Teuzi na Tenguzi za Viongozi Mabalimbali Zilizofanywa na Rais Wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (2005-2015)

Teuzi na Tenguzi za Viongozi Mabalimbali Zilizofanywa na Rais Wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (2005-2015)

Inabidi bunge na wabunge wapate somo kuwa kile walichosema ni uzushi mpaka kupelekea kutoa adhabu isiyostahili sasa rais kaona kina mantiki ingawa naye ameona kwa shinikizo kutoka kwa wananchi.

By the Way, inabidi karamagi na akina Kamfumu waombe radhi na hasa Karamagi aadhibiwe kwa kulidanganya bunge kuwa mapitio yameshakamilika wakati bosi wao kasema yalikuwa bado.

Raisi wetu pia inabidi ajifunze kuamua kwa wakati siyo maauzi yake yawe driven na malalamiko!
 
JK amteua Zitto kamati ya madini

Tanzania ni kutumia bongo.Miradi ni aina nyingi na ukitaka pesa wewe kuwa against na serikali lazima utanunuliwa tu kama alivyonunuliwa MWKJJ! Huyo Zitto sitashangaa kama hatanunuliwa na RICHMONDULI.
Yangu macho na masikio
 
Pia amezidisha maafisa wa serikalini. Badala yake angeongeza wajumbe utoka nje ya serikali. Naunga mkono kumshirikisha Prof. Shifji. Hata mimi simuamini bwana Mapesa. Dr. Mwakyembe pia anaonekana kuwa kigeugeu (kumbukeni alivyokuwa akitetea matatizo ya CUF na CCM kwenye muafaka aliposhirikishwa kwenye kamati ya muafaka wakati wa Mhes. Mkapa.

Tundu Lisu si muhimu kwani ataweza kumpatia ushauri bwana mdogo Zito. Ila, pia Mzee Mark Bomani sina uhakika naye sana kuendesha kamati hii. Bi Simba Kijo angefaa kushirikishwa pia.

Kama kuna watu wa karibu na Mheshimiwa Kikwete, basi watufikishie ujumbe.
 
"Mbunge wa Bariadi Mashariki, Chadema, John Cheyo." sio kweli. cheyo ni mbuge wa udp sio chadema.
sitashangaa kama wabunge hao wawil hawata shughulikiwa na el ra na muungwana kama walivyofanya kwa mwanakjj wa jf. wengine wote waliotajwa kwenye kamati ni wale wale waliotayarisha mikataba iliyopita.

hakuna aliye independent na wanafuata maagizo ya wizara(waziri) wao. mwenyekiti sijui ni nani asiyejua ni damu damu tangu enzi za kale. labda kamati hii tuite ze comedy!!

macinkus
 
Mimi nadhani hiyo kamati ingekuwa na objectivity zaidi kama na wajumbe wake wangekuwa hawana uhusiano ama connection yoyote na vitu vifuatavyo: madini, nishati, siasa na serikali. Cha msingi wawe wamebobea katika fani zao aidha wawe wasomi wetu toka vyuo vya elimu ya juu.

Yaani kamati hiyo ingekuwa kama vile jury zilivyo huru, halafu wawe na uwezo kwa kuwahoji wenye hisa na sekta ya madini na nishati bila kujali nyadhifa zao na hatimaye kuja na mapendekezo ambayo kweli yatafanyiwa kazi la sivyo zitakuwa talalila zile zile za kila siku.

Mwisho, kama tutampongeza Mheshimiwa Rais kwa hili basi tuandamane kumpongeza pia akikaa nchini miezi 6 bila kusafiri!
 
Hivi mbona nimeona huyo Mwakyembe kateuliwa tena kuchunguza RDC sasa atapata muda kweli? hakuna watu wengine?
 
Hivi mbona nimeona huyo Mwakyembe kateuliwa tena kuchunguza RDC sasa atapata muda kweli? hakuna watu wengine?

Hapo ndiyo inashangaza tena kwani jana hiyo hiyo ametajwa tena kamati ya richmond.There is no coordination between executive and parliament.Kila mmoja anapiga tiktaka kivyake.
 
Rais ametoa uwanja mpana sana kwa hii kamati ikiwemo kukusanya maoni kutoka kwa mtu au kikundi chochote. Sasa hii ndio nafasi ya JF na wengine wenye uzoefu au maoni ya maana kwenye suala la madini kuchangia.

