Tetesi za Matokeo ya NECTA kidato cha nne 2012 [Kabla Hayajatoka]

Status
Not open for further replies.
Usiwe na wasi kwa kuwa leo ndio 4m 6 wanaanza mitihani bac mishale ya saa 9 hivi tuyasikilizieni
 
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema matokeo ya kidato cha nne bado hayajakamilika na kuwa habari zilizozagaa wiki hii kuwa yapo tayari si za kweli.


Hata hivyo Baraza hilo limebainisha kuwa licha ya kutokamilika, matokeo hayo yanakaribia kutoka kwa mujibu wa ratiba za baraza hilo ambapo hutakiwa kutoa matokeo hayo mwezi Februari.


Ofisa Habari na Mawasiliano wa NECTA, John Nchimbi amesema uvumi wa kwamba matokeo hayo yako tayari ulitokana na kuzushwa kupitia mtandao wa kijamii (Facebook).


Alifafanua kwamba habari kuwa matokeo hayo yameanza kutoka kisirisiri kabla hayajatangazwa rasmi na kwamba hatua hiyo inalenga kuyachakachua, siyo taarifa sahihi.


Aliwataka wananchi kuwa makini na uvumi huo kwa vile endapo matokeo hayo yatakuwa tayari yatatangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na pia kuwekwa kwenye tovuti ya Baraza pamoja na wananchi kuweza kuyapata kupitia simu zao za mkononi.
 
Sasa kama ni uzushi ukweli ni upi si wanayo ratiba si waeleze yatatoka lini
 
wewe tatizo nini matokeo utayapata siku yakitoka hata mwezi wa 3 utayapata tu tafuta cozi za computer kasome ...hizo ulizosikia ni tetesi kaa tulia fanya mambo mengine uliambiwa hayatatoka....
 
Madogo sasa hizi post zenu humu zinaboa si msubiri; kwani kwa kupost humu ndio mtayaharakisha au?!
 
Nchi bila maandamano haiendi.

IFM waliandamana kwa kukosa ulinzi.

Sasa ivi wanalindwa mpaka wanapokuwa wanafanya ufuska.

Na nyie andamaneni matokeo yatangazwe.
 
Bas km wote wanaoandka sms hz wamesoma wanatakiwa kupelekwa kwenye chuo chao milembe-dodoma
 
Naiunga mkono hoja iliyoletwa na Mkirua 100%.
 
Last edited by a moderator:
hayana haraka maana hata hivyo form five ni Julai au Septemba..mtaala umebadilika
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…