Temeke: DC Jokate Mwegelo aagiza kuwekwa chini ya ulinzi, Viongozi wa Chuo cha Lubondo Training College

Temeke: DC Jokate Mwegelo aagiza kuwekwa chini ya ulinzi, Viongozi wa Chuo cha Lubondo Training College

Wanafunzi wanakuwa wamesaidikaje chuo kikifungwa na viongozi wakiwekwa ndani?

Nilidhani njia sahihi ni kurasimisha uendeshaji na kutoa muda ku-comply na kanuni sheria na taratibu ikiwemo uboreshaji wa madhari ya chuo kama hai-suite sawa na inavyotakikana!!!
 
PhD holder ana msaada gani kwenye ujasiliamali wa kitaaluma? Tatizo mmeweka mkazo kwenye vyeti kama kwamba ndivyo vinavyotoa elimu. Kuna PhDs lundo nchi hii hawana kabisa msaada zaidi ya kutumia vile vyeti kama kitegauchumi wakati wanapwaya kwenye nafasi walizopewa kusimamia.
Utaratibu uko hivi, mtu anayesoma degree au bachelor anatakiwa afundishwe na PhD holder au Associate Professor, watu wenye masters wanabaki kuwa kama ma Assistant Tutorial, Diploma anafundishwa na mtu wa degree + masters holder,

haitakiwi mtu mwenye diploma tu amfundishwe diploma mwenzake, tuachane na mambo ya uzoefu au la maana inawezekana kweli mtu akawa ana diploma na akwa nondo hasa kiasi cha kuweza kufundisha diploma wenzake.

Ila kwa mujibu wa Policy za elimu Duniani kote ni lazima diploma afundishwe na mtu mwenye degree na degree afundishwe na mtu mwenye masters au PhD au Professor
 
Serikali ilishatoa muda kwa vyuo kama hivi kwenda kujisajili na kufuata taratibu zote ila wamiliki hawakufuata taratibu. Shida inakuja pale wamiliki hawataki kujulikana ili wasilipe kodi na kwa sababu wanajua uwezo wao kuwa kujiendesha ni mdogo ndiyo wanaamua kujifichaficha sana, mwisho wa siku elimu wanayotoa inakuwa haitambuliki na inakuwa ni hasara kwa wahitimu hasa wanapoambiwa vyeti vyao havitambuliki.
Mkuu hao wanaojificha lazima wana sababu! Kwa vyovyote kuna mtu mwenye fani yake anafichwa hapo tena inawezeka yuko kwenye system!. Chunguzeni vizuri mtagundua kitu muhimu... Lakini sio kwa mtindo huo wa kufunga vyuo kama vile mnakomesha mtu, Huwezi kuanzisha chuo hivi hivi bila kuwa na A B C ya fani.
 
Mh.Jokate yuko sahihi....

Hao ndio wanaharibu ELIMU YETU.....
Elimu maana yake kuelimishana ili miundombinu ya elimu iliyopo iweze kutoa matokeo tunayoyataka. Kufungia wajasiliamali siyo suruhisho. Kwani hao wanaofungiwa si wana vigezo vya kuajiriwa na Serikali kama kweli huko ndiko kwenye elimu bora?.
 
Hayo yote unayoyasema yalishafanywa na kutolewa maelekezo, sema wabongo ni wagumu kutii sheria na kufuata utaratibu uliowekwa na Mamlaka zao. Serikali kwa upande wake ilishajitahidi kuweka utaratibu wa kumiliki taasisi za Elimu binafsi. DC JOKATE amefanya kwa mujibu wa Sheria.
Hapana! Angeweza kufanya zaidi kwa kujua kiini cha kukaidi agizo. Kama kiongozi anatakiwa kuwa smart sio kuamua kwe mihemuko. Hao watu wanashiriki kujenga, Sasa kama fito wanazotumia kama haziko sawa si wanaelekezwa tu?.
 
