Teuzi mbalimbali kujaa majina ya watoto wa viongozi na vigogo Serikalini kama taifa tunaelekea wapi?

Nipo nawaza tu kama mwanangu nae ipo siku mtamkumbuka kwenye teuzi zenu ama ndiyo atakula kulingana na urefu wa kamba ya baba yake ilipoishia.

Kweli maisha kwa masikini ni ndoto isiyofikika, dunia uwanja wa vita na sisi ndiyo tunaopiganishwa, masikini mwenzangu hamka ukachakarike uitafutie familia mlo wa siku na ulipe kodi yao, kumbuka kuwa wapo wavuja jasho na wapo wanaofaidi matunda ya keki hiyo..bahati nikubahatika kuwa na mkono mrefu utafikiwa.

Walianza babu zao sasa wamemaliza mzunguko wa baba zao katika ufalme, picha linaashiria kabisa ni kuwa wazazi wanawapokeza mikoba watoto wao kurithi miliki wakati mwanangu namrithisha jembe la mkono na ardhi yenye ugumba kwa kukosa mbolea na pembejeo ni wazi wananing'ong'a.

Hata ile ada niliyotumia kumsomesha nikidhani ndiyo ukombozi nayo imeishia matumboni mwao hivi sasa wananikejeli tu wakinena kwa vinywa vyao vinavyonuka rushwa,upendeleo, ubinafsi na unafiki..ajira nichache mwambie mwanao ajiajiri aache uvivu mbona kazi ni nyingi tu graduate kafuge hata bata...huku bata la masaki hajui anachokula watabata kweli wanao haki kuna day watapata..dunia ni njema ila walimwengu hawana maana.
Sasa ungechambua jina moja moja na ukasema fulani ni mtoto wa fulani kuteuliwa kushika position fulani

Hiki ulichoandika kitawaacha wengi
 
Nipo nawaza tu kama mwanangu nae ipo siku mtamkumbuka kwenye teuzi zenu ama ndiyo atakula kulingana na urefu wa kamba ya baba yake ilipoishia.

Kweli maisha kwa masikini ni ndoto isiyofikika, dunia uwanja wa vita na sisi ndiyo tunaopiganishwa, masikini mwenzangu hamka ukachakarike uitafutie familia mlo wa siku na ulipe kodi yao, kumbuka kuwa wapo wavuja jasho na wapo wanaofaidi matunda ya keki hiyo..bahati nikubahatika kuwa na mkono mrefu utafikiwa.

Walianza babu zao sasa wamemaliza mzunguko wa baba zao katika ufalme, picha linaashiria kabisa ni kuwa wazazi wanawapokeza mikoba watoto wao kurithi miliki wakati mwanangu namrithisha jembe la mkono na ardhi yenye ugumba kwa kukosa mbolea na pembejeo ni wazi wananing'ong'a.

Hata ile ada niliyotumia kumsomesha nikidhani ndiyo ukombozi nayo imeishia matumboni mwao hivi sasa wananikejeli tu wakinena kwa vinywa vyao vinavyonuka rushwa,upendeleo, ubinafsi na unafiki..ajira nichache mwambie mwanao ajiajiri aache uvivu mbona kazi ni nyingi tu graduate kafuge hata bata...huku bata la masaki hajui anachokula watabata kweli wanao haki kuna day watapata.. dunia ni njema ila walimwengu hawana maana.
Pk na mu7 wanafanyaje nao

Huo ndiyo mfumo....

Mjiulize na mtafakari mtauvunjaje

Huo mfumo...

Na wewe ukifanikiwa kuuvunja huo mfumo utakuja kuendeleza mfumo huo huo

Huo ndiyo mfumo

Ova
 
Mbali na teuzi hata ajira nyingi serikalini zimejaa watoto wa wakubwa kutoka chama tawala. Chunguza kama utakuta mtoto wa waziri, manaibu, rc, dc, makatibu wakuu nk ambaye hana ajira
 
Wa kulaumiwa ni babu na wazazi wako. Wakati kina Julius wanapigania uhuru wao walikuwa wanakunywa Chimpumu na kuzichakata papuchi za wake wa watu...

