Tendo la ndoa chanzo cha kuua ndoa nyingi

Tendo la ndoa chanzo cha kuua ndoa nyingi

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Wanandoa wengi wanaonekana kuamka nyumba moja na wenza wao tena wengine wakionekana kuwa na nyuso za furaha lakini kiukweli yanayoendelea humo ndani sio ya kufurahisha hata kidogo.

Ukweli wenyewe wanandoa wengi hawapati tendo kama walivyokuwa wanafikiria kabla ya kuingia kwenye ndoa. Lakini ni ngumu na aibu kubwa kulalamikia mambo haya kwanza unatoa wapi huo ujasiri wa kusema haupewi na mtu umelala naye kitanda kimoja!

Unakuta kabla ya ndoa mambo yalienda kwa kunyooka. Ila sasa mkioana tu ndo konakona zinaanza visingizio vingi vya hapa na pale haviishi. Mara kichwa kitasingiziwa kuumwa mara tumbo nk. Inafika wakati unaona isiwe kesi nawewe unapotezea au ikibidi unaenda kula mchepuko au malaya huko kitaa maisha yanaendelea.

Mkiamka asbh wanazengo wanajua nyinyi ni wenza na mnaishi kwa furaha amani na utulivu.

Kuna ndoa nyiingi zina staili hii ya maisha ya kinafiki maana unakuta ndio tena mmezaa, mna assets kibao za pamoja na watu wengine hawawezi tu maisha ya kuoa na kuacha kila uchao inabidi tu ufe kiume na tai shingoni. Acha maisha yaendelee.
 
FB_IMG_17170934187102315.jpg
 
Umeongea kuonyesha wanawake ndio mara zote ukataa kutoa utamu
Wakati naamini kuna wanaume pia wanawabania wake zao wakisingizia wamechoka

Lawama zote kwa mwanamke❌
Ukitaka kujuwa ni viumbe gani wana mapepo wewe nenda kwenye makanisa ya kiroho, muda wa kukemea mapepo utakupa majibu wala usimuulize mtu yeyote.
 
Yaani kwamba Watu wanaoana kwa ajili ya tendo la ndoa? Labda hawa watoto wa tisini na 2000 hapo
Mimi bila tendo la ndoa nisingeingia kwenye taasisi hiyo.Ni sawa na unieleze kwamba niwe mtumishi tu ila nisioneshe kuupenda mshahara na nisisumbuesumbue kuhusu kikotoo.Haipo hiyo.Maana halisi ya ndoa bila kuhusisha tendo la ndoa ni kujidanganya mchana kweupe na kunguru wanashangilia viroja vyenu.
 
Back
Top Bottom