Hapa ndipo tunaweza kutumia kuwepo kwa Zitto kule ambaye ni mwanachama mwenzetu kuweza kufikisha maoni yetu, of course kama yeye mwenyewe anakubaliana nayo.

Hapa ndipo watu kama akina Dr. Hamis wanaweza kumwaga cheche zao juu ya wapi tumekosea na tufanye nini ili kurekebisha.

Mimi wasiwasi wangu uko zaidi kwenye ku control pato ambalo hao wachimba madini wanapata. Hata kama tunapata asilimia inayofaa lakini kama wajanja wanatorosha madini kinyemelea utakuta hiyo asilimia haitatusaidia.

Kwahiyo kuna matatizo makuu mawili, je asilimia wanayotoa inatosha? na pili je tuna njia zipi za kuhakikisha hizo madini hazipakiwi kwenye containers kama mchanga na kwenda kupigwa bei huko nje?

Kwasasa nadhani haitakuwa rahisi tena kuongeza mjumbe kwenye hiyo kamati, muhimu ni kuwatumia wajumbe waliopo vizuri, kuwabana ili wajue tunawafuatilia na wakitusaliti watakuwa nao ni mafisadi na hatutawaachia, kuhakikisha hiyo kamati haigeuki kuwa mapambano ya CCM na upinzani. Inabid mambo waliyokubaliana watuambie na yale ambayo hawakukubaliana pia watuambie ili tujue nani katukwamisha huko.
 
Hapo ndiyo inashangaza tena kwani jana hiyo hiyo ametajwa tena kamati ya richmond.There is no coordination between executive and parliament.Kila mmoja anapiga tiktaka kivyake.


Mi namshauri ajitoe katika moja ya hizi kamati ili wawekwe watu wengine wenye uwezo kama wake au kumzidi, haina maana kabisa hata kama ni uhuru wa bunge na serikali ninapata wasi wasi na utendaji wa kiufanisi katika kamati mbili kwa wakati mmoja tena zenye kufuatilia mambo yanayofanana.
 
Hapo ndiyo inashangaza tena kwani jana hiyo hiyo ametajwa tena kamati ya richmond.There is no coordination between executive and parliament.Kila mmoja anapiga tiktaka kivyake.

Mimi sishangai,

Mimi naona hii kama ni uthibitisho kwamba kweli mihimili hii miwili inafanya kazi zake bila kuingiliana. Ninahakika Rais na Spika hawakufahamu kwamba kila mmoja alikuwa ateue kamati yake siku hiyo na wajumbe gani?

Kwa hiyo Spika aliona anamuhitaji mjumbe huyo, na wakati huo huo Rais naye akaona anamuhitaji na kilichotokea jina hilo likatokea mara mbili!

Tuamini kwamba viongozi hawa wanabusara wataliona hili na mmojawapo ataamua kumwondoa huyo mjumbe ili kazi zifanyike vizuri.
 
Quote: Mzee Mwanakijiji
sasa na wewe unalalamika nini? maana umezidi kulalamika kila ninachoandika au kufanya, na ikipita siku kwa wewe kutokulalamika kuhusu mimi huwa nashangaa!



Na wewe umezidi mno kushangaa. Ikipita siku hujashangaa kwa nini unashangaa sote humu hukushangaa

Yaani niecheka hadi ulimi umezama katika koromeo sasa nimekuwa Bubu originale
 
Babu,

Hapa kwa usanii ndipo penyewe, hao Ze Comedy hawaoni ndani. Bahati tu ya JF ni kwamba tunafaidi bure. Wasanii wetu hawahitaji pesa wala hawitaji kununuliwa na akina Lowassa au
RA.
 
i) Mpaka kieleweka et al.: Si kweli kwamba Issa Shivji na Tundu Lissu ndio watu pekee wanaoijua mikataba ya madini au wenye uchungu na Tanzania. Kwa hiyo mimi kutukuwepo hawa katika kamati sioni tatizo kabisa. Tuache kasumba ya kufikiri kwamba ni watu fulani katika jamii yetu wenye uwezo wa kufanya mambo, huo na ni utegemezi! Ile nchi ina watu mil 36 wenye vipaji mbalimbali. Watu wakipewa kazi, tuwasukumu na kuwatia moyo kuhakikisha wanafanya kazi ya vizuri.
ii) Ndio nasema kila siku kuwa nchi yetu ina uhaba wa mafanikio kiasi kwamba hata likitokea jambo dogo inabidi tushangilie kama mazuzu. Ndiyo tuliweza kubagawa hata Rashid kushinda mashindano ya BBA. Sasa na hili nalo sishangai. Lakini binaafsi, at the risk of being seen cynical, sioni cha kushangilia. Yaani mafanikio hapa ni nini hasa hadi tumsifu JK? Huyu mtu kuna siku tutamsifia hata atakapoamka mapema. Kosa la mikataba mibovu walifanya wao, sasa wanapochukua hatua za kurekebisha tena kwa shinikizo, sisi tunachosifia hapa ni kitu gani hasa? Tunamsifia baba kununua nepi za mwanae? Ndio kusema siku JK atakapoamua kuwatoa akina Karamagi itabidi tufanye maandamana ya kumpongeza, tuna wazimu au nini
?

