Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani kuna chama gani zaidi ya ccmNi wachama gani huyo?
Sio kweli ulimwengu wa Sasa hivi ni ngumu Sana kuvikimbia vyombo vya ulinziHii kitu sijawahi kuikubali hata kidogo Mimi
Yaani mtu uwe na uraia wa nchi mbili kiusalama hii haijakaa vizuri hata kidogo.
Hapo sawaKwani kuna chama gani zaidi ya ccm
Kuruhusu uraia pacha kuna athali gani kama taifa.....??Wasiruhusu uraia pacha.
Waanzishe utaratibu wa permanent residency.
Permanent residents wanakuwa na haki zote lakini hawaruhusiwi kushiriki ktk uchaguzi, na kutumikia ktk taasisi nyeti za serikali.
Tuanxie na permanent Residency kabla ya kufikia dual citizemship.Tundu Lissu mbona ana uraia wa nchi mbili huko ubelgiji ni raia na huku Tanzania bado ni raia. Uraia zaidi ya nchi moja ni nzuri tu tena waafrika itatusaidia sana. Kuna watanzania wanaoishi marekani wamejenga majumba na kuwekeza biashara zao Tanzania, ni ngumu kuwafukuza raia kama hawa. Serikali ikubaliane na mabadiliko dunia ya sasa sio kama ya zamani watu hawaishi kuhama hama hasusan waafrika wanaoenda kutafuta maisha kwenye nchi zilizoendelea. Watanzania tuache uhafidhina.
Kuruhusu uraia pacha kuna athali gani kama taifa.....??
Mkuu wewe kama JokaKuu kama leo Tanzania ikiruhusu uraia pacha, utakuathiri vipi?
Mimi nadhani watanzania hatuna budi kukubali..wakati si milele. Uraia pacha utakuja tuu. ni swala la mda. Kikubwa , kama taifa tuwekane sawa.....tukiamua kuuruhusu..kipi kifanyike kulinda maslahi CORE ya taifa letu. Sioni sababu ya kuzuia uraia pacha.
Mfano kuna watanzania wengi wako nje, wengine walienda kusoma, wengine walijilipua. Hawa waote wameoa, wana familia zao huko ughaibuni. Na majority wanakuja bongo wakiwa na passport za nchi husika. Utawajuaje? Ukweli ni kwamba Uraia pacha hauruhusiwi kisheria lakini watanzania wengi wana passport za nje. Hata serikali hili wanalijua.
Ukweli ni kwamba uraia pacha upo..sema tuu kama kawaida, wadanganyika ukiwadanganya majukwaani...wanademka upepo unakodemkia.
Hata kwenye serikali yetu naamini wamo wengi wenye uraia pacha! Kikubwa serikali should recognize the obvious!
Inawezekana hofu yao ikawa sahihi.....lakini tuache kufaidika na uraia pacha kwa hofu ya watu wachache.....??..kuna watu wana HOFU na suala la uraia pacha.
..kwa mfano, wako wenye hofu kwamba mtu mwenye uraia wa Tz na Uk anaweza " kutuuza " waTz au akafanya hujuma fulani dhidi ya nchi yetu.
Inawezekana hofu yao ikawa sahihi.....lakini tuache kufaidika na uraia pacha kwa hofu ya watu wachache.....??
Ina maana walio pitisha uraia wa nchi mbili wanapata matatizo ya kiusalama? Kama hawapati sisi tunaogopa nini?Hii kitu sijawahi kuikubali hata kidogo Mimi
Yaani mtu uwe na uraia wa nchi mbili kiusalama hii haijakaa vizuri hata kidogo.
Hilo ni wazo zuri sana....naamini wenye mamlaka wanaweza wakalifanyia kazi maana penye wengi pana mengi..binafsi sina hofu.
..ila naamini wenye hofu ni wengi kuliko wasio na hofu.
..nazungumza haya kwa kuzingatia nilichokiona wakati wa mjadala wa uraia pacha ktk bunge maalum la katiba.
