Temeke: DC Jokate Mwegelo aagiza kuwekwa chini ya ulinzi, Viongozi wa Chuo cha Lubondo Training College

Wanafunzi wanakuwa wamesaidikaje chuo kikifungwa na viongozi wakiwekwa ndani?

Nilidhani njia sahihi ni kurasimisha uendeshaji na kutoa muda ku-comply na kanuni sheria na taratibu ikiwemo uboreshaji wa madhari ya chuo kama hai-suite sawa na inavyotakikana!!!
 
Utaratibu uko hivi, mtu anayesoma degree au bachelor anatakiwa afundishwe na PhD holder au Associate Professor, watu wenye masters wanabaki kuwa kama ma Assistant Tutorial, Diploma anafundishwa na mtu wa degree + masters holder,

haitakiwi mtu mwenye diploma tu amfundishwe diploma mwenzake, tuachane na mambo ya uzoefu au la maana inawezekana kweli mtu akawa ana diploma na akwa nondo hasa kiasi cha kuweza kufundisha diploma wenzake.

Ila kwa mujibu wa Policy za elimu Duniani kote ni lazima diploma afundishwe na mtu mwenye degree na degree afundishwe na mtu mwenye masters au PhD au Professor
 
Mkuu hao wanaojificha lazima wana sababu! Kwa vyovyote kuna mtu mwenye fani yake anafichwa hapo tena inawezeka yuko kwenye system!. Chunguzeni vizuri mtagundua kitu muhimu... Lakini sio kwa mtindo huo wa kufunga vyuo kama vile mnakomesha mtu, Huwezi kuanzisha chuo hivi hivi bila kuwa na A B C ya fani.
 
Mh.Jokate yuko sahihi....

Hao ndio wanaharibu ELIMU YETU.....
Elimu maana yake kuelimishana ili miundombinu ya elimu iliyopo iweze kutoa matokeo tunayoyataka. Kufungia wajasiliamali siyo suruhisho. Kwani hao wanaofungiwa si wana vigezo vya kuajiriwa na Serikali kama kweli huko ndiko kwenye elimu bora?.
 
Hapana! Angeweza kufanya zaidi kwa kujua kiini cha kukaidi agizo. Kama kiongozi anatakiwa kuwa smart sio kuamua kwe mihemuko. Hao watu wanashiriki kujenga, Sasa kama fito wanazotumia kama haziko sawa si wanaelekezwa tu?.
 
DC ameanza kujifunika mashuka kama yule muimba taarab, njaa kitu mbaya sana
 
Ukweli ni kwamba pamoja na kuwa na changamoto ila vyuo kama hivyo ni vingi na ni utapeli tu maana watu wanapoteza muda na gharama, wabongo huwa Wana ujanja mwingi sana na ukute hata watu walishahitimu na kupewa vyeti vya magumashi
 
Huyu dada kachemka vibaya!!!
mambo ya kuwekana ndani ni ushamba....
Hayo wazungumza ni ya huko nje ya Afrika.

Hii ni Tanzania donor country.

Hata huko Ulaya vyuo vya magumashi hufungwa na wamiliki kutozwa faini kwa kuendesha chuo bila usajili.

Ukiendesha chuo bila usajili maana yake unahatarisha hata usalama kwa kuwa na wanafunzi usowafahamu maana hutaandikisha kiufasaha.

Kwa sheria zetu mwenye chuo ametenda kosa la jinai na anapaswa kusaidia uchunguzi akiwa rumande kwanza.

Ni hadi hapo nchi yetu itapofikia "level" ya kuweza kubaini kuwa huyu mwenye chuo anaweza kuwa msaada zaidi kwa jamii akisaidiwa kwa namna moja au ingine.

Ila baadae huyo mwenye chuo kwa kusaidiwa namna ya kuendesha chuo kwa kufuata taratibu au la, aacha.
 
Haya ni mambo ya kipuuzi tu, makonda alikuwepo dar panya rodi walifutika kama hawezi kulinda raia na mali zao arudi maneromango makonda achukue mikoba
 
Tiss cid polisI wapo tutoto tumerekodiwa kwa tecno tuko mitandaoni wanatujua kwa majina kuvikamata shida iko wapi?
 
Sasa mtu amefungua Chuo anatoa elimu mnakimbilia kumfungia!
Kwa nini msikae naye muone anashindwa nini kusajili na mumsaidie apate usajili au apewe provisional registration ili akidhi vigezo then asajiliwe full.
Nchi ya Wajinga hii, elimu ndiyo adui yao Mkuu!
Wajinga wajinga kama akina Mwijaku ndio wanahitajika na Hawa vil.aza waliopewa uDC!
 
Na hakuna tamshi kuhusu wanafunzi waliopo chuoni. Serikali ipo kuanzia ngazi ya Mtaa na haikuliona kwa miaka. Alichokifanya ni kupata simple popularity, au mgao wa hongo umeyeyuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…