Tetesi: Tetesi za usajili wa dirisha dogo ligi kuu Tanzania bara 2023/2024

Wapo, watatangazwa soon
 
Uzi wa tetesi
Lkn hauna tetesi zozote
SIMBA imemaliza usajili wa ndani na sasa imehamia anga ya kimataifa baada ya usiku wa kuamkia jana kushusha mashine kimyakimya tayari kwa kuboresha kikosi hicho kilichopo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa sasa visiwani Zanzibar.
.
Simba imemshusha fundi Michael Charamba (27) raia wa Zimbabwe, anayemudu nafasi tofauti kwa eneo la mbele ambaye inaelezwa ni pendekezo la Kocha Abdelhak Benchikha. Huyo ni staa wa kwanza wa kigeni kwa Simba kwenye dirisha dogo kushushwa baada ya awali kutambulishwa Saleh Masoud Karabaka kutoka JKU, huku ikielezwa pia imemalizana na Ladeck Chasambi kutoka Mtibwa Sugar na Edwin Balua kutoka TZ Prisons ikiwa ni wachezaji wa ndani.
.
Charamba aliyeitumikia Chicken Inn ya Zimbabwe anasifika kama kiraka ambaye amekipa kikosi hicho ubora mkubwa kutokana na kumudu kucheza nafasi ya straika, kiungo mshambuliaji, na winga wa kulia.
.
Zaidi ya hayo jamaa anajua kufunga kwa mashuti ya mbali makali ambayo yalimpa ubora mkubwa kwenye Ligi Kuu ya Zimbabwe na sasa anahamishia makali hayo Msimbazi.
 
Hata kwa sawadogo ilikuwa hivi hivi.
 
Mungu asaidie asije kuwa ni winga tena, maana ni kama kamati ya usajili imeelekezwa kusajili winger tu bila kujali mapungufu ya timu
 
Huyu charamba daah , basi bana yaani hadi unajikuta waona aibu kwakweli, hata kama ni upigaji huu ni too much, Bora iwe ni trial tu, JARIBU TENAE, NA HUYO SCOUT HAPANA hii ni dharau kuu ase
 
FUNDI MAIKO
 
Piga mahesabu na kiuwasubu mwasibu ndio utapata jibu.
Punguza shobo. Timu haiwezi kuacha kusajili kwa sababu kuna mtu hakufanya vizuri. Changia kwa utimamu
Mwasibu punguza munkari basi. Mwenzako alikutaka upige tu zile hesabu zako za kihasibu kama ulivyofanya kwenye usajili wa Aziz Kii kipindi kile. Sasa ukali wa nini tena?

Wewe ulitakiwa tu kukukotoa hesabu iwapo huyo Chalamba kutoka timu ya wauza kuku wa kienyeji; ya Chicken inn kama ataisaidia timu yenu, au la. Maana ukumbuke Bosi wako Mo atakuwa ameshakamuliwa mzigo wa kutosha tu hapo na wajanja.
 
Eti kaja kwa majaribio. Kuna vitu vinachekesha sana, timu inayojiita Bora Afrika inamfanyia mchezaji majaribio kabla ya kumsajili.
 
Babakar Sarr kiungo mkabaji raia wa Senegal kutoka US Monastir ya Tunisia kama nilivyosema hapo awali amewasli bongoland na tayari ni mnyama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…