Tetesi: Azam Tv kutoonyesha La liga msimu huu

Tetesi: Azam Tv kutoonyesha La liga msimu huu

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Kumekuwa na uvumi kuwa kampuni ya Azam Tv wameamua kutokuongeza tena mkataba wake wa kuonyesha ligi kuu ya Uhispania, maarufu kama La Liga. Hivyo kufanya chaneli yao ya Azam Sports HD iliyokuwa ikitumika kurusha matangazo ya mechi za Laliga kujikita zaidi kuonyesha ligi ya VPL.

Inadaiwa hasara imekuwa kubwa, matangazo wanayanunua kwa bei kubwa sana, huku wakiuza kwa bei rahisi kwa wateja wao.

Hizi bado ni fununu hazijathibitishwa, ila ikiwa ni kweli, nawaona Dstv wakizidi kutunyonya kwani lazma watapandisha chaneli yao ya michezo ya Laliga kwenye vifurushi vya juu!

Ngoja tuone Azamtv wakithibitisha ukweli wa tetesi hizi!
 
Ligi kuu tz itawabeba sana azam

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Wahamie EPL mazima hawatajuta na watakuja kunishukuru baada ya msimu mmoja tu ila wasipandishe bei ya vifurushi
Hiyo la liga tu wapate hasara, ndio wathubutu kwenye epl?!!! Kwa hivi vifurushi vya 18,000-28,000?!!kwanza hiyo haki tu kuipata ni balaa!! Kama unakumbuka kampuni ya G-TV, walikuwa wana bei ya 46,000,mbona hata msimu haukuisha wakachemka,??? Sio rahisi ki hivyo.
 
Mesi na Ronaldo hawapo Laliga hivyo hakuna mvuto tena. Waangalie uwezekano wa kuonyesha ligi ya EPL. Pia Italy au Germany angalau kuna kiji mvuto.

Pia ligi yetu Bongo inaanza kuvutia, wajaribu kupanua wigo wa Ving'amuzi vya Azam kwenye nchi tulizochukua wachezaji mfano Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Zambia, Msumbiji na Zimbabwe.
 
Back
Top Bottom