Kaza buti wanao wasije kulalamika kama wewe...
Mkuu ni kama umeamua tu kumtusi huyo mtu!

Ina maana wewe mfumo unaoendelea katika teuzi za vyeo vya maana vya juu hapa nchini hauuoni?

Kuna watu wanateuliwa kwa sifa ya visomo vya elimu yao hapo, ama kwa kushindanishwa na nani waweza kuthibitisha?

Chukulia mfano ulio hai, ni wazazi wangapi leo wanajikusuru kusomesha watoto wao na wakapata ufaulu na sifa sahihi za kufanya kazi, lakini mwisho wa siku wanazagaa mitaani bila chochote.

Majina ya viongozi kubakia maofisini milele, Nyerere, Nyerere Jnr, Kikwete, Kikwete Jnr, Mizengo, Mizengo Jnr nk nk, huo ni mfano tu, maana wapo wengine Identity wanaficha lakini wamo bila ya kuwa na sifa za maana kuwashinda waliopo mitaani.

Ni hoja ya msingi jamaa kasema, kuna upendeleo mkubwa wa wazi katika teuzi hizi, maana si teuzi za kuangalia sifa ya uongozi ama elimu ya mtu, ni kuangalia jina tu, jina ndiyo sifa ya kusogezwa nafasi za juu.

Kwa kuwa ni watoto wa vigogo, hata wafanye makosa ya kinidhamu ama ki jinai ya kuonekana katika nafasi hizo, wananchi mtazugwa katumbuliwa, hatumbuliwi kwa kuwajibishwa, ni mfano wa spare tyre kupumzishwa, muda wowote linapachikwa!

Sasa matendo haya huwa yanachochea chuki na matabaka katika jamii, pia kutoaminika kwa viongozi wakuu wanaotenda haya, kwa sababu kila mwenye akili timamu anaona.

Ifike wakati tukubali kwamba, umuhimu wa Katiba ni sasa, Katiba bora itakayoziba mianya ya upendeleo na kutuweka raia wote katika mizani sawa.
 
Mkuu ni kama umeamua tu kumtusi huyo mtu!

Ina maana wewe mfumo unaoendelea katika teuzi za vyeo vya maana vya juu hapa nchini hauuoni?

Kuna watu wanateuliwa kwa sifa ya visomo vya elimu yao hapo, ama kwa kushindanishwa na nani waweza kuthibitisha?

Chukulia mfano ulio hai, ni wazazi wangapi leo wanajikusuru kusomesha watoto wao na wakapata ufaulu na sifa sahihi za kufanya kazi, lakini mwisho wa siku wanazagaa mitaani bila chochote.

Majina ya viongozi kubakia maofisini milele, Nyerere, Nyerere Jnr, Kikwete, Kikwete Jnr, Mizengo, Mizengo Jnr nk nk, huo ni mfano tu, maana wapo wengine Identity wanaficha lakini wamo bila ya kuwa na sifa za maana kuwashinda waliopo mitaani.

Ni hoja ya msingi jamaa kasema, kuna upendeleo mkubwa wa wazi katika teuzi hizi, maana si teuzi za kuangalia sifa ya uongozi ama elimu ya mtu, ni kuangalia jina tu, jina ndiyo sifa ya kusogezwa nafasi za juu.

Kwa kuwa ni watoto wa vigogo, hata wafanye makosa ya kinidhamu ama ki jinai ya kuonekana katika nafasi hizo, wananchi mtazugwa katumbuliwa, hatumbuliwi kwa kuwajibishwa, ni mfano wa spare tyre kupumzishwa, muda wowote linapachikwa!

