Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mzurimie tunajaribu kutafta kodi ya kuendesha nchi we unaleta mahaba. Hiyo sio siasa ndo hali halisi tena hii nchi inapambana na muuza saa kariakoo akati kuna 700mill imeingia na inaondoka bila kodi na wewe eti unasema ni wivu. Nakuomba Chabruma nisaidie kumwambia DC wetu kama wilaya imeingiza kiasi gani kwa onesho lile kufanyikia wilayani kwake. Na pia tujue TRA imelamba ngapi. Nchi ndo inaendeshwa namna hyo sio kuwaonea wafanyakazi kwa kuwakata mikodi tu
Si vizuri kumwaga vitu vya watu hadharani namna hii.Ni kama mnawachongea! TRA wanapitaga huku mjue!!!
Mapambo ya Milioni 700? Hata PARADISO hakuna mapambo ya gharama hiyo
Very Cheap argument kiongoziChimunguru acha upimbi pale uwanja wa taifa hakujawahi kuwa na ticket ya Milioni Tatu toka historia ya nchi hii...kwenye party ya Zari kiingilio cha chini kilikua ni Tzs 50,0000 wakati uwanja wa taifa hata Tzs 3,000 unaingia...go back to school otherwise usije na bullshit arguments
yaaan huu uzi nmeupitia kuanzia mwanzo adi mwisho.ndio naanza kupata picha kwa nini wabongo hasa vijana biashara znatushinda hata at the initial stage.yaaan mtia mada hata biashara ya vitumbua huiwezi kwa hesabu zako.yaaan aiseee adi naona aibu kusoma baadhi ya comment.ivi ruge unaweza kumtenganisha na babu tale au saidi fella!!? kweli unashindwa hata kujua udhamini wa mawingu kwenye ile party??unadhani udhamini ni lazima utaoe pesa??kweli unaahindwa hata kujua kua mlimani city iliwekwa faniture na mapambo ya kila aina ya gharama.yaaan io ml700 yako unayoisema kama viingilio yaweza kua ilishia kwenye mapambo ya ukumbi na kodi.aiseee jaman tuache kujidhalilisha ivyo.tuongee mambo ya kitaharam angalau kitaharamu.izi konyagi tunazokunywa vilabuni na kuja kuandika uzi jf zitatuvunjia heshima hata kimataifa jaman
Kwa kweli hata kama ningekuwa ni zuzu wa kuamini kila wala nisingeamini madai ya kuwapo VIP Tables 150. Si kwamba hakuna idadi hiyo ya watu wenye uwezo wa ku-order idadi hiyo ya meza bali ni kwamba ukumbi mzima ungetapakaa meza za VIP!Jumla Tiketi za Tzs 3,000,000 ( VVIP Table) zilizouzwa ni 150 only = (3,000,000 x 150 = 450,000,000)
Kwa kweli hata kama ningekuwa ni zuzu wa kuamini kila wala nisingeamini madai ya kuwapo VIP Tables 150. Si kwamba hakuna idadi hiyo ya watu wenye uwezo wa ku-order idadi hiyo ya meza bali ni kwamba ukumbi mzima ungetapakaa meza za VIP!
WanaJamii,
I hope mko vizuri jumamosi hii. Jana ile party iliyokuwa inasuburiwa kwa hamu EAST AFRICA nzima ZALI ALL WHITE PARTY ambayo ilifanyika pale Superbrand Hall Mlimani City Beibee....lol
Issue iko hivi originally hiyo party ilikuwa na ya mwana dada Zarina Hassan a.k.a The Boss Lady...alikuja Bongo akiamini hiyo show ni yake exclusively na atakua fully incharge na mapato ya party nzima....kama mtakumbuka matangazo ya mwanzo ya party hii yalikua kama yamedorora flani hivi yani yalikuwa yamekosa SPARK sasa kama kawa Kijana Ruge wa Mawingu akimtuma Bwana Mdogo Seba akachonge na Zari ili wazee wa Mawingu wanunue hiyo show nzima then jukumu la promotion na maandalizi yote waachiwe wao..
Kijana Seba akakutana na Zari pamoja na Diamond pale Kilimanjaro Hotel na kuwapa offer ya Milioni 100 yaani wachukue huo mpunga then mambo mengine wawaachie wao...Mrembo akagoma kabisa kwani aliamini hiyo party inaweza ikamwingizia kama Milioni 500 so hakuwa tayari....Seba ikabidi arudi kwa Ruge na kumwambia The Boss Lady Amekataa hiyo offer...
Ruge ikabidi awa face Zari na Diamond yeye mwenyewe na habari zisizo za uhakika zinasema Zari na Diamond walikubali kuchukua Milioni 200 na kuuza hiyo party kwa wazee wa Mawingu......Kwahiyo mapato yote yaliyopatikana jana usiku yanayokadiriwa kuwa Milioni 700 yalienda kwa the Don mwenyewe.
Jamani hizi ni tetesi tu. Disclaimer...lol
=======Update===
Kutokana maswali mengi yanayohusu mchanganuo wa mapato wa Milioni 700 nimelazimika kuweka mchanganua huo hapa chini.
Ukumbi wa Mlimani City una uwezo wa kuchukua watu waliokaa 'seating capacity' Elfu mbili na mia tano ( 2,500 People).
Jumla Tiketi za Tzs 3,000,000 ( VVIP Table) zilizouzwa ni 150 only = (3,000,000 x 150 = 450,000,000)
Jumla ya Tiketi za Tzs 1,000,000 (VIP Table) zilizouzwa ni 120 only = ( 1,000,000 X 120 = 120,000,000)
Jumla ya Tiketi za Tzs 100,000 zilizouzwa ni 570 only = ( 100,000 x 570 = 57,000,000)
Jumla ya Tiketi za Tzs 50,000 zilizouzwa ni 1,563 only = ( 50,000 X 563 = 78,150,000).
HAYO NI MAKADIRIO YA MAPATO TU
Shikamoo Ruge/Shikamoo Diamond/Shikamoo Zari
Kuna video hapo juu, ni mahojiano kati ya Babu Tale na Millardi.
Tale amesema VIP zilikuwa ni 12 za 1,000,000
VVIP zilikuwa 10 za 3,000,000
Hivyo jumla ya VIP zote ni 22 thamani yake ni 42,000,000