Re: Tendwa kuweka historia?Tendwa akifuata sheria na kumtosa ata loss nini kwani JK atakuwa rais tena rais si atakuwa Slaa .Go Tendwa onyesha busara fuata sheria si ulikuwa Judge ww weka historia
Hilo ndili lilikuwa swali la msingi. Mimi nadhani maamuzi yeyote yatamfanya Tendwa awe ameweka historia. Akiamua kumuwekea JK pingamizi ni historia, akiamua kutupilia mbali pingamizi ni historia pia.
Kama akilikubali pingamizi, atakuwa ameiweka TZ katika chart nzuri sana ya kuwa na free and fair election kwa vizazi vijayo, sheria hiyo ya gaharama za uchaguzi itaogopwa sana. Akiamua kutupilia mbali kwa sababu yeyote ile, basi hiyo sheria ndio itakuwa imezikwa moja kwa moja na hatutakaa tuisikie tena, si hivyo tu, atakuwa ameiweka Tanzania njia panda kwa sababu kwa dalili zote alichofanya JK na serekali yake ni rushwa! Ni baada ya Slaa kuziomba kura za wafanyakazi huo mchezo ulifanyika, shame on JK
Halafu ndugu zangu wafanyakazi, hako kanyongeza kanaweza kunyofolewa wakati wowote, sidhani kama mmemepewa hata barua, ni kuwa tu kameonekana kwenye pay check. Kanaweza kunyofolewa baada ya uchaguzi. Msikubali kutumiwa, mtanyanyaswa hadi muone raha. Mishahara yenu itakuwa inaongezwa tu wakati wa chaguzi, so ni vyema mkampuuza JK na kumpa kura mpinzani, kwani JK ameonyesha kuwa inawezekana kuwalipa mshahara huo, ni kuwa vile hawathamini na hakuona kama mnastahili kabla, ni baada ya kuona kura zenu ni muhimu anawahadaa kwa rushwa, shame on him again!