Digital base
Senior Member
- Jul 19, 2020
- 140
- 217
Hello habari ya leo wakuu, hongera kwa mapambano ya kutafuta ajira pasipo Kuchoka licha ya kukosa nafasi
Leo nimekuja na wazo la biashara ambalo binafsi nimelifanyia kazi kwa zaidi ya miaka 3 mfululizo na kwa mafanikio makubwa
Kama utaamua kuchukua hatua na kulifanyia kazi basi utajikomboa kiuchumi wewe pamoja na vijana wenzako utakao waajiri ama kuwapa vibarua
Biashara nnayolenga ni usafi maalum wa kutatua changamoto ya uchafu sugu katika Tiles na Masink ya vyoo
Lakini pia unaweza kujihusisha pia na kusafisha Sofa za Vitambaa,makabati jikoni,kuua wadudu majumbani, sehemu za biashara n.k
Hpa unaweza kutumia mtaji wa kuanzia Tsh. 10,000 mpaka Tsh.150,000 kutokana na namna unavyotaka kuanza
Binafsi nilianza kufanya biashara kwakutafuta wateja mtaani lakini mafanikio makubwa niliyapata baada ya kuanza kufanya matangazo mitandaoni
Vifaa vikubwa vya hii biashara ni dawa za usafi (Tiles cleaner) zipo madukani lakini pia unaweza kutengeneza mwenyewe,Gloves, Mask,Brush n.k
Gharama za kusafishia Tiles zenye uchafu sugu kwa choo ama bafu 1 kwangu mimi nilitoza Tsh. 35,000 mpaka Tsh. 50,000 ikiwa ni pamoja na Sink la choo
Dawa utakayotumia hapa si zaidi ya lita 1 tu ambayo ukinunua dukani ni Tsh.5,000 na ukitengeneza mwenyewe kwa Tsh. 10,000 unapata zaidi ya lita 5 mpaka 8
Mtaji mkubwa wa biashara hii ni nguvu zako, kujitoa, kuipenda kazi yako na kuifanya kwa moyo mmoja bila kujali watu wanasema nini
Ikitokea umepata tenda ya kusafisha nyumba mpya au iliyokarabatiwa unapata pesa nyingi zaidi kwakuwa kazi nayo ni kubwa
Ambapo utatakiwa kusafisha Masink na Tiles kwakuondoa madoa yote na kuvifanya ving'ae kama vilipo toka Dukakis, kusafisha madirisha/Vioo, kutoa uchafu ndani na nje n.k
Asante kwa muda wako kufuatilia ujumbe huu, ikiwa umeipenda biashara hii nitumie ujumbe Pm ntakupa msaada zaidi
Lakini pia ntakupa masomo ya kutengeneza dawa pamoja na jinsi ya kutumia dawa hizo kufanyia usafi
Masomo hayo ntakupatia BURE kabisa bila kulipia chochote lengo ni kukusaidia kijana mwenzangu
Uwe na wakati mwema