Temba wa TMK wanaume ashushwa jukwaani baada ya kuwaponda Polisi kwenye jukwaa la wasanii wa CCM uwanja wa UHURU

Temba wa TMK wanaume ashushwa jukwaani baada ya kuwaponda Polisi kwenye jukwaa la wasanii wa CCM uwanja wa UHURU

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Msanii Temba baada ya kuimba wimbo wake wa Nampenda yeye, akawaambia ma-DJ watulie kuna jambo anataka kusema. Na haya hapa ni maneno yake!

"Acha niseme na wanyonge wangu na tupo ardhi ya nyumbani, Polisi nyie ni masikini wenzetu tu hivyo mnapaswa kutulinda na siyo kutuwinda"

Kilichofuatia kazimiwa mic na camera zikaelekezwa kwingine. Baadaye naona wanarudi na TID.

Watu wanatema nyongo live!
 
Temba kafanya vizuri sana, Polepole ameshapata ujumbe, japo wanawapata hao wasanii kwa njaa zao, lakini mioyo ya hao wasanii wote iko upinzani, CCM muache kujidanganya muda wenu wa kuendelea kuitawala nchi hii ulishapita.

Wote tumeona wahuni wakijificha nyuma ya polisi na kuurushia mawe msafara wa Chadema jana kule Hai, kama walikuwa wanajikausha hawajui kilichotokea, sasa Temba keshawachafua roho kwenye tamasha lao, hata wakimshusha jukwaani tayari ujumbe umeshafika.
 
Safi sana. CCM wajue kujaa huko uwanjani ni kwa vile kuna burudani ya bure na watu wengi wametiwa umasikini kiasi kwamba kama ni hela kidogo waipatayo inakwenda kwenye mlo, lakini sio mapenzi kwa waandaaji walio waletea umasikini.
 
Msanii Temba baada ya kuimba wimbo wake wa Nampenda yeye, akawaambia ma-DJ watulie kuna jambo anataka kusema. Na haya hapa ni maneno yake!

"Acha niseme na wanyonge wangu na tupo ardhi ya nyumbani, Polisi nyie ni masikini wenzetu tuu hivyo mnapaswa kutulinda na siyo kutuwinda"

Kilichofuatia kazimiwa mic na camera zikaelekezwa kwingine. Baadaye naona wanarudi na TID.

Watu wanatema nyongo live!
Police wa Tanzania si masikini,labda Kama anazungumzia umasikini wa akili na fikra,Ila kwenye kipato hakuna police masikini,minimum wage ya police wa Tanzania ni 5,000,000 take home
 
Back
Top Bottom