DC ameanza kujifunika mashuka kama yule muimba taarab, njaa kitu mbaya sana
 
Ukweli ni kwamba pamoja na kuwa na changamoto ila vyuo kama hivyo ni vingi na ni utapeli tu maana watu wanapoteza muda na gharama, wabongo huwa Wana ujanja mwingi sana na ukute hata watu walishahitimu na kupewa vyeti vya magumashi
 
Huyu dada kachemka vibaya!!!
mambo ya kuwekana ndani ni ushamba....
Hayo wazungumza ni ya huko nje ya Afrika.

Hii ni Tanzania donor country.

Hata huko Ulaya vyuo vya magumashi hufungwa na wamiliki kutozwa faini kwa kuendesha chuo bila usajili.

Ukiendesha chuo bila usajili maana yake unahatarisha hata usalama kwa kuwa na wanafunzi usowafahamu maana hutaandikisha kiufasaha.

Kwa sheria zetu mwenye chuo ametenda kosa la jinai na anapaswa kusaidia uchunguzi akiwa rumande kwanza.

Ni hadi hapo nchi yetu itapofikia "level" ya kuweza kubaini kuwa huyu mwenye chuo anaweza kuwa msaada zaidi kwa jamii akisaidiwa kwa namna moja au ingine.

Ila baadae huyo mwenye chuo kwa kusaidiwa namna ya kuendesha chuo kwa kufuata taratibu au la, aacha.
 
Haya ni mambo ya kipuuzi tu, makonda alikuwepo dar panya rodi walifutika kama hawezi kulinda raia na mali zao arudi maneromango makonda achukue mikoba
 
Tiss cid polisI wapo tutoto tumerekodiwa kwa tecno tuko mitandaoni wanatujua kwa majina kuvikamata shida iko wapi?
 
Sasa mtu amefungua Chuo anatoa elimu mnakimbilia kumfungia!
Kwa nini msikae naye muone anashindwa nini kusajili na mumsaidie apate usajili au apewe provisional registration ili akidhi vigezo then asajiliwe full.
Nchi ya Wajinga hii, elimu ndiyo adui yao Mkuu!
Wajinga wajinga kama akina Mwijaku ndio wanahitajika na Hawa vil.aza waliopewa uDC!
 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. JOKATE MWEGELO Aagiza Kuwekwa Chini ya Ulinzi Mkali Viongozi wa Chuo cha LUBANDO TRAINING COLLEGE

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo ameagiza kuwekwa chini ya ulinzi kwa Viongozi wa Chuo cha Lubando Training College kilichopo Mtaa wa Butiama, Kata ya Mtoni Kijichi baada ya kubaini Chuo hicho kinaendeshwa kinyume cha Sheria.

DC Jokate ametoa agizo hilo wakati alipoungana na Wataalamu katika ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo ambapo aliambatana pia na Mkurugenzi-Uthibiti, Ufuatiliaji na Tathmini kutoka NACTE Dkt. Joefrey Oleke.

Baada ya kufanya mahojiano na Mkuu wa Chuo hicho, DC Jokate alibaini kuwa kwa muda sasa Chuo hicho kimekua kikitoa mafunzo bila kupata usajili, pamoja na kutoa mafunzo kwenye mazingira yasiyo rasmi .

"Hamna kitu kibaya kama kufanya utapeli halafu ukadhani hutagundulika, Serikali ina macho kila sehemu, NACTE kaeni hapa na Polisi, lazima tupate 'information', Chuo hakijasajiliwa lakini hata mandhari yake haistahili, kuna Watu wanatoa huduma ambazo kiuhalisia hawastahili kutoa, tushirikiane katika ufuatiliaji, hawa wachukuliwe hatua kali huu ni utapeli"———-DC Jokate

Kwa upande wake Dkt. Jofrey Oleke amesitisha shughuli zote zinazoendelea katika chuo hicho, huku akielekeza taratibu nyingine za kisheria kufuatwa huku akisema kwa ukaguzi uliofanyika, chuo hicho hakitambuliki NACTE wala VETA.​


View attachment 1919666


Na hakuna tamshi kuhusu wanafunzi waliopo chuoni. Serikali ipo kuanzia ngazi ya Mtaa na haikuliona kwa miaka. Alichokifanya ni kupata simple popularity, au mgao wa hongo umeyeyuka.
 
Back
Top Bottom