Tetemeko kubwa lazikumba Uturuki na Syria. Watu zaidi ya 36,257 Wafariki Dunia

Nasikia eti ukichomewa Qur'an wewe unaelalamikia kuchomewa Qur'an unapigwa na tetemeko la sekunde 90, kweli au uongo?
Huna akili ,tokea wewe ndiye mwanzilishi wa mambo ya kidini humu na tokea mwanzo mpaka sasa bado unaendelea udini katika masuala mazito kama haya na kuandika ili watu waandike negative kuhusu uislamu na tukio hili.

Kumbuka haujui Kesho yako hivyo haipendezi siku wewe ufiwe na Baba yako Mzazi ,Mama yako Mzazi ,Mwanafamilia nk halafu mtu akuletee kejeli za kidini .Jiheshimu angalau kidogo majanga waliyopata hawajaomba wala kusababisha wao.
 
Yalitabiriwa haya Kutokea.

Ni kati ya Oct 20 mwaka 2022 Hadi March 20 mwaka 2023.

Bado yatatokea mengi.

Tuendelee kuomba REHEMA na TOBA.

Aaamen.
 

Ningelikua admin watu kama hawa wanaokejeli na kuchagua race za kuwapa pole ningelikua nawalima life ban.
 
Erdogan katangaza hali ya hatari kwa miezi 3

Hotel za Kitalii kubadilishwa kwa muda na kuwa sehemu ya makazi.

Nchi zaidi ya 70 zimepeleka watu kusaidia, kati ya hizo nchi hakuna nchi moja ya Afrika.

Tanzania yatoa salamu twitter masaa 17 baada ya tukio
 
Jiheshimu angalau kidogo majanga waliyopata hawajaomba wala kusababisha wao
Ila km Qur'an isingechomwa na Sweden na Turkey isingekua msitari wa mbele kulalamika yote haya yasingetokea, hapo pia utapinga?

Erdogan anasema zaidi ya watu 5000 wamefariki dunia, pole kwa Marehemu walale wanapostahiri
 
Kwenye hizo 70 Sweden ipo au haipo?
 
Kwenye epicenter destruction Huwa ni ndogo ukilinganisha na nje kule mawimbi yanapoenda kuishia..... epicenter ni huko Syria.
Mkuu naona somola Jiografia ulililidharau kabisa.

Nawakaribiksha wadau wenzangu wanokumbuka Physical Georgrapy ya Forms Six Topic ya Earthquake.

Epicentre ni kitovu cha tetemeko yaani pale katikati ya Uturuki na karibu kabisa na mji wa Gaziantep.

Sasa Uturuki ipo ndani ya sahani iitwayo "Anatolia Plate" na hii sahani yakinzana na sahani ingine iitwayo "Arabian Plate".

Hivyo tetemeko la ardhi husababishwa na kukinzana kwa sahani hizi mbili yaani movement of tectonic plates na pale zinapokuwa zikisogea ndipo husababisha ardhi kuinuka na kutokea tetemeko la ardhi.

Ule mtikisiko au "tremor" waweza kuenea hadi katika maeneo mengine "provided yamo ndani ya ule mkanda au mkondo wa tetemeko uitwao "faultline".

Tetemeko laweza kutembea umbali mrefu na ndo maana limeweza kufika kilomita hadi 18 na kuingia Syria na pia kutetesha maeneo kama Lebanon Israel, Ugiriki na Cyprus kwa sabau ya ule mkanda.

Kinachoshangaza ni uwezo wa uturuki kama nchi ilipoyo barani Ulaya lakini yashindwa kuwekeza katika sayansi na kuwa na vituo vya kusoma alama za nyakati kuhusu matetemeko na majanga mengine, na hivyo kuwa wamejiandaa kwa kuokoa maisha ya watu.

Japan ambayo nayo huathirika na matetemeko wana somo kabisa la disaster na uokozi pale tetemeko linaposomwa au kugundulika kutaka kutokea.

Watoto wa shule hufundishwa namna ya kujikinga endapo tetemeko linatokea.

Tetemeko la ardhi pia laweza kusababisha tsunami na ndo maana nchi ya Italia yajiandaa kwa hilo.
 
Tetemeko la ardhi pia laweza kusababisha tsunami na ndo maana nchi ya Italia yajiandaa kwa hilo.
Kuna mjinga atakua anachimba madini huko dunia ya pili kalipua baruti kwenye mkanda ili apate Ruby, nimehisi tu
 
Waache kumuudhi Mungu na shepu zao za bandia
 
Ila km Qur'an isingechomwa na Sweden na Turkey isingekua msitari wa mbele kulalamika yote haya yasingetokea, hapo pia utapinga?

Erdogan anasema zaidi ya watu 5000 wamefariki dunia, pole kwa Marehemu walale wanapostahiri
Elimu ya kujua yote hayo umeitoa wapi na unaweza kuweka ushahidi ?

Ni katika ujinga wa mtu kuzua na kuzungumza mambo pasipo na ushahidi.

Waliokufa wanahusika vipi na hilo wakati kuna wengine ni wakiristo na atheist na Waislamu wasiolalamika mbona wamefariki na hilo janga ?

Kwa kuongeza eneo liliotokea maana karibu na mpaani mwa Syria kwa asilimia kubwa linakaliwa na Kurdish people ambao Sweden inawaunga mkono na wanauhasama na serikali ya Turkey..
 
Kwa kuongeza eneo liliotokea maana karibu na mpaani mwa Syria kwa asilimia kubwa linakaliwa na Kurdish people ambao Sweden inawaunga mkono na wanauhasama na serikali ya Turkey
Mchezaji Christian Atsu ameokolewa kwenye kifusi huko Turkey amepona, mkurugenzi wao bado yupo chini ya kifusi hajatolewa hadi mda huu
 
Mbon kwenye video wengi walikua wanaimba

Railauraha Railauraha Railauraha

Vipi hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…