Teuzi na Tenguzi za Viongozi Mabalimbali Zilizofanywa na Rais Wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (2005-2015)

Teuzi na Tenguzi za Viongozi Mabalimbali Zilizofanywa na Rais Wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (2005-2015)

Mwafrika,

Huyu mtu ni kituko sana hapa Jf,hataki kuona watu wanatoa maoni ingawa watu wamemvumilia sana na kumpa uhuru wa kumwaga upupu wake hapa siku zote hadi kwa sababau tu walijali uhuru wa kutoa mawazo.

Tangu ajifunze kutype amekua akiwashwa sana,kila thread anayochangia ni upuuzi tu lakini hatukujali kwani pia tulitambua uwepo wa watu walio na nerves zenye kasoro.

Tumkome nyani sasa! Tukate ishus mpaka kieleweke!

wapi nimetaka watu wasitoe maoni ?
nashukuru kwa kunivumilia
uhuru huo huo ninaoutumia mie ndio uhuru huo huo unaoutumia wewe kumwaga upupu wako !
ni kweli tangu nijifunze kutype nimekuwa nikiwashwa kutype, !
kila thread ninayochangia ni upuuzi ni kweli, kwa maoni yako na imani yako !
hongera kwa kutambua uwepo wa watu JF ! maana watu ndio JF na si vinginevyo !

baab kubwa ! tukate ishuz !
 
Wana JF nadhani tufike mahali tutumie Busara. Tukitaka kila mtu awepo kwenye kamati basi kutakuwa na watu wengi saaana.

Busara walionayo baadhi ya wanaJF ni kutoridhika na uteuzi wa baadhi ya watu either kwa kuwafahamu utendaji waji uliopita au kwa kuhisi vinginenvyo.Wao hawajasema kila mtu aingie kwenye kamati ila wanasema kwanini kama mambo haya niya sheria yasichukue zaidi watu waliobobea kwenye hiyo kamati.Na si lazima wawe wabunge kwani huko ndo walioikataa.
 
Busara walionayo baadhi ya wanaJF ni kutoridhika na uteuzi wa baadhi ya watu either kwa kuwafahamu utendaji waji uliopita au kwa kuhisi vinginenvyo.Wao hawajasema kila mtu aingie kwenye kamati ila wanasema kwanini kama mambo haya niya sheria yasichukue zaidi watu waliobobea kwenye hiyo kamati.Na si lazima wawe wabunge kwani huko ndo walioikataa.


Nyangumi, Tume ya Rais haikuhitaji Wabunge kabisa, period. Ilihitaji wataalamu na wasomi kwani msingi wake ulikuwa ni katika sheria na taratibu. Siyo tume ya uchunguzi. Hivyo kungekuwa na wasomi wa sheria za Kimataifa, Mikataba ya Biashara, n.k
 
napendekeza mheshimiwa ZITTO ajitoe kwenye hiyo kamati ilikulinda heshima yake na upinzani kwa ujumla.kwenye hiyo kamati hakuna jipya zaindi ya kummaliza zitto na upinzani kwa ujumla.


Mie nakubaliana na hisiazako lakini natofautiana na issue ya Zitto kujiuzuru.Nia yao nikutaka baadaye wajewaseme yako wapi sasa tulimuweka Zitto kwenye hiyo kamati.

Mh Zitto,
Kuwa makini,hutafanyikiwa ikiwa lango lenu kati ya wajumbe litakuwa tofauti.Kazi yako itakuwa ngumu kama malengo yenu yatakuwa tofauti,ila fanya kazi ambayo nia yako ilitaka kuitimiza kwa watanzania.Pale utakapopata vikwazo nukuu(na siku hizi kuna visound recorder vidogo, kuwa nacho)Hata kama katika kuwajibika utatofautiana na wajumbe wenzako weka kumbukumbu na ikiwa too much, mueleze Mwajiri wako(JK).Kama yeye hata sikiliza na unahakika kutofanya marekebisho hakutaboresha basi jiuzuru na waambie watanzania sababu za kujitoa ila sio sasa.
 
ukiangalia kwa umakini, hiyo kamati haina tatizo kwani ina watu wenye upeo from different angle, i.e political na Technical, baadhi ya watu kama David Tarimo wamekuwa wakiangalia na kutafiti suala la madini kwa muda mrefu hapa Tanzania kabla hata ya Zito kuibua issue (political agenda) at public interest at the right time,

hivyo wakati utasema kama kamati imeharibu au la,

na tusubiri
 
..We need a new direction in our Mining Sector.

