Teknolojia ni nzuri ila imechangia sana kuwe na ongezeko la Gen - Z kujitenga na jamii

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Kijana anaweza kukaa ndani siku nzima bila kutoka kwenda nje kujichanganya, tena sio nje tu hata humo humo ndani ya nyumba hatoki kujichanganya na wenzake.

Laptop na simu zimekuwa bei rahisi sana na zenye teknolojia ya juu sana, Internet zimeshuka sana bei ukiwa na elfu 70 unatumia internet bila kikomo hakuna mambo ya kupimiwa GB, kuna mitandao mingi sana yenye watengeneza maudhui wa kila aina na wafuasi wao hawataki kupitwa.

Games zimekuwa na ubora wa hali ya juu kila siku zinaboreshwa na mnazoweza kucheza online na ni moja kati ya addiction ambayo imekamata vijana wengi, kijana anaamka saa sita mchana anacharaza game hadi saa 12 asubuhi.

Kwa upande mwengine watu wameanza kujiingizia vipato vyao tandaoni, ukiwa grpahics designer, video editor, copy writer, social media manager, n.k siku hizi huna haja ya kwenda ofisini, popote kambi ilimradi uwe na internet na laptop yako, Huko Mexico kuna maandamano yanafanyika, wenyeji wa mitaa waliozoea kuchanganyika wanalalamika wamarekani wanaokuja kupanga nyumba wanaofanya hizo kazi wameharibu mitaa yao, mtu kajifungia ndani na kilaptop chake wala hana habari ya kuchanganyika, baada ya mwezi anasepa anakuja mwengine.
 
Si ndio unyama nje umbea mwingi, sehem napoishi nikirud mishe mishe nipo ndani
unakuta wake za watu wananisema nitoke tuwe tunapiga story nje, sijui tupige story Gani
bhasi wanasema mim kiburi najidai aisee changamoto kweli sijui kuishije
 
Kijana anaweza kukaa ndani siku nzima bila kutoka kwenda nje kujichanganya, tena sio nje tu hata humo humo ndani ya nyumba hatoki kujichanganya na wenzake.

Laptop na simu zimekuwa bei rahisi sana na zenye teknolojia ya juu sana, Internet zimeshuka sana bei ukiwa na elfu 70 unatumia internet bila kikomo hakuna mambo ya kupimiwa GB, kuna mitandao mingi sana yenye watengeneza maudhui wa kila aina na wafuasi wao hawataki kupitwa.

Games zimekuwa na ubora wa hali ya juu kila siku zinaboreshwa na mnazoweza kucheza online na ni moja kati ya addiction ambayo imekamata vijana wengi, kijana anaamka saa sita mchana anacharaza game hadi saa 12 asubuhi.

Kwa upande mwengine watu wameanza kujiingizia vipato vyao tandaoni, ukiwa grpahics designer, video editor, copy writer, social media manager, n.k siku hizi huna haja ya kwenda ofisini, popote kambi ilimradi uwe na internet na laptop yako, Huko Mexico kuna maandamano yanafanyika, wenyeji wa mitaa waliozoea kuchanganyika wanalalamika wamarekani wanaokuja kupanga nyumba wanaofanya hizo kazi wameharibu mitaa yao, mtu kajifungia ndani na kilaptop chake wala hana habari ya kuchanganyika, baada ya mwezi anasepa anakuja mwengine.

Itafika mahali binadamu tutakua kama mazombi.. tutakua hatuna uwezo hata wa kutembea tena.
 
Back
Top Bottom