SI KWELI Tembo akilala kama wanyama wengine hatoweza kuamka kwasababu ya uzito

SI KWELI Tembo akilala kama wanyama wengine hatoweza kuamka kwasababu ya uzito

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Je ni kweli mnyama Tembo huwa hawezi kulala kama wanyama wenzie na akilala kama wanyama wenzake hupelekea kifo kwasababu ya uzito wa mwili wake

1728820375678.jpeg
 
Tunachokijua
Tembo ni miongoni mwa Wanyama wakubwa wa nchi kavu huku akiwa na mwili mkubwa, mkonga mrefu na kichwa kikubwa huku wakikadiriwa kufikisha hadi kilogram 5,500 kulingana na aina ya tembo husika.

Kama ilivyo kwa binadamu Wanyama pia wanahitaji vitu mbalimbali ikiwemo kula, kuepuka kuuawa, kuzaliana na kulala ili waweze kuvuka kutoka kizazi kimoja Kwenda kingine.

Ukweli upoje kuhusu tembo kulala kama Wanyama wengine?

JamiiCheck imefuatilia tafiti mbalimbali ili kubaini uhalisia wa suala hilo na kubaini kuwa si kweli kwamba tembo akilala kama Wanyama wengine hatoweza kuamka na kupelekea kifo chake. JamiiCheck imebaini kuwa tembo wanalala chini kama Wanyama wengine lakini pia wanalala wakiwa wamesimama, zipo sababu zinazopelekea tembo kutokulala chini mara kwa mara kama Wanyama wengine.

kwa mujibu wa Safari Ventures ambao wamewazungumzia tembo wa Afrika wanaeleza kuwa tembo waishio hifadhini wanalala kwa muda mfupi sana huku wakiwa wamesimama, tembo hufanya hivyo ili kujiepusha na athari mbalimbali zinazoweza kutokea wakiwa wamelala chini kama Wanyama wengine wafanyavyo kwa sababu wao wana uzito mkubwa ambao unawafanya wainuke taratibu hivyo kufanya wakamatwe au wadhurike kwa urahisi na majangiri ama Wanyama wanaokula wanyama wengine.
1728820237924-jpeg.3123521

Aidha tovuti ya Herd trust wanaeleza kuwa tembo mara nyingi huwa wanalala huku wakiwa wamesimama kwa kuegemea miti ama kwenye milima. sababu ya tembo kutokulala chini mara kwa mara ni kutokana na uzito alionao na iwapo atalala chini kwa muda mrefu basi inaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu Kwenda katika baadhi ya viungo ambapo inaweza kuwasababishia majeraha katika baadhi ya maeneo yao ya mwili.

Kwa mujibu wa Safari Venture Tembo wakubwa wanaweza kulala kwa masaa mawili tu kwa siku ingawa pia usingizi huu huwa si wa moja kwa moja na badala yake huwa wanalala kwa dakika chache chache. Inaelezwa kuwa sababu inayowafanya tembo walale kwa muda mfupi ni kwa sababu wanatumia muda mwingi kula ambapo inachukua muda mwingi pia kukimeng’enya chakula walichokula. Hali ni tofauti kwa tembo wanaofugwa ambao wao hulala kwa masaa mengi zaidi ambapo hutumia hadi masaa sita kwa siku kwa ajili ya kulala na pia wao hulaza miili yao chini na hii ni kwa sababu wao hawana hofu na mazingira waliyopo.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na chuo cha Witwatersrand kwa baadhi ya tembo walibaini kuwa tembo wanalala wastani wa masaa mawili kwa siku, tembo wengi hulala wakiwa wamesimama lakini hulala chini kila baada ya siku tatu au nne. Lakini walibaini pia kwamba ulalaji na uamkaji wa tembo unategemeana na usalama wa mazingira na sio kuchomoza na kuzama kwa jua.
Back
Top Bottom