..Tunaelekea kuwa kama Nigeria. Wao wanachimba mafuta lakini hawana Rifenery. Vilevile foleni za mafuta ni jambo la kawaida Nigeria.

..Hao wateule wa Raisi tungependa tujue wasifu wao wa kazi. Huenda hawana ujuzi wala uzoefu wa kuchunguza mikataba yetu ya madini.

..Kwa mtizamo wangu mikataba ya Madini siyo mibaya Kisheria, ni mibaya Kiuchumi. Tuelekeze kurunzi letu kwa waliopanga bei ya madini yetu.

..Wadau wakishapatana bei ndipo huenda kwa wanasheria kuandikiwa mikataba. Ukiamua kuuza kwa bei mbaya, hasara ni jambo la uhakika. Usitegemee Mwanasheria akusaidie kwa mazingaombwe upate faida.
 
kamati ina wajumbe wenye upeo tofauti na maono lakini yenye mwisho mmoja katika public interest ya watanzania,hatutegemei political agenda zikashinda technical input
kuna mtu kama David Tarimo ameshafanya utafiti mkubwa sana kuhusu madini ya Tanzania yanamnufaishaje mtanzania kabla hata ya Zitto kuibuka na issue kama political agenda yenye 100% public interest with right timing,
wafanye kazi tuone, ulalamishi kwa kila kitu ni issue ita dilute fact na mategemeo ya watanzania
 
PRESS SECRETARY TO THE PRESIDENT
OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

The State House,

P.O. Box 9120,
Tel: 255-22-2116539/2116913
Fax. No. 255-22 2113425 DAR ES SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz Tanzania.
ikulumawasiliano@yahoo.com


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Kikwete amemteua na kumwongeza Mhe. Iddi Simba kuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya kuangalia upya mikataba ya uchimbaji wa madini, Kamati ambayo iko chini ya Uenyekiti wa Mhe. Mark Bomani.

Mhe. Iddi Simba ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Ilala.

Wajumbe wengine waliokwisha teuliwa ni:

Mhe. John Momose Cheyo (Mbunge) - Bariadi Mashariki (UDP) - Mjumbe

Mhe. Zuberi Zitto Kabwe (Mbunge) - Kigoma Kaskazini (CHADEMA) - Mjumbe

Mhe. Dkt. Harrison George Mwakyembe (Mbunge) - Kyela (CCM) - Mjumbe

Mhe. Ezekiel Magolyo Maige (Mbunge) - Msalala (CCM) - Mjumbe

Bw. Peter L. Machunde - Soko la Hisa, DSM (DSE) - Mjumbe

Bw. David Tarimo - PriceWater Coopers - Mjumbe

Bi Maria N. Kejo - Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa Wizara ya Katiba na Sheria) - Mjumbe

Bi. Salome Makange - Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini - Mjumbe

Bw. Mugisha Kamugisha - Kamishna wa Sera Wizara ya Fedha - Mjumbe

Bw. Edward Kihundwa - Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi - Mjumbe


Ikulu,
DAR ES SALAAM.

14/11/2007
 
Tatizo letu ni kuwa hawa wasoni njaa wetu linapotokea tatizo huwa wanajificha na kukaa kimya kanakwamba hakuna kilichotokea ktk nchi yetu.Wengi watakubaliana na mimi kuwa vyombo vingi vya ulya na marekani huwa tunawaona wasomi wa taaliuma mbalimbali wakichambua mambo mbalimbali ilikuwaelimisha wananchi ni kitugani hasa kimetokea na nini hatua za kufanya ili kuboresha au vinginevyo.lakini kwa bongo swala la kitaaluma wataachiwa wanasiasa,wakitoka nje basi ni shivji au lissu.
Sasa hivi imetokea lileswala la moi hatujasikia watalaamu wa kibongo wakiliongelea kitaaluma zaidi ya kujificha kama hakuna kilichotokea.
 