..napendekeza ukaazi maalum / permanent residency ambapo mhusika ana fursa zote isipokuwa kushiriki siasa, na kuajiriwa serikalini.
..naamini hoja ya ukaazi maalum / permanent residency inajadilika na inajibu hofu za wanaopinga uraia pacha.
Kwanini uraia pacha una shida?Wasiruhusu uraia pacha.
Waanzishe utaratibu wa permanent residency.
Permanent residents wanakuwa na haki zote lakini hawaruhusiwi kushiriki ktk uchaguzi, na kutumikia ktk taasisi nyeti za serikali.
Nani aliyemwambia huyo mh.mbunge kuwa hakuna uraia pacha.wapo tena wamejaa.Fanya uchunguzi wa kina utapata majibu kiurahisi.Kwani mabilionea waliopo nchini wanapataje mikopo kwenye mabenki nchi za nje?nenda wewe au mimi na vitabu vyetu vya kijani,samahani vya bluu kama hatukujikuta tupo Tandale!!!!!Mbunge wa Viti Maalum Grace Tendega amesema uamuzi wa Tanzania kutoruhusu uraia pacha kunaikosesha fursa nyingi za kiuchumi.
Tendega ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Juni 1, 2021 bungeni wakati akichangia katika hotuba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka 2021/22.
Suala la uraia pacha lilipata mashiko zaidi katika mjadala wa Bunge Maalum la Katiba ambapo rasimu ya awali ilipendekeza liruhusiwe kwenye Katiba hata hivyo katika Katiba inayopendekezwa liliondolewa
Hata hivyo limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika mijadala hasa wakati wa Bunge la bajeti ingawa jambo hilo halijapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Leo Tendega amesema kutoutambua au kukubali uraia pacha ni sawa na taifa kuendelea kujitenga na watu wake wakati mataifa mengine wanaendelea kuneemeka.
Mbunge huyo ametaka Tanzania kuwa na orodha kamili ya utambuzi kwa watu wake walio nje ili wasaidie kukuza uchumi ndani ya nchi. Ametolea mfano wa Kenya inapata zaidi ya Dola 2.7 bilioni ambayo ni asilimia 3 ya pato lao zinazotokana na watu wao kwenye uraia pacha.
Akizungumzia hadhi za Balozi za Tanzania amesema majengo ya balozi yamechoka hata kutia aibu lakini Serikali haipeleki fedha za ukarabati. Ameitaka Serikali kuwawezesha mabalozi katika masuala ya kidiplomasia ili walitangaze Taifa hata kwenye mambo ya uchumi.
Mwananchi
Unaanzaje kumpa permanent residence mtu mwenye asili ya Tanzania. aliezaliwa, kukulia Tanzania na amebadili status kwa minajili ya kutafuta fursa ambazo matunda yake anataka kuwekeza nyumbani. Ifike mahali watanzania tubadili mind-set zetu na twende na wakati. Iweje uraia pacha uwe ni jambo gumu na hatari kwa Tanzania tu ( pengine na nchi chache zenye mindset kama zetu)? Wakati umefika sheria zibadilishwe na uraia pacha uruhusiwe period.Wasiruhusu uraia pacha.
Waanzishe utaratibu wa permanent residency.
Permanent residents wanakuwa na haki zote lakini hawaruhusiwi kushiriki ktk uchaguzi, na kutumikia ktk taasisi nyeti za serikali.
Elezea "HOFU" za Urai Pacha kwa kiunaga ubaga...(kima cha chini cha maneno yasiozidi 1500) Chambua? (Assignment deadline- 00-00-0000)..kuna watu wana HOFU na suala la uraia pacha.
..kwa mfano, wako wenye hofu kwamba mtu mwenye uraia wa Tz na Uk anaweza " kutuuza " waTz au akafanya hujuma fulani dhidi ya nchi yetu.
Elezea "HOFU" za Urai Pacha kwa kiunaga ubaga...(kima cha chini cha maneno yasiozidi 1500) Chambua? (Assignment deadline- 00-00-0000)