Tetesi huanza na minong'ono

Tetesi huanza na minong'ono

Mbona kwenye kikao hapa wanasema "mitano Tena"
Harafu vipi Cuba hali ya hewa kweli ni mbaya????
Hali ya hewa ilisitisha ziara ya siku 2....

Nilikuwa nasubiri pia tufe ghafla maana kuna mwendawazimu mmoja aliandika kuwa .....sijui nani anaenda kuisimamisha dunia akiwa Cuba....nijajisemea moyoni, dunia hii hii tunayoambiwa iko kwenye 1600kph!
 
Tetesi huanza na minong'ono.. Hiyo minong'ono ikikoma huwa tetesi na tetesi zikikoma huwa breaking news..!
Dunia ya sasa iko uchi kutokana na maendeleo makubwa ya teknolojia.. Dunia haina siri tena!
Unafanya jambo gizani.. Tena giza totoro kabisa lakini unakuja kushangaa jambo hilo linakuja kuwekwa upenuni peupe kwa picha safi kabisa

Kuficha taarifa yoyote kubwa inayoihusu Jamii haisaidii chochote.. Tunaweza kafanya hivyo kwa lengo maalum na sababu maalum lakini kwa dunia hii ya sasa.. Taarifa zinaweza kuvuja zenyewe bila hata kuvujishwa na yoyote yule

Kuna madhara makubwa kwenye taarifa kuvuja zenyewe.. Maana ni sawa na bomba la maji lililopasuka na kuvujisha maji barabarani.. Yale maji hayana mwenyewe.. Yeyote anaweza kuyatumia vyovyote
Taarifa zinazovuja zenyewe hurembwa, hutiwa nakshi na kuongezewa vikolombwezo vya kila aina kulingana na mahitaji ya mlengwa!

Hakuna siri ya mtu moja duniani.. Ni fikra finyu kuruhusu minong'ono itawale kuliko kuweka wazi.. Akili ya binadamu ni kitu kisichozuilika.. Ukiibania taarifa unaiongezea udadisi na mshawasha wa kutaka kujua zaidi.. Kujua kulikoni...

Minong'ono ya Msechu kujiandaa kuingia studio ni uzushi usiofaa kupewa kipaza sauti
Labda ndio spinning za mapingamizi ya uchaguzi you have to be smart enough to punch some of the cockroaches practices
 
Back
Top Bottom