BAADHI ya wanasiasa na wasomi wameunga mkono uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuunda na kuteua wajumbe Kamati ya kupitia upya mikataba ya uchimbaji wa madini wakiwemo wajumbe kutoka kambi ya upinzani.

Mbunge wa Karatu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk Willibrod Slaa, aliunga hatua ya Rais Kikwete ya kuunda kamati hiyo kwa kuwa
ametekeleza haraka ahadi aliyoitoa hivi karbuni

Hata hivyo, alisema ana wasiwasi wa utekelezaji wa ripoti ya kamati akisema kuwa kamati hiyo inayoongozwa na Jaji Mark Bomani si ya kwanza kuundwa na serikali
nchini kushughulikia mambo yanayogusa maslahi ya umma.

��Hii ni tume ya nne, lakini hakuna utekelezaji,�� alisema Dk Slaa.

Alisema kuundwa kwa kamati hiyo hakumaanishi kwamba tuhuma mbalimbali, zikiwamo za ufisadi walizozitoa dhidi ya vigogo kumi na moja wa serikali zimefutika.

��Suala la madini, ni sehemu ndogo sana katika yote tuliyoyaeleza. Sasa kinachotakiwa Rais asiishie hapo tu, ashughulikie tuhuma zetu pia,�� alisema Dk Slaa.

Mbunge wa Longido (CCM), Michael Lekule Laizer alisema amefurahishwa na hatua hiyo ya Rais Kikwete kwani itasaidia tuhuma zote zilizotolewa katika madini kupata
ukweli wake, badala ya watu kuachwa wakiendelea kupiga kelele kila siku.

��Nadhani serikali imeanza kutambua vilio vya wananchi. Hilo ni muhimu kwani litaondoa manung��uniko. Na nimefurahishwa na muundo wa kamati ambayo itakuwa
ni muungano wa wajumbe kutoka vyama vyote,�� alisema Laizer.

Naye Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Mgana Msindai alisema anaunga mkono kamati hiyo kwa kuwa italisaidia Bunge kujua mambo yaliyomo kwenye mkataba wa uchimbaji madini katika Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, ulioko Kahama, mkoani Shinyanga.

��Pia naunga mkono kamati kuwa na wajumbe kutoka upinzani, itaondoa utata kwa wabunge na pia ni haki kwa wapinzani kuteuliwa katika kamati,�� alisema Msindai.

Naye Mwenyekiti wa Chama caha Tanzania Labour (TLP), alisema hatua ya rais kumteua, Zitto Kabwe imeonyesha kuwadhalilisha wabunge kutokana na hatua yao ya kumsimamisha mbunge huyo kuhudhuria vikao hivyo.

Mrema alisema Kikwete ameonyesha ujasiri mkubwa ambao wabunge wa CCM walishindwa kuufanya, hivyo wameumbuka kwa kitendo walichokifanya.

��Hii ni aibu kubwa kwa Bunge letu, mtu mnayemsimamisha ndiye anakuwa kinara katika kamati ya uchunguzi, Kikwete anastahili pongezi kwani ameweza kutetea maslahi ya taifa bila kuangalia tofauti za vyama,�� alisema Mrema na kuongeza kuwa katika maslahi ya Taifa lazima kusimama kwa pamoja na kuacha tofauti zilizopo.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa hatua ya kuunda tume hiyo inaweza kuzuia ufisadi unaoendelea katika sekta ya madini ambao alidai kuwa ni watu wachache tu wanaofaidika huku Watanzania wengi wakiwa katika hali mbaya.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila alishauri Tume hiyo kupewa uwezo zaidi badala ya jukumu la kutoa mapendekezo pekee.

Alisema kumekuwa na Tume nyingi zilishowahi kuundwa nchini kwa kutumia pesa nyingi ambazo ni kodi za wananchi, lakini matokeo yake yanakuwa ni kiini macho kutokana na ripoti zake kufungiwa kwenye makabati.

Hata hivyo, Mchungaji Mtikila aliitaka kamati hiyo kufanya kazi yake kwa uwazi mkubwa na kutoruhusu kuingiliwa katika maamuzi yake ili kuhakikisha mafisadi wote waliohusika kuwekwa hadharani.

