Tetemeko la ardhi latokea Dodoma, Singida

Tetemeko la ardhi latokea Dodoma, Singida

Yaani wanatoa taarifa baada ya matetemeko badala watoe kabla ya matetemeko
Angalia hiki wanachosema hao jamaa zenu hapa...
".
.. Hadi hivi sasa hakujagunduliwa teknolojia ya kuweza kutabiri kutokea kwa tetemeko la ardhi, ... "
 
Huku Afrika huwa tunakutana na matetemeko madogo tu...

Ikitokea siku likapiga lenye scale kuanzia 6 hivi, tutapata hasara ya majengo na miundombinu kwa sana tu...
 
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 4.9 na 4.3 katika kipimo cha richter limetokea kwenye Mikoa ya Singida na Dodoma leo February 17, 2023.

Akithibitisha taarifa hizo Mjiolojia Mwandamizi kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Gabriel Mbogoni amesema kuanzia jana yametokea matetemeko ya ardhi matatu, moja lilitokea maeneo ya mpaka wa Singida na Dodoma likiwa na ukubwa wa 4.9 katika kipimo cha richter, jingine lilitokea asubuhi ya leo likiwa na ukubwa wa 4.3 likifuatiwa na lenye ukubwa wa 4.9 na haya mawili yametokea katika wilaya ya Manyoni.

Hata hivyo Mbogoni amesema mpaka sasa hakuna taarifa zozote za madhara ambayo yamesababishwa na matetemeko ya ardhi ambayo yametokea toka jana.
 
Litokee tu pale mgaso limgunike yule muusji.
 
Hivi dodoma ujenzi wa maghorofa mwisho ngapi kwenda juu

Ova
 
Back
Top Bottom