Sasa matendo haya huwa yanachochea chuki na matabaka katika jamii, pia kutoaminika kwa viongozi wakuu wanayotenda haya, kwa sababu kila mwenye akili timamu anaona.

Kama taifa kuna umuhimu wa kufanya reforms katika mifumo ya kiutawala & uwajibikaji (katiba), Elimu na vipaumbele vyetu katika uchumi unaotuinua sote.
 
Nipo nawaza tu kama mwanangu nae ipo siku mtamkumbuka kwenye teuzi zenu ama ndiyo atakula kulingana na urefu wa kamba ya baba yake ilipoishia.

Kweli maisha kwa masikini ni ndoto isiyofikika, dunia uwanja wa vita na sisi ndiyo tunaopiganishwa, masikini mwenzangu hamka ukachakarike uitafutie familia mlo wa siku na ulipe kodi yao, kumbuka kuwa wapo wavuja jasho na wapo wanaofaidi matunda ya keki hiyo..bahati nikubahatika kuwa na mkono mrefu utafikiwa.

Walianza babu zao sasa wamemaliza mzunguko wa baba zao katika ufalme, picha linaashiria kabisa ni kuwa wazazi wanawapokeza mikoba watoto wao kurithi miliki wakati mwanangu namrithisha jembe la mkono na ardhi yenye ugumba kwa kukosa mbolea na pembejeo ni wazi wananing'ong'a.

Hata ile ada niliyotumia kumsomesha nikidhani ndiyo ukombozi nayo imeishia matumboni mwao hivi sasa wananikejeli tu wakinena kwa vinywa vyao vinavyonuka rushwa,upendeleo, ubinafsi na unafiki..ajira nichache mwambie mwanao ajiajiri aache uvivu mbona kazi ni nyingi tu graduate kafuge hata bata...huku bata la masaki hajui anachokula watabata kweli wanao haki kuna day watapata.. dunia ni njema ila walimwengu hawana maana.
Kuwa mtoto wa kiongozi sio dhambi,na wao wanastahili teuzi,na Wala sio wengi kiivyo,ndani ya serikali hii,yenye mawaziri na manaibu 52,watoto wa viongozi hawafiki 10,bunge Lina watu 252!watoto wa viongozi hawafiki 20!kwenye ma RC,DC,RAS,DAS,watu zaidi ya 120,watoto wa viongozi hawafiki 40!!sasa kelele za nini.
 
Mbali na teuzi hata ajira nyingi serikalini zimejaa watoto wa wakubwa kutoka chama tawala. Chunguza kama utankuta mtoto wa waziri, manaibu, rc, dc, makatibu wakuu nk ambaye hana ajira
Maana ya taifa ni kugawana kidogo kidogo kilichopo hili kila mtu apate mkate, atukatai kuna wenye nguvu watamega pakubwa na walio dhaifu watapata hata masalia lakini ni ajabu wakikosa hata chakukombeleza kisa keki yao yote inaliwa na watu wachache tena walewale.
 
Kuwa mtoto wa kiongozi sio dhambi,na wao wanastahili teuzi,na Wala sio wengi kiivyo,ndani ya serikali hii,yenye mawaziri na manaibu 52,watoto wa viongozi hawafiki 10,bunge Lina watu 252!watoto wa viongozi hawafiki 20!kwenye ma RC,DC,RAS,DAS,watu zaidi ya 120,watoto wa viongozi hawafiki 40!!sasa kelele za nini.
Ishu sio idadi ndogo, ishu ni je wanastahili kuliko wengine?
 
Mkuu ni kama umeamua tu kumtusi huyo mtu!

Ina maana wewe mfumo unaoendelea katika teuzi za vyeo vya maana vya juu hapa nchini hauuoni?

Kuna watu wanateuliwa kwa sifa ya visomo vya elimu yao hapo, ama kwa kushindanishwa na nani waweza kuthibitisha?