Wakati huo huo, taasisi ya Utafiti na Tathmini ya rasilimali ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (IRA) imeipongeza kamati hiyo ikisema kuwa imeundwa wakati muafaka na kuwahusisha watu muhimu.

Mmoja wa wakurugenzi wa IRA ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini alisema kamati hiyo imetoa sura mbili kwa serikali.

Alisema sura ya kwanza ni serikali kutokuwa makini na kufanya mambo kwa msukumo wa wanasiasa na ya pili ni dhamira ya dhati ya rais kushughulikia tatizo la mikataba ya madini.

Hata hivyo alisema katika sura yoyote ambayo mtu angependa kuipokea, kuundwa kwa kamati hiyo ni changamoto kwa wanasiasa hasa wapinzani ambao sasa wanatakiwa kujipanga ili waje na agenda mpya.

"Hapa maana yake amemaliza mjadala wa madini, wapinzani wanatakiwa kujipanga upya kwa kutafuta agenda mpya," alisema.

Katika hatua nyingne, Mbunge wa Tarime (Chadema), Chacha Wangwe, aliipinga kamati hiyo Zitto, kujitoa kwenye kamati hiyo.

Alisema anapinga suala hilo kwa madai kwamba, kuundwa kwa kamati hiyo kumelenga kudhoofisha hoja ya msingi ya wapinzani ya kutaka sheria ya madini ifutwe kabla ya kwenda katika hatua ya pili ya kujadili mikataba.

��Kizingiti kikubwa ni sheria, ndio haijakaa vizuri. Hivyo, kilichotakiwa ni sheria kufutwa kwanza halafu ndio tuzungumze mikataba mipya,�� alisema Wangwe.

Alisema mbali na hilo, ana wasiwasi kamati iliyoundwa na Rais Kikwete haitakuwa na tofauti na kamati zilizopita, kama vile ya Brigedia Mang��enya, Jenerali Mboma na Dk
Kipokola ambazo alisema hazikubadilisha lolote, badala yake baadhi ya makampuni ya uchimbaji madini, yameendelea kupora madini ya Watanzania.

Wangwe alisema wasiwasi wake unatiwa nguvu na baadhi ya watu walioteuliwa katika kamati hiyo ambao alisema ni walewale waliohusika kutengeneza sera mbovu, mawakili
wa serikali na wachumi wanaoishauri vibaya serikali.

��Ndio hao hao wamerudishwa kuishauri tena serikali katika suala la madini, ni ushauri gani watautoa?,�� alihoji Wangwe.

Juzi Rais Jakaya Kikwete aliunda kamati ya kupitia upya mikataba ya uchimbaji madini na kuteua wajumbe kumi akiwamo Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.

Kamati hiyo inayoongozwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu, Jaji Mark Bomani, Wajumbe wengine ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishina wa Sera Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa na Mbunge wa Kyela (CCM) na Dk. Harrison Mwakyembe.

Wengine ni Mbunge wa Msalala (CCM),Ezekiel Maige, Peter Machunde kutoka Soko la Hisa, Dar es Salaam (DSE), Mkaguzi wa Mahesabu kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Mahesabu, Price Water Coopers, David Tarimo ambaye ni mtaalam wa masuala ya kodi na Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo.

Habari hii imendikwa na Muhibu Said, Kizitto Noya na Tausi Mbowe

Source: Mwananchi
 
kamati ya kuangalia upya mikataba ya madini...i dont get it
 
nampongeza Rais kwa kuteua kamati huru wajumbe wengi ni wale wenye msimamo tunawafahamu .Naamini watasaidia Taifa kujua ukweli katika kamanyola hii
 
Monday, October 1, 2007
SAKATA LA ZITTO:

Karamagi amuingiza Kikwete

Serikali yazidi kuanikwa

· Karamagi alisaini mkataba akiwa peke yake
· Ajaribu kumwingiza Rais Kikwete
· Masilingi, Mwakyembe, wambana mbavu
· Mudhihiri alalamika, "Ninatumiwa lakini…"


