Mkuu ni kama umeamua tu kumtusi huyo mtu!
Ina maana wewe mfumo unaoendelea katika teuzi za vyeo vya maana vya juu hapa nchini hauuoni?
Kuna watu wanateuliwa kwa sifa ya visomo vya elimu yao hapo, ama kwa kushindanishwa na nani waweza kuthibitisha?
Chukulia mfano ulio hai, ni wazazi wangapi leo wanajikusuru kusomesha watoto wao na wakapata ufaulu na sifa sahihi za kufanya kazi, lakini mwisho wa siku wanazagaa mitaani bila chochote.
Majina ya viongozi kubakia maofisini milele, Nyerere, Nyerere Jnr, Kikwete, Kikwete Jnr, Mizengo, Mizengo Jnr nk nk, huo ni mfano tu, maana wapo wengine Identity wanaficha lakini wamo bila ya kuwa na sifa za maana kuwashinda waliopo mitaani.
Ni hoja ya msingi jamaa kasema, kuna upendeleo mkubwa wa wazi katika teuzi hizi, maana si teuzi za kuangalia sifa ya uongozi ama elimu ya mtu, ni kuangalia jina tu, jina ndiyo sifa ya kusogezwa nafasi za juu.
Kwa kuwa ni watoto wa vigogo, hata wafanye makosa ya kinidhamu ama ki jinai ya kuonekana katika nafasi hizo, wananchi mtazugwa katumbuliwa, hatumbuliwi kwa kuwajibishwa, ni mfano wa spare tyre kupumzishwa, muda wowote linapachikwa!
Sasa matendo haya huwa yanachochea chuki na matabaka katika jamii, pia kutoaminika kwa viongozi wakuu wanayotenda haya, kwa sababu kila mwenye akili timamu anaona.
Ifike wakati tukubali kwamba, umuhimu wa Katiba ni sasa, Katiba bora itakayoziba mianya ya upendeleo na kutuweka raia wote katika mizani sawa.