KERO TEOFILO KISANJI UNIVERSITY MBEYA nilipeni stahiki zangu, mama amefariki kwa mimi kukosa hela za kumuuguza

KERO TEOFILO KISANJI UNIVERSITY MBEYA nilipeni stahiki zangu, mama amefariki kwa mimi kukosa hela za kumuuguza

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hivi mtu unajiita msomi kabisa unawezaje kukaa sehemu mpaka unakua na malimbikizo yote hayo ,tena private sector?
Mimi enzi niko nafanya kazi private sector ilikua hata mshahara ukichelewa siku moja bila maelezo,nilikua nahoji,nssf nilikua nakagua kila mwezi kama wameweka na wakichelewa kuweka pia nilikua nawakumbusha.
 
Wajikute tu kuwa mfano😹
Hakuna sehemu kuna fitna kama huko Makanisani 🙌, kufanya kazi huko ni aidha uwe mnafiki uishi kwa kujipendekeza, usipokuwa hivyo utateseka sana.

Ila hizo hela wanazo.
Akizingatia ushauri tuliompa atazipata.
Hicho Chuo alichofanya kazi,,kama sikosei,Makao yake makuu kuna hizo ofisi za ufadhili na Ofisi za top leaders..akapeleke huko malalamiko.Hao uongozi wa Chuo wote wapo chini ya Makao makuu ya Kanisa,
Na si ajabu HQ hawajui anachokipitia. Suluhisho ni yeye kwenda huko.
Nilikuwa nasali Moravian. TEKU walikopa mkopo CRDB bilioni 4 hivi, ikapigwa na watumishi kadhaa hapo chuoni. Zingatia hao watumishi wanakuaga ni wachungaji wenye taaluma nyingine, mfano, HR Management nk, kwa hiyo viongozi wengi wa nafasi za kitaaluma kwenye vyuo vya makanisa ni wachungaji au mapadri. Kwa hiyo fedha ilipigwa na wachungaji

CRDB wakataka kukipiga mnada ili wapate fedha yao. Makao Makuu ya Kanisa la Moravian badala ya kuwawajibisha waliopiga pesa, wao wakaleta deni kwa waumini, kila jumapili mnatangaziwa mchango wa kulipa deni la bilioni 5 sijui (na riba). Wanasema unachangia ili kazi ya Mungu iendelee kufanyika. Kazi ya Mungu ndio huo upigaji

Sasa jamaa hapa anasema kuwa hawalipwi mishahara huku fedha ipo inapigwa na wachungaji. Kumshauri aende kudai makao makuu ni kupoteza muda, kwa kuwa licha ya kuwa hana mahusiano ya kiajira na kanisa bali na TEKU, kanisa na TEKU ni wamoja, wanashirikiana kupiga pesa na kulea wezi, ni vigumu sana kumsaidia.
 
nimefungua kesi SMA lakini kesi ilifutwa kwa mujibu wa wakili aliyekuwa anasimamia kesi hiyo.
Fafanua hapa, kesi ilifutwa lini na kwa sababu zipi. Kwa nini hukua unaenda CMA kwenye kesi yako ili ujue kinachoendelea? Kwa uwepo wa hii kesi, TEKU watasimamia ukucha hapa kuwa ufuate njia za kisheria. Umeshakwenda mahakamani, suala limalizike kimahakama. Fafanua hapa ushauriwe ipasavyo
 
Nilikuwa nasali Moravian. TEKU walikopa mkopo CRDB bilioni 4 hivi, ikapigwa na watumishi kadhaa hapo chuoni. Zingatia hao watumishi wanakuaga ni wachungaji wenye taaluma nyingine, mfano, HR Management nk, kwa hiyo viongozi wengi wa nafasi za kitaaluma kwenye vyuo vya makanisa ni wachungaji au mapadri. Kwa hiyo fedha ilipigwa na wachungaji

CRDB wakataka kukipiga mnada ili wapate fedha yao. Makao Makuu ya Kanisa la Moravian badala ya kuwawajibisha waliopiga pesa, wao wakaleta deni kwa waumini, kila jumapili mnatangaziwa mchango wa kulipa deni la bilioni 5 sijui (na riba). Wanasema unachangia ili kazi ya Mungu iendelee kufanyika. Kazi ya Mungu ndio huo upigaji

Sasa jamaa hapa anasema kuwa hawalipwi mishahara huku fedha ipo inapigwa na wachungaji. Kumshauri aende kudai makao makuu ni kupoteza muda, kwa kuwa licha ya kuwa hana mahusiano ya kiajira na kanisa bali na TEKU, kanisa na TEKU ni wamoja, wanashirikiana kupiga pesa na kulea wezi, ni vigumu sana kumsaidia.
Nimekumbuka kuna siku nimeenda kusali kanisa fulani, nikasikia tangazo la kuchangia shule ya kanisa maana ina hali mbaya hadi wafanyakazi hawajalipwa mshahara miezi mitatu na wanafunzi wanahama. Nilishangaa mnoo aisee maana hilo kanisa linamiliki shule chache hapa nchini, hawakutakiwa kufikia hatua ya kushindwa kujiendesha hadi kuhitaji michango ya waumini.
 
Kifupi ni kwamba, wote mnaosoma vyuo nchini Tanzania mpo kwenye kundi moja kitaaluma. Tofauti kubwa ni ukongwe, mazingira na historia ya vyuo mnavyosoma,,si sababu ya mmoja kujiona bora kuliko mwingine.

Aliyesoma TEKU, UDOM, UDSM na vyuo vingine, wote mpo kwenye mfumo mmoja wa elimu ya juu. Kwa hiyo, msijenge dharau kwa kutegemea jina la chuo ulichosoma. Mwisho wa siku, kinachomtofautisha mtu ni uwezo, maarifa, ujuzi na namna anavyovitumia, si jina la chuo pekee.

Kwa hiyo, kwa lugha nyepesi, msichekane kwa majina ya vyuo; mko kundi moja, tofauti ni ukongwe wa vyuo tu.
 
Back
Top Bottom