Na Saed Kubenea

SAKATA la Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi la kusainia mkataba wa madini nje ya nchi, liliibua mtafaruku mkubwa ndani ya Kamati ya Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), MwanaHALISI limeelezwa.
Wabunge wengi waliopata fursa ya kuchangia, walimbana Karamagi aeleze hasa kilichotokea kuhusiana na kusaini mkataba.
Kikao cha wabunge wa CCM kilifanyika siku mbili baada ya Bunge kumsimamisha Zitto Kabwe kuhudhuria mikutano ya Bunge hadi Januari mwakani. Kabwe ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Taarifa kutoka ndani ya kikao zinasema alipoanza kujieleza, Karamagi alionekana kama anayetaka kumhusisha Rais Kikwete, lakini ghafla akakaa kimya.
Hiyo ilikuwa baada ya kuulizwa iwapo Rais Kikwete alikuwa anajua jambo hilo. Hata hivyo baadhi ya wabunge walishikilia kutaka kujua nafasi ya rais katika sakata hilo.
MwanaHALISI limeambiwa kuwa awali, Karamagi alikieleza kikao kuwa alimuanga Rais Kikwete kwamba anakwenda kukutana na wamiliki wa kampuni hiyo.
Hapo ndipo palizua kasheshe. Wabunge walihoji, mara hii kwa kutoa macho, "Je rais alijuajie kama Karamagi alikuwa anakwenda kusaini mkataba wakati alimuanga anakwenda kukutana tu na wamiliki?"
Taarifa zinasema alikuwa ni, Dk. Harisson Mwakyembe, mbunge wa Kyera na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Biashara na Uwekezaji, aliyesimama na kumtaka Waziri Karamagi kusema ukweli juu ya sakata zima lilivyokuwa.
Gazeti hili limedokezwa kwamba Mwakyembe alisema mbele yawabunge wenzake kuwa Karamagi hajawahi kuiambia kamati yake juu ya kusaini mkataba na yeye, Karamagi hakuzungumzia suala hilo hata katika bajeti ya wizara yake.
"Nje tumelimaliza. Ndani atueleze ilikuwaje? Mimi ni Makamu Mwenyekiti (Kamati ya Bunge ya Biashara na Uwekezaji). Ndani ya kamati yetu hatujui hili. Hajatueleza," amenukuliwa Mwakyembe akisema.
Taarifa zinasema Mwakyembe alihoji hata uamuzi wa kusainia mkataba huo hotelini badala ya ubalozini.
Alisema hata kama mkataba huo ulisainiwa hotelini kwa bahati mbaya, lakini mbona kuna taarifa kwamba hakukuwa na hata ofisa mmoja wa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, wakati wa utiaji saini.
Chanzo chetu cha habari kinasema kauli ya Mwakyembe ilitanguliwa na malalamimiko ya Mudhihir Mudhihir, mbunge wa Mchinga, ambaye alimlalamikia Karamagi akisema, "Si mtu mwenye shukurani."
"Mheshimiwa mwenyekiti, mimi nimekuwa kinga kwa muda mrefu. Nimekuwa nikilinda chama chetu. Lakini hakuna shukurani. Huu ni uungwana kweli," alisema mtoa habari akimnukuu Mudhihir.
Chanzo chetu cha habari kinasema Mudhihir alilalama, "Nimechoka kutumika. Huyu Bwana Karamagi kabla ya sijasimama bungeni kumtetea, alikuwa ananipigia simu mara kadhaa na hata kunitembelea nyumbani kwangu.
"Lakini sasa hata nikimpigia simu hapokei. Jamani huu ni uungwana?" aliuliza Mudhihir.
Ni Mudhihir aliyewasilisha hoja ya kumbana Zitto hadi bunge kufikia uamuzi wa kumsimamisha vikao vya bunge hadi Januari mwakani kwa madai ya "kusema uwongo" dhidi ya Karamagi.
Zitto atakuwa akipata nusu mshahara kwa mwezi kwa kipindi chote.