Chukulia mfano ulio hai, ni wazazi wangapi leo wanajikusuru kusomesha watoto wao na wakapata ufaulu na sifa sahihi za kufanya kazi, lakini mwisho wa siku wanazagaa mitaani bila chochote.

Majina ya viongozi kubakia maofisini milele, Nyerere, Nyerere Jnr, Kikwete, Kikwete Jnr, Mizengo, Mizengo Jnr nk nk, huo ni mfano tu, maana wapo wengine Identity wanaficha lakini wamo bila ya kuwa na sifa za maana kuwashinda waliopo mitaani.

Ni hoja ya msingi jamaa kasema, kuna upendeleo mkubwa wa wazi katika teuzi hizi, maana si teuzi za kuangalia sifa ya uongozi ama elimu ya mtu, ni kuangalia jina tu, jina ndiyo sifa ya kusogezwa nafasi za juu.

Kwa kuwa ni watoto wa vigogo, hata wafanye makosa ya kinidhamu ama ki jinai ya kuonekana katika nafasi hizo, wananchi mtazugwa katumbuliwa, hatumbuliwi kwa kuwajibishwa, ni mfano wa spare tyre kupumzishwa, muda wowote linapachikwa!

Sasa matendo haya huwa yanachochea chuki na matabaka katika jamii, pia kutoaminika kwa viongozi wakuu wanayotenda haya, kwa sababu kila mwenye akili timamu anaona.

Ifike wakati tukubali kwamba, umuhimu wa Katiba ni sasa, Katiba bora itakayoziba mianya ya upendeleo na kutuweka raia wote katika mizani sawa.
Kwa nchi za Africa utadubiri mpaka Jesu arudi kufanya ukombozi haki na usawa ni kitu adimu Tanzania
 
Pk na mu7 wanafanyaje nao

Huo ndiyo mfumo....

Mjiulize na mtafakari mtauvunjaje

Huo mfumo...

Na wewe ukifanikiwa kuuvunja huo mfumo utakuja kuendeleza mfumo huo huo

Huo ndiyo mfumo

Ova
Mfumo wa kuongoza nchi unapaswa kufuata katiba iliyoandikwa na wananchi wake kwa mizania na kufuatwa kwa ukamilifu na kila mtawala na raia wa nchi husika.

Na siyo suala la kutegemea utashi au hisia za kiongozi zitende kwa busara, suala ambalo haliwezekani maana binadamu kifilosophia ameumbwa na ubinafsi.
 
Kwamba uongozi ndo lengo la kusomesha watoto wako?wasipopata uongozi inakuwa umepata hasara?

Kwamba uongozi ni ulaji na unataka zamu ya ulaji Kwa watoto wako?

Hizo mentality Bora wakose kabisa uongozi hata wa mtaa...
Mentality za kijinga sana
Anaongea kwa uchungu as if its the only thing precious to become......
 
Lazima waendelee kutengeneza mfumo wazidi kuukamata
Wazidi kutawala...
Mara nyingi nawaambiaga ,na nyie paganeni muingie kwenye mfumo

Ova
Ili uingie kwenye mfumo lazima mfumo unaokuingiza wewe usiyenacho uwepo na uwe ni mfumo wazi na shindani lasivyo ikiwa kama taifa wasionacho ubaki kuwa wasio nacho nani ataikomboa jamii ambayo haikubahatika kujishkiza.
 
Sasa ungechambua jina moja moja na ukasema fulani ni mtoto wa fulani kuteuliwa kushika position fulani

Hiki ulichoandika kitawaacha wengi
Mdau inachosha kutaja majina ya watoto na ndugu za watafuna kodi za wananchi, maana hata ukiwataja haisaidii kwa maana tiyari ni wateule..kikubwa ni namna gani na sisi tunatoka hapa walipotutelekeza.
 
Inasaidie kuprove point yake kwanza then tuendelee kujadili namna ya kujinasua

Hivi hajaweka uchambuzi what if anatudanganya mkuu?
 
Back
Top Bottom