Teknolojia itakavyosaidia kuepusha kupandisha nauli kwenye usafiri wa umma pale mafuta yanapopanda

Teknolojia itakavyosaidia kuepusha kupandisha nauli kwenye usafiri wa umma pale mafuta yanapopanda

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
3,250
Reaction score
5,509
TEKNOLOJIA ITAKAVYOSAIDIA KUEPUSHA NAULI KUPANDA KWA WANAOTUMIA USAFIRI WA UMMA BEI YA MAFUTA IKIPANDA.

Najaribu kuwaza miaka ya baadae jinsi teknolojia itakavyosaidia kuepusha nauli kupanda kwa watumiaji wa usafiri wa Umma pale kunapotokea mabadiliko ya bei za mafuta Duniani.

Nawaza kwa namna:

Kwamba kila mtoa huduma ya usafiri wa Umma awe na kadi maalumu ya kutumia kwenye vituo vya kujazia mafuta na wakaachana na matumizi ya 'Cash' isipokuwa kwa wenye usafiri binafsi.

Kwamba kila kituo Cha kujaza mafuta kiwe na mfumo wa kutumia kadi hiyo unaodhibitiwa na mamlaka ya EWURA na mamlaka nyingine.

Kwamba , kadi hiyo wakati ya dharura na upungufu tu wa mafuta EWURA watakuwa wanaiwekea kiwango cha mafuta ambacho kitahitajika kutumika kwa ajili ya kutoa huduma kwa siku tatu, nikiwa na maana ya kwamba kadi itakuwa ina taarifa za msingi ya sehemu mtoa Huduma anapotolea Huduma na lita ngapi atahitaji kwa siku 3 ili kutoa Huduma bila kukwama .

Kwamba ,kadi hiyo itakapojaza kiwango cha lita za mafuta zinazotakiwa kutoa Huduma haitajaza tena mpaka siku 3 ziishe.

Kwamba , kila mwenye kadi hiyo atatumia kadi kwa ajili ya chombo husika cha kutolea Huduma ya usafiri kwa Umma tu na si vinginevyo na hapa Sheria iwekwe ili kudhibiti.

Kwamba, kadi hiyo itatumika ili kuweka udhibiti wa bei yanapopanda kwa wanaotumia usafiri wa Umma ili kuepusha nauli kupanda kwa kasi

MANUFAA YA UTEKELEZAJI WA MPANGO HUU

Kwanza , Serikali itaweza kudhibiti wa bei ya nauli mafuta yanapopanda kwa sababu wenye kadi hizo ambao ni watoa Huduma wa usafiri wa Umma watapata mafuta kwa bei ile.

Pili ,Serikali itaweza kudhibiti foleni kwa sababu asilimia kubwa ya wenye usafiri binafsi wakiona wanapata mafuta kwa bei kubwa watakuwa wanatumia usafiri wa Umma.

Tatu, Umma utapunguziwa maumivu ya kupanda nauli pale tu mafuta yanapopanda.

Nne, Serikali itakuwa na udhibiti mkubwa wa bei za mafuta unaomlinda mlaji wa chini ambaye ni mtumiaji wa usafiri wa Umma pale mafuta yanapopanda bei.

Tano, mpango huu utasaidia kudhibiti wa mazingira.

Naomba kuwasilisha.
Ahsante
Karlo Thobias Mwilapwa
0715804254
0785655580
[email protected]
 
Back
Top Bottom