Teuzi mbalimbali kujaa majina ya watoto wa viongozi na vigogo Serikalini kama taifa tunaelekea wapi?

Nipo nawaza tu kama mwanangu nae ipo siku mtamkumbuka kwenye teuzi zenu ama ndiyo atakula kulingana na urefu wa kamba ya baba yake ilipoishia.

Kweli maisha kwa masikini ni ndoto isiyofikika, dunia uwanja wa vita na sisi ndiyo tunaopiganishwa, masikini mwenzangu hamka ukachakarike uitafutie familia mlo wa siku na ulipe kodi yao, kumbuka kuwa wapo wavuja jasho na wapo wanaofaidi matunda ya keki hiyo..bahati nikubahatika kuwa na mkono mrefu utafikiwa.

Walianza babu zao sasa wamemaliza mzunguko wa baba zao katika ufalme, picha linaashiria kabisa ni kuwa wazazi wanawapokeza mikoba watoto wao kurithi miliki wakati mwanangu namrithisha jembe la mkono na ardhi yenye ugumba kwa kukosa mbolea na pembejeo ni wazi wananing'ong'a.

Hata ile ada niliyotumia kumsomesha nikidhani ndiyo ukombozi nayo imeishia matumboni mwao hivi sasa wananikejeli tu wakinena kwa vinywa vyao vinavyonuka rushwa,upendeleo, ubinafsi na unafiki..ajira nichache mwambie mwanao ajiajiri aache uvivu mbona kazi ni nyingi tu graduate kafuge hata bata...huku bata la masaki hajui anachokula watabata kweli wanao haki kuna day watapata.. dunia ni njema ila walimwengu hawana maana.
Acha watu wa kwenye mfumo walambe asali tamu ndugu yangu.
 
ukipanda mabua utavuna mabua maisha unayopitia ivi leo ni matoke ya maisha waliopanda baba zako kwaiyo kubwa sio kulalamika kupambana na kumbuomba mungu watoto wako watatoboa tu ukiishi kwa kukata tamaa hutofanikiwa kwa jambo lolote manaa mungu wetu sisi ni wa rehema anasema anatuwazia mema kutupa tumaini siku zetu za mwisho tumtumaini bwana
 
Wazembe walikosa
Kwani waliopambania uhuru na vizazi vyao mpaka yakaja matawi mengine ya wachumia tumbo kwenye mfumo wao, walifanya hivyo ili tuwalipe kwa madaraka yasiyo na ukomo na kujilimbikizia mali nyingi wao tu na koo zao mpaka mwisho wa dunia?
 
Kama wapo akina Makonda kinachotakiwa ni uchapaji kazi ila kuna ambao wapo tu kwa kuwa ni wa vigogo na wenye uwezo wapo mtaani. Mimi ninaona kwa kuwa uongozi ni kipaji basi achukuliwe mtu yoyote mwenye kipaji.
 
Wa kulaumiwa ni babu na wazazi wako. Wakati kina Julius wanapigania uhuru wao walikuwa wanakunywa Chimpumu na kuzichakata papuchi za wake wa watu...

Kaza buti wanao wasije kulalamika kama wewe...
Hii ni spana balaa wakati tabata mpk kinyerezi....ni mapori matupu Kuna majaruba...

Wazee wetu walishindwa kutafuta connections za maana kuwezesha wao na familia zao kupata connection za kuinjoi keki ya taifa....

Enzi izo mbagala mpk kongowe na Kule chamazi ni mapori kina muogo mchungu wa kaole wanaenda kuigizia zile thamsilia za Kila jumamosi.... Bado yalikua mapori

Kwaio sis masikini wa Tz ambao ni 70% hatuna watu huko serikali kuu...makapuku 🤣🤣 wazazi wetu walikua hawana maono....yaan hizi ni spana balaa
Yaan 🤠🤠 hata kakiwanja na ka nyumba dar es salaam ukoo mzima hamna
Rai yangu Tupambane kutengeneza kesho nzuri za koo zetu na familia zetu

Nimeandika andika tu sijui hata nimeandika nini🤣🤣🤣🤣🤣😂😂😂😂
 
ukipanda mabua utavuna mabua maisha unayopitia ivi leo ni matoke ya maisha waliopanda baba zako kwaiyo kubwa sio kulalamika kupambana na kumbuomba mungu watoto wako watatoboa tu ukiishi kwa kukata tamaa hutofanikiwa kwa jambo lolote manaa mungu wetu sisi ni wa rehema anasema anatuwazia mema kutupa tumaini siku zetu za mwisho tumtumaini bwana

Amen! Siku zote penye nia pana njia na penye tumaini lolote lile linawezekana..ubarikiwe.
 
Mfumo wa kuongoza nchi unapaswa kufuata katiba iliyoandikwa na wananchi wake kwa mizania na kufuatwa kwa ukamilifu na kila mtawala na raia wa nchi husika.

Na siyo suala la kutegemea utashi au hisia za kiongozi zitende kwa busara, suala ambalo haliwezekani maana binadamu kifilosophia ameumbwa na ubinafsi.
Sisi,nchi za kiafrika hatufati hiyo

Ova
 
Nipo nawaza tu kama mwanangu nae ipo siku mtamkumbuka kwenye teuzi zenu ama ndiyo atakula kulingana na urefu wa kamba ya baba yake ilipoishia.

Kweli maisha kwa masikini ni ndoto isiyofikika, dunia uwanja wa vita na sisi ndiyo tunaopiganishwa, masikini mwenzangu hamka ukachakarike uitafutie familia mlo wa siku na ulipe kodi yao, kumbuka kuwa wapo wavuja jasho na wapo wanaofaidi matunda ya keki hiyo..bahati nikubahatika kuwa na mkono mrefu utafikiwa.

Walianza babu zao sasa wamemaliza mzunguko wa baba zao katika ufalme, picha linaashiria kabisa ni kuwa wazazi wanawapokeza mikoba watoto wao kurithi miliki wakati mwanangu namrithisha jembe la mkono na ardhi yenye ugumba kwa kukosa mbolea na pembejeo ni wazi wananing'ong'a.

Hata ile ada niliyotumia kumsomesha nikidhani ndiyo ukombozi nayo imeishia matumboni mwao hivi sasa wananikejeli tu wakinena kwa vinywa vyao vinavyonuka rushwa,upendeleo, ubinafsi na unafiki..ajira nichache mwambie mwanao ajiajiri aache uvivu mbona kazi ni nyingi tu graduate kafuge hata bata...huku bata la masaki hajui anachokula watabata kweli wanao haki kuna day watapata.. dunia ni njema ila walimwengu hawana maana.
maji ufuata mkondo hata uzunguni watoto wa watawala upata nafasi
 
Back
Top Bottom