..Good analysis Kitila. Nadhani wale vijana wa Mlimani miaka ile hawakukosea kukupatia uraisi wa daruso.
 
Tunaelekea kuwa Taifa la walalamikaji au namna gani?

Hello Kitila,

Kweli ndugu yangu nashukuru kwamba umeliona hili na kwa wale watakaochukua nchi 2010 mnatakiwa kuwaandaa wananchi wasiwe hivyo maana kama speed itaendelea kuwa hii mpaka 2010 mtakapokuwa mnachukua nchi, mtashindwa hata kuongoza kwa kuwa ndio ugonjwa huo utakuwa ushakuwa kidonda ndugu.

Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.
 
Kuna habari kwamba Iddi Simba ameongezwa katika kamaati ya Madini
 
Pia amezidisha maafisa wa serikalini. Badala yake angeongeza wajumbe utoka nje ya serikali. Naunga mkono kumshirikisha Prof. Shifji. Hata mimi simuamini bwana Mapesa. Dr. Mwakyembe pia anaonekana kuwa kigeugeu (kumbukeni alivyokuwa akitetea matatizo ya CUF na CCM kwenye muafaka aliposhirikishwa kwenye kamati ya muafaka wakati wa Mhes. Mkapa.

Tundu Lisu si muhimu kwani ataweza kumpatia ushauri bwana mdogo Zito. Ila, pia Mzee Mark Bomani sina uhakika naye sana kuendesha kamati hii. Bi Simba Kijo angefaa kushirikishwa pia.

Kama kuna watu wa karibu na Mheshimiwa Kikwete, basi watufikishie ujumbe.

tukishamfikishia ujumbe then what? kamati ishatangazwa unataka aivunje tena? si ndo mtamuona hana msimamo na hajui anachofanya? Kama ni mtego tayari washajitega lets wait n c what will kam out of that kamati. btw mh zitto kazi unayo ku-prove kwa wananchi kwamba imani waliyo nayo kwako ni sahihi. be carefully coz among wote waloteuliwa inaonekana watu wanaamini wewe peke yako hutanunulika kirahisi.all the best
 
Lakini si vibaya jamii pia ikawa na mapendekezo yao imradi pawepo hoja. Prof. Shivji au Mama Kijo bi Simba anafaa kuongezwa.

Pia tukumbuke kuwa mheshimiwa aliahidi kushirikisha serikali, wabunge wa CCM, wabunge wa upinani, wanasheria, wasomi (academicians) wawakilishi wa dini, NGO's na kadharika. Samahani mimi nimeona Wabunge wa CCM, wabunge wa Upinzani, maafisa wa serikali na wanachama wa CCM (Jaji Mark Bomani. Kwa hiyo kwa haraka haraka wasiotoka openly CCM ni wawili tu, sasa kwa nini tuite kamati ya Kitaifa???? Kuna makundi ya kijamii mangapi Tanzania yaliyo rasimi mpaka zaidi ya asilimia 70 wawakilishe CCM????

Naunga mkuna kutumia vyombo vya habari kupendekeza majina machache wanaoweza kuongezwa kwenye kamati, angalau wawili au watatu.

Pia muda wa miezi mitatu hautoshi kupitia mikataba na sheria zinazo simamia mali asili ya madini. Kama wao wametumi miaka miwili na hakuna walicho kuna nacho zaidi ya kusaini mkataba mwigine wa Buzwagi ni nini??? angalau awape miezi sita ili wapate muda wa kutosha kutembelea nchi zingine za kutosha ili kujiridhisha na taarifa itakayo tolewa.

Tusifanye mzaha, huu ndiyo nafasi pekee tusifanye mambo nusu nusu.
 
Jakaya na kisa cha mfuga mbwa

jhgf342fgdzj4.jpg


Credit mjengwa blog
 
Back
Top Bottom