Tetemeko laipiga Morocco, zaidi ya Watu 2000 wafariki Dunia, majeruhi waongezeka

Acha ujinga. Majanga ya asili yalikuwepo kabla hata ya babu wa babu wa babu yako wa babu yake
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٤١﴾

Ufisadi umedhihiri katika nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale yaliyochuma mikono ya watu ili (Allaah) Awaonjeshe baadhi ya waliyoyatenda ili wapate kurejea.
[Ar-Ruwm 30: 41]


Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekwishabainisha kuwa maafa yatakuwa ni mengi karibu na Qiyaamah pindi aliposema:


“Saa (Qiyaamah) haitosimama hadi elimu ifutwe, wakati kukimbia kwa kasi, #zilzala (#tetemeko la ardhi) kuzidi kwa wing, fitnah nyingi kudhihirika na al-Harj kuengezeka.” Ikaulizwa, “Ee Rasuli wa Allaah, nini hiyo al-Harj?” Akasema, “Al-Qatl, al-Qatl (mauaji).” [Imaam Ahmad]

Sikulazimishi uamini..
 
Huu ni uthibitisho na ushahidi tosha wa kwamba, Mungu HAYUPO.
 
Mungu awajibe? Amuwajibikie nani? Who is above God so that God is accountable to?
Ulipodau kuwa Mungu awanusuru hao waliopatwa na janga hili ulimaanisha nini!?

Kwanini Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote kaumba dunia yenye tetemeko?
 
Ziezi la uokoaji linaendelea, lakini Yesu mwokozi amelala tu.

Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote naye kalala bado.

Kazi ya kuokoa wanafanya wanadamu tu.

Hyo ni kwasababu habari za Mungu ni imani potofu.

Hakuna Mungu katika uhalisia
 
Poleni Sana
Huu Ni Msiba Mzito Kwa Ndugu Zetu
 
Mungu awasaidie Ndugu zetu!🙏
#I feel Morroco❤
Sasa awasaidie nini wakati alikuwa na uwezo wa kuzuia na Hakuzuia?

Ni kwamba, huko anakula bata baada ya mpango wake kutiki, na anajiapisha kuwa na bado Mtamtambua kwa jeuri yake.
 
Sasa awasaidie nini wakati alikuwa na uwezo wa kuzuia na Hakuzuia?

Ni kwamba, huko anakula bata baada ya mpango wake kutiki, na anajiapisha kuwa na bado Mtamtambua kwa jeuri yake.
Walishatukana hao! Na bado, Mungu wao ana mipango mingi dhidi yao.
 
Hao Saudi Arabia zile pesa nyingi wanazotumia kununulia wachezaji rejects toka Ulaya si sasa wazitumie kuwasaidia waislamu wenzao maanake wanadai waislamu wote ni ndugu.

Waarabu sio watu wa kutoa kwa wenye shida ila ni watu mabahiri sana na kwa hapo wazungu ni namba moja duniani kwa kutoa.

Na hao wamorocco kama ni pa kukimbilia wakiwa na shida basi ni Ulaya, Marekani au Canada lakini sio kwa waarabu wenzao kwani sanasana wakienda kwa waarabu wenzao watafurumishwa vibaya. Waarabu bure kabisa.
 
Nipende kutoa pole kwa wamorocco katika tukio hili baya lililoikumba nchi yao.

Nimepitia baadhi ya comments za watu kwenye thread hii na sikupenda kumquote mtu yeyote ili isijeleta picha mbaya, hivyo nipende kusema hili janga halijapangwa na Mwenyezi MUNGU.

Wala hausiki nalo hata kidogo, isipokua jambo hili limetengenezwa na binadamu walio na nia mbaya kabisa kuhusu dunia yetu. Wenye mipango mingi miovu ambapo baadhi wameishaitekeleza na mingine inasubiriwa wakati maalumu kutekelezwa.

MUNGU yupo na huwa anatupigania sana lakini hilo huwa hatulitambui, sababu sisi binadamu huwa tunaongozwa sana na hisia.

Hivyo nimalizie tu kusema tujifunze kusoma sana na kusali, sababu hata huu mfumo wetu wa maisha tunaoishi leo binadamu ni mfumo feki ambao MUNGU hakutupangia tuishi.
 

Maneno ya mwanadamu akishakuwa ameshiba ugali...
 
Ndugu zao wa Ulaya wamekaa kimya kbs juu ya hili.
 
Ndugu zao wa Ulaya wamekaa kimya kbs juu ya hili.
Mkuu kwa wazungu wao pekee ndio wanaotoa misaada sana likija zoezi la uokoaji na hata ubinadamu tu

Mpaka sasa kuna mataifa mengi ya Ulaya yameenda, je huoni Spain wanajeshi na mbwa wa kutafuta miili ya watu na Royal Airforce ya 🇬🇧 wamepeleka misaada kibao

Kuna volunteers wengi wameondoka huku ulaya kwenda kusaidia ila sisi hata gunia la Unga wa ngano hatujawapa

Likija suala la msaada waafrika hatuna kwani kuna watu wanaona bora kumtajirisha mtu anaewadanganya kuwa pepo ni yao ila masikini kipofu aliekaa barabarani anampita kama hamuoni

Majanga yapo kila mahali tuwe na huruma kwani hata sisi yanaweza kutukuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…