Simba watakuwa wamefanya la maana sana, anahitajika kiungo mshambuliaji.. Playmaker wa viwango vya kimataifa.
Ila ndio mambo ya bahati tu, juzi kati nimekutana na mnaijeri anaitwa AYOBAMI JUNIOR ni fundi mnooo, anaujua saana, ingia youtube unamuona, yule kwa sasa ni kasoro yanga tu ndio anaweza asicheze sababu tayari wana PACOME, CHAMA na AZIZ KI, ila timu nyingine zoote anacheza na anafaa kuanza
Nilikutana nae mazoezini nilipoenda kupunguza sumu mwili, anapambana apate timu januari, ni fundi mnoo, akipata timu ya maana yule itakuwa ni moja ya vipaji vinavyoburudisha zaidi ligi yetu.
Namuuliza mchezaji mkubwa kama wewe umekujaje bila connection ya maana, anasema tamaa yake kucheza ligi kuu ya bongo, plus wakala vimeponza, viongozi wake wa shooting stars wanampigia simu kila mara, kapita, kano pillars, kapita akwa united, CV yake kacheza mpaka Confederation cup. Hapo ndio nikagundua kweli ligi yetu ina thamani sana.
Anapambana apate timu yuko radhi kumpa kitu kidogo atakaempa connection