Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,422
- 5,659
Nipo nawaza tu kama mwanangu nae ipo siku mtamkumbuka kwenye teuzi zenu ama ndiyo atakula kulingana na urefu wa kamba ya baba yake ilipoishia.
Kweli maisha kwa masikini ni ndoto isiyofikika, dunia uwanja wa vita na sisi ndiyo tunaopiganishwa, masikini mwenzangu hamka ukachakarike uitafutie familia mlo wa siku na ulipe kodi yao, kumbuka kuwa wapo wavuja jasho na wapo wanaofaidi matunda ya keki hiyo..bahati nikubahatika kuwa na mkono mrefu utafikiwa.
Walianza babu zao sasa wamemaliza mzunguko wa baba zao katika ufalme, picha linaashiria kabisa ni kuwa wazazi wanawapokeza mikoba watoto wao kurithi miliki wakati mwanangu namrithisha jembe la mkono na ardhi yenye ugumba kwa kukosa mbolea na pembejeo ni wazi wananing'ong'a.
Hata ile ada niliyotumia kumsomesha nikidhani ndiyo ukombozi nayo imeishia matumboni mwao hivi sasa wananikejeli tu wakinena kwa vinywa vyao vinavyonuka rushwa, upendeleo, ubinafsi na unafiki.
Ajira ni chache mwambie mwanao ajiajiri aache uvivu mbona kazi ni nyingi tu graduate kafuge hata bata huku bata la Masaki hajui anachokula wa Tabata kweli wanao haki kuna day watapata.. Dunia ni njema ila walimwengu hawana maana.