Temitope Balogun Joshua, (TB Joshua) afariki Dunia

Amevipiga vita vilivyo vizuri , mwendo ameumaliza imani ameilinda.
 
Pole kwa msiba.....

Baada ya kukuona hapa, nimekumbuka mbali sana. Enzi za Yahoo Messenger 😊.
 
Nilitegemea CCN/BBC watangaze habari za kifo cha TB Joshua (kama ni kweli). Wala sijaona matangazo kuhusu hilo, tangu saa 11 asubuhi naangalia CNN na BBC! Kweli wazungu wana dharau. Kifo cha TB Joshua is not news to them!
Kwa nini unataka Wamarekani na Waingereza watangaze kifo cha M Nigeria?

Kwani wa Nigeria hawana TV?

CNN na BBC equivalents za Nigeria ziko wapi?

Unataka kuwapangia watu cha kuonesha kwenye TV zao?

Tanzania habari za Jerry Falwell mnaonesha ITV na TBC?

Mnamjua hata Jerry Falwell ni nani?
 
Binfsi simhesabu Tb Joshua kama nabii wa KWELI wa MUNGU. Tb Joshua alikuwa nabii wa uongo, na kipimo cha kumpima Nabii yoyote yule ni NENO LA MUNGU.

Lakini vyovyote vile iwavyo, kama alihubiri Injili kwa husuda, kwa kujipatia faida au kwa kupotosha, hiyo ni juu yake yeye, muhimu ni kwamba jina la BWANA NA MWOKOZI WETU, YESU KRISTO, limetangazwa duniani.
Hukumu tunamwachia MUNGU.
 
"Kama ni kweli" kwahiyo bado unaamini hawezi kufa?
 
Mkuu mpaka Sasa hakuna officially statement from the family or the synagogue. Kwa hivi vyombo kutoa Habari lazima kuwe na official confirmation from reliable sources.

Watatangaza muda muafaka lakini pia waafrica tuache kuabudu miujiza
 
Binfsi simhesabu Tb Joshua kama nabii wa KWELI wa MUNGU. Tb Joshua alikuwa nabii wa uongo, na kipimo cha kumpima Nabii yoyote yule ni NENO LA MUNGU.

Lakini vyovyote vile iwavyo, kama alihubiri Injili kwa husuda, kwa kujipatia faida au kwa kupotosha, hiyo ni juu yake yeye, muhimu ni kwamba jina la BWANA NA MWOKOZI WETU, YESU KRISTO, limetangazwa duniani.
Hukumu tunamwachia MUNGU.
 
Usihukumu ili usije ukahukumiwa Mathayo1:7
 
Kwani mwenyewe TB Joshua amesemaje kuhusu kifo ? Msikilize kwenye video hii !

Usihukumu ili usije ukahukumiwa Mathayo1:7
Unaelewa maana ya neno, "kuhukumu"?

Kuhukumu maana yake ni kutoa adhabu kwa mtu kwa tendo alilofanya.
Sasa mimi nimemuadhibu Tb Joshua???

Unapaswa kuelewa kwamba kuna tofauti kubwa sana kati ya kutoa maoni na kuhukumu.
By the way, ukiisoma comment yangu mpaka mwisho nimeandika wazi kabisa kuwa, "hukumu tunamwachia MUNGU".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…