Tetesi: Tetesi za usajili dirisha dogo Tanzania bara 2024/2025

Tetesi: Tetesi za usajili dirisha dogo Tanzania bara 2024/2025

Hichilema

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2016
Posts
1,608
Reaction score
1,687
1. Kiungo mkabaji Kelvin Nashon anatakiwa Young Africans
2. Kiungo Mshambuliaji Foday Trawally anatakimmowa na Simba SC
3. Larry Bwalya anawindwa na Singida Black Stars na Pamba Jiji
4. Kiungo raia wa DRC, Harvey Onoya anatakiwa na Yanga
5.Kiungo Mbrazil, Bruno Gomez anaweza kurejea Singida Black Stars
6. Kuna uwezekano mkubwa Kwa mchezaji wa Singida Black Stars kupelekwa Young Africans Kwa mkopo/ makubaliano maalumu
7. Kibwana Shomary anatakiwa KMC Kwa mkopo
8. Beki Lameck Elias Lawi anaweza kusajiliwa Simba dirisha dogo au kubwa. Yanga na Azam pia zinamfukuzia
9. Fredy Michael Koublan anatakiwa na Young Africans
10. Kuna mtifuano unaendelea kati ya kocha Gamond, baachi ya wachezaji wa Yanga.
11. Abdelhay Forsy anatakiwa na Simba
12. Sabri Kondo anatakiwa na Simba SC
13. Charles Senfuko anatakiwa Simba SC
14. Salim Mwalimu anatakiwa Azam FC
15. Kambou Dramane anawindwa Simba na Yanga
16. Ibrahima Seck anstakiwa Simba SC
17. Kocha Abdelhamid Moalin atakuwa kocha msaidizi wa Young Africans akimsaidia kocha mkuu mpya
18. Jonathan Sowah amesajiliwa Singida Black Stars
19. Fabrice Ngoma anaweza kuondoka Simba SC hivi karibuni
20. Lameck Lawi anakaribia kujiunga Young Africans kama mambo hayatabadilika
21. Ayoub Lakred anaweza kuondoka Simba SC dirisha dogo. Anatakiwa na Raja Casablanca pamoja na JSK
22. Kuna uwezekano kati ya kocha Sead Ramovic au Kheireddine Madoui kuchukua nafasi Miguel Gamond, Young Africans
23. Kocha Gamond na msaidizi wake wanaweza kuelekea JS kabylie ya Algeria
24. Beki wa kulia wa KMC , Abdallah Said Lanso anatakiwa na Young Africans
25. CEO wa Yanga, Andre Mtine naye anaweza kutimuliwa
26. Mwanasheria wa Yanga, Simon Patrick naye amekalia kuti kavu
27. Kama mambo hayatabadilika, Singida Black Stars itawapa Yanga mchezaji wao mpya Jonathan Sowa huku Yanga wakiwapa Kennedy Musonda kwa mkopo
28. Striker raia wa Uganda, Fahad Bayo anawindwa na Young Africans baada ya kuachana na timu yake
29. Kiungo Lasinne Kouma anazivutia Simba, Yanga na Azam fc
30. Yanga SC inawinda saini ya Kiungo raia wa Mali, Mamadou Koita
31. Winga wa AS Vita, Jonathan Ikangalombo anatakiwa na Young Africans
32. Kiungo mkabaji toka Singida Black Stars, Kevin Nashon anawindwa vikali na Young Africans
33. Israel Mwenda anatakiwa na Yanga
34. Kiungo Micky Harvey Ossete anatakiwa na Young Africans
35. Thank you Ayoub Lakred
36. Thank you Jean Baleke
37. Lauren Makame anatakiwa na Young Africans
38. Mashabiki wa Gamond, wajiandae kuhamia Singida Black Stars
39. Simba SC inaangalia uwezekano wa kumsajili Allan Okello
40. Edgar William anawindwa na Simba SC
41. Joshua Mutale aendelee kuomba sana
42. Kitumbua Cha Lameck Lawi kwenda Young Africans kinatiwa mchanga na Ubaya Ubwela wanaodai ni mchezaji wao na yuko Coastal Union Kwa mkopo. Yanga wanaangalia uwezekano wa kumpata beki mwingine namba 37 hapo juu
43. Djigui Diara nje wiki sita. Max Nzengeli nje wiki mbili
44. Chama nje wiki mbili hadi 3
45. Kulandana anawindwa na Yanga na Simba
46. Kibu Denis anatakiwa na Amazulu ya Afrika Kusini
47. Jonathan Sowah amegoma kujiunga Singida Black Stars baada ya timu yake kumuuza
48. Clement Mzize anatakiwa na Wydad na Al Ittihad ya Libya
49. Imourane Hasane anatakiwa na Simba SC
50. Aishi Manula anaweza kuuzwa Azam FC
51. Karabaka anaelekea Namungo kwa mkopo
52. Stephen Amankona anawindwa na Simba SC
 
Simba watakuwa wamefanya la maana sana, anahitajika kiungo mshambuliaji.. Playmaker wa viwango vya kimataifa.

Ila ndio mambo ya bahati tu, juzi kati nimekutana na mnaijeri anaitwa AYOBAMI JUNIOR ni fundi mnooo, anaujua saana, ingia youtube unamuona, yule kwa sasa ni kasoro yanga tu ndio anaweza asicheze sababu tayari wana PACOME, CHAMA na AZIZ KI, ila timu nyingine zoote anacheza na anafaa kuanza

Nilikutana nae mazoezini nilipoenda kupunguza sumu mwili, anapambana apate timu januari, ni fundi mnoo, akipata timu ya maana yule itakuwa ni moja ya vipaji vinavyoburudisha zaidi ligi yetu.

Namuuliza mchezaji mkubwa kama wewe umekujaje bila connection ya maana, anasema tamaa yake kucheza ligi kuu ya bongo, plus wakala vimeponza, viongozi wake wa shooting stars wanampigia simu kila mara, kapita, kano pillars, kapita akwa united, CV yake kacheza mpaka Confederation cup. Hapo ndio nikagundua kweli ligi yetu ina thamani sana.
Anapambana apate timu yuko radhi kumpa kitu kidogo atakaempa connection
 
Simba wanatakiwa Kuachana na wachezaji wafuatao.
KATI YA DIRISHA DOGO NA DIRISHA KUBWA.

1. Ayoub Lakred.
2. Valentino Nouma.
3. Karabue Chamoe.
4. Fabrice Ngoma.
5.Agustine Okejepha.

_____________________

6.Charles Ohua.
7. Joshua Mutale
 
Timu lote bovu, tufukuze wote tuache Debora, Ateba na Camara. Wengine sio wabaya ila wakacheze Namungo, Geita Gold na Azam huko.
Tusipo fanya hivyo tutaendelea kuburuzwa, ligi imebadilika.kufukuza wote,
Kufukuza wote si rahisi, kimahesabu ya kihasibu haiwezekani, kuwalipa gharama za kuwavunjia mkataba zaidi ya wachezaji 20, kisha usajili wengine 20, simba inaweza filisikia hapo hapo..

Ni kusajili wazuri taratibu na kuacha viazi inapobidi au wakimaliza mkataba.
Utopolo walienda hatua kwa hatua mpaka kufikia kwenye ubora huu
 
Back
Top Bottom