Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mbunge wa Viti Maalum Grace Tendega amesema uamuzi wa Tanzania kutoruhusu uraia pacha kunaikosesha fursa nyingi za kiuchumi.
Tendega ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Juni 1, 2021 bungeni wakati akichangia katika hotuba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka 2021/22.
Suala la uraia pacha lilipata mashiko zaidi katika mjadala wa Bunge Maalum la Katiba ambapo rasimu ya awali ilipendekeza liruhusiwe kwenye Katiba hata hivyo katika Katiba inayopendekezwa liliondolewa
Hata hivyo limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika mijadala hasa wakati wa Bunge la bajeti ingawa jambo hilo halijapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Leo Tendega amesema kutoutambua au kukubali uraia pacha ni sawa na taifa kuendelea kujitenga na watu wake wakati mataifa mengine wanaendelea kuneemeka.
Mbunge huyo ametaka Tanzania kuwa na orodha kamili ya utambuzi kwa watu wake walio nje ili wasaidie kukuza uchumi ndani ya nchi. Ametolea mfano wa Kenya inapata zaidi ya Dola 2.7 bilioni ambayo ni asilimia 3 ya pato lao zinazotokana na watu wao kwenye uraia pacha.
Akizungumzia hadhi za Balozi za Tanzania amesema majengo ya balozi yamechoka hata kutia aibu lakini Serikali haipeleki fedha za ukarabati. Ameitaka Serikali kuwawezesha mabalozi katika masuala ya kidiplomasia ili walitangaze Taifa hata kwenye mambo ya uchumi.
Mwananchi