Tenzi za rohoni

TENZI NA. 24
1. Tangu siku hiyo aliponijia,
Akae moyoni mwangu,
Sina giza tena, ila mwanga pia
Kwa Yesu mwokozi wangu.

Amani moyoni mwangu,
kwa Yesu, Mwokozi wangu;
Sina shaka kamwe,
Kwa sababu yeye,
Yu nami moyoni mwangu.

2. Sina haja tena, ya kutanga-tanga,
Ndiye kiongozi wangu.
Dhambi zangu zote zimeondolewa,
Na Yesu, Mwanawe Mungu.

3. Matumaini yangu ni ya hakika,
Katika Mwokozi wangu.
Hofu zangu na hamu zimeondoka,
kwa kuwa ninaye Yesu.

Vv
 
Kaa Nami tena ni mwimba ninao upenda sna Tena ukikuta akiimba angela chibalonza kwakweli aliutendea haki wimbo huu
Mkuu, Mungu amrehemu huyo mama maana nyimbo zake zinatufariji sana sisi tulio baki bado hapa Duniani.
 
Huu wimbo mzuri sana kuuimba
 
Naupenda sana huu. "Tufani inapovuma Sana moyoni mwangu"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…