Tendega asema Tanzania kutoruhusu uraia pacha kunaikosesha fursa nyingi za kiuchumi

Hii kitu sijawahi kuikubali hata kidogo Mimi

Yaani mtu uwe na uraia wa nchi mbili kiusalama hii haijakaa vizuri hata kidogo.
Sio kweli ulimwengu wa Sasa hivi ni ngumu Sana kuvikimbia vyombo vya ulinzi
 
Ccm wanaogopa sana uraia pacha hofu ya daispora watawabumburusha wanyonge kujua haki zao, wanyonge na masikini ndio uiweka ccm madarakani.
Diaspora awavuti moshi wa mwenge thus Wana exposure ya mambo kuliko wanyonge
 
Nimesoma comments hapa za watu unabaki unacheka tu wanavyo sema kuhusu URAIA PACHA.

Watu wengi wanasema uraia pacha ni hatari kwa usalama wa nchi hebu muulize hatari kivipi hawezi kukupa jibu la uhakika.kwani Watu wengi Wa-Tanzania wamekuwa affected sana na Sera za Ujamaa kutoka hapo walipo aisee nikazi ngumu sn na Bahati mbaya sn miaka 5 iliyopita aisee imewarudisha kwenye zile sera za UJAMAA kwa kasi ya Ajabu.
 
Wasiruhusu uraia pacha.

Waanzishe utaratibu wa permanent residency.

Permanent residents wanakuwa na haki zote lakini hawaruhusiwi kushiriki ktk uchaguzi, na kutumikia ktk taasisi nyeti za serikali.
Kuruhusu uraia pacha kuna athali gani kama taifa.....??
 
Tuanxie na permanent Residency kabla ya kufikia dual citizemship.
 
Kuruhusu uraia pacha kuna athali gani kama taifa.....??

..kuna watu wana HOFU na suala la uraia pacha.

..kwa mfano, wako wenye hofu kwamba mtu mwenye uraia wa Tz na Uk anaweza " kutuuza " waTz au akafanya hujuma fulani dhidi ya nchi yetu.
 
..Uraia pacha hautaniathiri mimi.

..ila ninakumbuka jinsi suala hili lilivyojadiliwa wakati wa bunge la katiba.

..mjadala ule haukuwa mzuri na wenye afya hata kidogo. Ulikuwa wa hovyo sawa na malumbano ya ukabila.

..ndio maana mimi nimeona nije na pendekezo ambalo linajadilika, na linaweza kuwa na nafasi ya kupitishwa.
 
..kuna watu wana HOFU na suala la uraia pacha.

..kwa mfano, wako wenye hofu kwamba mtu mwenye uraia wa Tz na Uk anaweza " kutuuza " waTz au akafanya hujuma fulani dhidi ya nchi yetu.
Inawezekana hofu yao ikawa sahihi.....lakini tuache kufaidika na uraia pacha kwa hofu ya watu wachache.....??
 
Inawezekana hofu yao ikawa sahihi.....lakini tuache kufaidika na uraia pacha kwa hofu ya watu wachache.....??

..binafsi sina hofu.

..ila naamini wenye hofu ni wengi kuliko wasio na hofu.

..nazungumza haya kwa kuzingatia nilichokiona wakati wa mjadala wa uraia pacha ktk bunge maalum la katiba.

..napendekeza ukaazi maalum / permanent residency ambapo mhusika ana fursa zote isipokuwa kushiriki siasa, na kuajiriwa serikalini.

..naamini hoja ya ukaazi maalum / permanent residency inajadilika na inajibu hofu za wanaopinga uraia pacha.

Kv100, Rogojin The Idiot
 
Hii kitu sijawahi kuikubali hata kidogo Mimi

Yaani mtu uwe na uraia wa nchi mbili kiusalama hii haijakaa vizuri hata kidogo.
Ina maana walio pitisha uraia wa nchi mbili wanapata matatizo ya kiusalama? Kama hawapati sisi tunaogopa nini?

Na kama hayo matatizo yapo vyombo vya ulinzi na usalama kazi yake ni nini?

NB: Ukienda kwa mentality hiyo ina maana hata internet izimwe maana ina risks za kisalama.
 
Hilo ni wazo zuri sana....naamini wenye mamlaka wanaweza wakalifanyia kazi maana penye wengi pana mengi
 
Wasiruhusu uraia pacha.

Waanzishe utaratibu wa permanent residency.

Permanent residents wanakuwa na haki zote lakini hawaruhusiwi kushiriki ktk uchaguzi, na kutumikia ktk taasisi nyeti za serikali.
Kwanini uraia pacha una shida?
 
When a fool shoots himself in the foot when starting a marathon, increase your speed.
 
Nani aliyemwambia huyo mh.mbunge kuwa hakuna uraia pacha.wapo tena wamejaa.Fanya uchunguzi wa kina utapata majibu kiurahisi.Kwani mabilionea waliopo nchini wanapataje mikopo kwenye mabenki nchi za nje?nenda wewe au mimi na vitabu vyetu vya kijani,samahani vya bluu kama hatukujikuta tupo Tandale!!!!!
 
Wasiruhusu uraia pacha.

Waanzishe utaratibu wa permanent residency.

Permanent residents wanakuwa na haki zote lakini hawaruhusiwi kushiriki ktk uchaguzi, na kutumikia ktk taasisi nyeti za serikali.
Unaanzaje kumpa permanent residence mtu mwenye asili ya Tanzania. aliezaliwa, kukulia Tanzania na amebadili status kwa minajili ya kutafuta fursa ambazo matunda yake anataka kuwekeza nyumbani. Ifike mahali watanzania tubadili mind-set zetu na twende na wakati. Iweje uraia pacha uwe ni jambo gumu na hatari kwa Tanzania tu ( pengine na nchi chache zenye mindset kama zetu)? Wakati umefika sheria zibadilishwe na uraia pacha uruhusiwe period.
 
..kuna watu wana HOFU na suala la uraia pacha.

..kwa mfano, wako wenye hofu kwamba mtu mwenye uraia wa Tz na Uk anaweza " kutuuza " waTz au akafanya hujuma fulani dhidi ya nchi yetu.
Elezea "HOFU" za Urai Pacha kwa kiunaga ubaga...(kima cha chini cha maneno yasiozidi 1500) Chambua? (Assignment deadline- 00-00-0000)
 
Elezea "HOFU" za Urai Pacha kwa kiunaga ubaga...(kima cha chini cha maneno yasiozidi 1500) Chambua? (Assignment deadline- 00-00-0000)

..kuna baadhi wanaamini waliochukua uraia huko nje hawana uzalendo na uaminifu kwa Tz. Wanaonekana wasaliti wenye tamaa ya kupenda vya nyumbani na ughaibuni.

..pia wanaamini Mtanzani mwenye uraia wa nchi nyingine akipewa uraia wa Tanzania anaweza kuutumia kufanya uhalifu / hujuma dhidi yetu na baadae kukimbilia kwenye nchi iliyompa uraia.

..wengine wanaamini kwamba Watanzania waliochukua uraia wa nchi nyingine hawana mitaji au uzoefu wa kutosha kiasi cha kulazimisha Tanzania iwarejeshee uraia wao wa awali.

..pia kuna suala la KISIASA ambapo inaaminika Watanzania walioko nje wameegemea zaidi upande wa upinzani kuliko upande wa chama tawala na serikali. Hali hiyo inawapa kigugumizi chama tawala kupitisha sheria itakayoruhusu uraia pacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…