TETESI: Mchakato wa Ajira za Ualimu kufanywa na TAMISEMI, utaratibu wa zamani kutumika

TETESI: Mchakato wa Ajira za Ualimu kufanywa na TAMISEMI, utaratibu wa zamani kutumika

Kwa hali hii tutaendelea kuwa na walimu wabovu miaka na miaka.
Hakuna mwalimu mbovu wewe, mlipe vizuri, mpe vitendea kazi vya kutosha kulingana na kile anachokifundisha, msimamie vizuri na ufuatilie ufundishaji wake mara kwa mara huku ukimpa semina za kutosha.
Haya mambo ya usaili kwa walimu ni upuuzi tu, siasa na kuendeleza rushwa kwa wanaohusika
 
Wanajukwaa, muda mfupi uliopita Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wametoa tangazo la kusitishwa kwa mchakato wa usaili wa ajira za ualimu hadi hapo itakapoarifiwa tofauti.

Aidha, tetesi zilizopo ni kwamba, kelele zimekua nyingi na hivyo imeamriwa mchakato urudi TAMISEMI na usihusihe usaili (interview). Yani, vigezo vile vya zamani ambavyo ni umri na mwaka wa kumaliza shule ndio vitumike katika kuchagua watu wa kujaza nafasi hizo.

Ni masikitiko yetu wadau wa elimu kwamba tulikua tumeanza kupiga hatua kubwa kwenye kuboresha na kubadilisha kabisa ubora wa elimu yetu kwa kuchuja walimu wetu kwa kuzingatia merits na sio kuzoa zoa kama ambavyo ilikua inafanyika.

Najua Profesa Mkenda atakua anasikitika sana huko aliko maana najua yeye ni mdau mkubwa sana wa merits and competence.

Naomba kusisitiza, hizi bado ni tetesi na taarifa rasmi itatolewa na Mamlaka husika. Hongereni mliokua against interview ila mjue ni kaburi la elimu yetu na tutaendelea kuwa inferior ukilinganisha na wenzetu wakenya na wanyarwanda.​
Ubovu sio walimu
Ubovu mfumo
Mfano interview mwalimu wenye GPA sawa
2015 na 2023
Huyu wa 2023 odds za kushinda ni uhakika maana bado vitu vipo moto kichwani
Pia mfumo wa elimu yetu ukiangalia udhaifu wa mitaala
 
MPOTOSHAJI MKUBWA!! Usaili huo unao-base kwenye objective questions hauna uwezo wa kutenganisha pumba na ngano! Inategemea sana bahati kuwa sehemu aliyojiandaa mtu ndiyo iliyotoka. Usaili unasaidia tu kupunguza watu bila lawama!! Labda uniambie wachague kwa ku-base kwenye GPA!! Nayo hiyo ni janga jingine!! Kuna udanganyifu sana vyuoni hasa vyuo vya private!! Watu wataanza kununua GPA!! Hapo ndip[o utaratibu wa zamani ndio ulio bora na fair kuliko utaratibu mwingine wowote!! Utaratibu huo unaamini kuwa kila aliyehitimu anaweza kufundisha vizuri maana chuo chake kimethibitisha ufaulu wake na akapewa cheti!! Lakinin pia uzoefu umeonesha kuwa siyo kila aliyuefaulu vizuri ana uwezo wa kufundisha vizuri!! Hicho ni kitu kingine kabisa!!
Umeonge ukweli
Maana wenye GPA kubwa sio kuwa ndio wanaweza kufanya mwanafunzi afaulu
Changamoto kazini nyingi mno toka kwa jamii na wazazi na wanafunzi
Na anayeamini katika GPA yupo mjini hajatembea
Mfano apewe shule moja ndani ndani huko,atende tuone GPA yake inafanyaje muujiza
 
Mimi ni mwalimu napendelea sana usaili ufanyike ili kupata mwl mahiri.Mwaka wa kumaliza si tatizo maana kama ulisoma ulaelewa sioni tatizo. Shida yetu waalimu tunaogopa usaili hii inaonesha tulikariri masomo pa si kuelewa.
Hapana,usaili huja kulingana na mitaala ya sasa
Tangu 2015 mitaala imebadilika mara tatu hivi
Je huyo wa 2015 kupitia wapi
Pia gharama za safari nk mtaji mkubwa unapotea na wanarudi zero na kazi hawana
Pia Rushwa
Rushwa
Rushwa
 
Huo ni upuuzi Yani mtu amemaliza chuo miaka 10 imepita Leo umfanyie usahili? Nani anawafanyia usahili mawaziri na wabunge...... huo ni ujinga mkubwa Wala si hatua,huko Kuna bias mingi Sana,unampa Mtu maswali ya kuchagua kumpima? Then oral maswali kadhaa,hii ni low level ya kupata watumishi... waongeze vigezo vya mtu kufaulu kusomea ualimu tu
Nakubaliana na wewe, serikali kama inatafuta walimu Bora ianzie kwenye matokeo ,wabadilishe vigezo vya kuwa mwalimu iwe kama unasomea rocket science, baada ya hapo hakuta kuwa na usaili kwa sababu walimu wanaomwagwa vyuo mtaani watakuwa wachache
 
Hakuna mwalimu mbovu wewe, mlipe vizuri, mpe vitendea kazi vya kutosha kulingana na kile anachokifundisha, msimamie vizuri na ufuatilie ufundishaji wake mara kwa mara huku ukimpa semina za kutosha.
Haya mambo ya usaili kwa walimu ni upuuzi tu, siasa na kuendeleza rushwa kwa wanaohusika
Kwahiyo kada nyingine wanaofanya usaili hawana akili ile nyie walimu wa ccm ndo mna akili ????
 
Back
Top Bottom