoto wa kike katika kipindi chao cha HEDHI.

Katika Andiko hili tutazungumzia mambo makuu matatu ambayo yataweza kuibua utatuzi wa kitabibu katika kipindi chote cha Hedhi kwa mwanamke tukilenga katika kipindi hiki cha ukuaji wa sayansi na teknolojia, Mambo mengi yamewezeshwa kuendana na kasi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia hivyo fuatana nami hatua kwa hatua:

Nitazungumzia mambo yafuatayo:

  • JE TUNAWEZAJE KUANGAZIA MATATIZO YA HEDHI KWA WANAWAKE?
  • SULUHISHO LILILODHAMILIWA NI LIPI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA?
  • SULUHISHO LITALETA MABADILIKO GANI?


JE TUNAWEZAJE KUANGAZIA HEDHI KWA WANAWAKE KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA?

Je Hedhi Ni Nini?

Hedhi ni baadhi ya mabadiliko katika mwili wa wanawake ambayo hutayarisha nyumba ya uke kupata ujauzito. Kila mwezi mji wa uzazi hupata kokwa ambapo mwanamke akipata ujauzito, mtoto ataweza kukuwa.. Mwanamke asipo pata ujauzito, kokwa haitajiki na damu itatokea ukeni- damu anayoipata mwanamke ambaye hana ujauzito ni hedhi.

Ni changamoto gani/zipi wanawake wengi huwakabili katika kipindi chao cha hedhi?

  • Kutokwa na damu nyingi hivyo kusababisha upungufu wa damu mwilini.
  • Ukosekanaji wa taulo za kike.
  • Kuto kufahamu dalili za visababishi vya magonjwa mengine makubwa.
  • Ukosekanaji wa elimu wa vyakula vipi na nguo zipi zivaliwe wakati wa hedhi.


SULUHISHO LILILODHAMILIWA NI LIPI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA?


  • Mobile Apps
  • Kwa kutumia mobile application wanawake wataweza kuorodhesha ni dalili gani alizonazo na kujibiwa moja kwa moja (Auto reply) kulingana na dalili zake na pia kama atahitaji msaada wa kiafya Zaidi moja kwa moja ataweza kuwasiliana na daktari ili kupewa ushauri zaidi nini afanye na aweze kupata nafuu.
  • Smart Devices.
  • Hivi ni vifaa vya ki elekronic ambacho mwanamke awaye yeyote ataweza kuvaa kama SAA YA MKONONI ambayo itakuwa na uwezo wa ku detect mabadiliko yote ya kimwili ambayo mwanamke anayapitia pia kifaa hiki kitaweza kutoa taarifa kwa muhusika kama ifuatavyo:
  • Kapungukiwa damu, na nini afanye?
  • Ku chunguza dalili zote za mwili na kutoa taarifa kwamba unakaribia katika siku zako za hedhi ili mtu aweze kujiandaa na Kuwasaidia wale wote wenye mvurugiko wa siku zao za hedhi.
  • Maumivu makali ya Tumbo na nini afanye?
  • Ni vyakula gani atumie wakati huo aliopo.

  • MUHIMU:
  • Kifaa hiki kitatolewa ‘’BURE’’ kwa watu waliopo mjini na vijijini

  • Kutumia GPS/ Vituo vya kila mtaa kutoa ‘’BURE’’ Taulo za kike.

Mimi na wewe tujiulize swali hapa??

Je? Wajua Condom Zinatolewa bure katika vituo, Je? Kwanini isiwe Taulo za kike ambayo huwakumba Watoto wakike wengi?


Njia hii itaniua upatikanaji wa taulo za kike kwani katika mobile Apps pia na katika smart devices niliyotaja hapo mwanzo itasaidia kwa watu wanaotumia vifaa hivi vya ki electronic kuwapa uelekeo sahihi wapi wapate taulo za kike BURE na endapo kama ni mgeni eneo husika GPS itamsaidia.
Pia, Kwa wale wote ambao sio watumiaji wa mitandao wataweza kufika katika vituo husika na kupata taulo hizi za kike BURE mijini na vijijini.

SULUHISHO LITALETA MABADILIKO GANI?


  • Afya bora kwa wanawake wote.
  • Kuepukana na magonjwa hatarishi yanayosababishwa na mwanamke kuwa katika kipindi cha hedhi.
  • Pia kurahisisha upatikanaji wa taulo za kike kwa urahisi kuwasaidia wengi walio na vifaa vya ki-electronic na wasio kuwa navyo.
  • Kuweza kuwafikia asilimia kubwa ya watu ili kutoa suluhu ya matatizo yao.


MUHIMU🙏

Usisahau ku Vote kwa Andiko hili, UBARIKIWE……………
 
Upvote 1
Back
Top Bottom