Taarifa za ndani ya kikao cha wabunge wa CCM zinasema, aliyepinga adhabu ya Zitto waziwazi, ni Wilson Masilingi, Mbunge wa Muleba Kusini. Alisema adhabu iliyotolewa haikuwa sahihi.
Masilingi alitoa msimamo huo baada ya makubaliano ya kikao kuwa iundwe "tume" ambayo itapita kwenye vyombo vya habari kutetea hoja ya bunge ya kumfungia Zitto.
MwanaHALISI inazo habari kwamba tume hiyo iliundwa na tayari imeanza kazi. Tume iko chini ya uenyekiti wa Naibu Spika, Anna Makinda.
Habari zinasema wajumbe wengine ni, Wilson Masilingi, Manju Msabya (Kigoma Kusini), Adam Malima (Mkuranga) na Mudhihir Mudhiri (Mchinga).
Hata hivyo, kwa mujibu wa habari hizo, Masilingi alisema kazi ya kuzuia moto wa wananchi itakuwa ngumu kutokana na suala zima kutawaliwa na utata.
"Mheshimiwa Mwenyekiti, mkataba wenyewe siujui. Yanayozungumzwa yana wingu zito. Nikiulizwa na waandishi wa habari je, umewahi kuuona huo mkataba unaoutetea, nitasemaje?" alisema mtoa habari akimnukuu Masilingi.
Aliongeza, "Suala limekwenda katika hali ya usiri. Hakuna uwazi, hakuna tunachokijua. Ni usiri juu ya usiri."
Masilingi ambaye kitaaluma ni mwanasheria aliwahi pia kuwa Waziri wa Utawala Bora, katika serikali ya Benjamin Mkapa.
Akionyesha kupinga adhabu dhidi ya Zitto, Masilingi alisema, "Kwanza, kilichokuwa mbele ya Bunge ilikuwa ni hoja ya kuunda kamati teule ya Bunge ya kuchunguza mkataba huu. Huwezi kuamua hoja juu ya hoja."
"Hapa ilikuwa ama kuunda kamati teule au kuliachia suala hili. Lakini badala ya kupiga kura kukata uamuzi wa kuunda kamati, tunapiga kura kumfungia mbunge. Hili si sahihi," amenukuliwa Masilingi akinasihi wenzake kistaarabu.
Taarifa toka kikaoni zinasema mbunge wa Kahama ambako ndiko uliko mradi huo, James Lembeli, alililamika kwamba hajawahi kuelezwa na Karamagi juu ya kuwapo kwa mradi huo.
Wapo pia baadhi ya wabunge walioonyesha mashaka yao juu ya busara iliyotumika.
Wengi walihoji iwapo suala la mfanyabiashara Reginald Mengi na mbunge wa Mkuranga, Adam Malima liliudiwa tume ya bunge, kwa nini hili limeshindwa kuundiwa tume.
Wachunguzi wa mambo wanasema ni uamuzi wa Kamati ya CCM wa kuunda tume ndio ulisababisha Katibu wa Bunge Damian Foka, kutoa taarifa kwa vyombo vya habari akizuia wananchi na asasi za kijamii kulalamikia maamuzi ya bunge juu ya Zitto.
Lakini kilichowaacha hoi wajumbe wengi, yalikuwa ni majibu ya Karamagi kwa madai ya Mudhihir.
Karamagi alisema ameshindwa kupokea simu za Mudhihir kwa kuwa amebanwa na kazi za kuandaa nyaraka za kikao cha Baraza la Mawaziri, mtoa habari amelieleza gazeti hili.
Majibu haya, hata hivyo, hayakuwafurahisha wabunge wengi. Mmoja wao amenukuliwa akisema "Ni kawaida ya baadhi ya mawaziri kujitia kiburi na hata kubadilisha simu."
Zitto aliwasilisha hoja binafsi bungeni akitaka Bunge liunde kamati teule kuchunguza hatua ya waziri Karamagi kusainia mkataba nje ya nchi.
Katika majibu yake bungeni, Karamagi alidai kwamba serikali isingeweza kuacha nafasi ya kusaini mkataba ipotee, ikiwa na maana kwamba wawekezaji huenda wangebadilisha mawazo.
Hoja hiyo, badala ya kuzima moto iliuwasha na kuibua maswali mengine mengi.
Je, ni serikali iliyowaomba wawekezaji hawa kuja nchini na sasa wanaweka masharti kuwa watawekeza tu ikiwa mkataba utasainiwa kabla ya mwisho wa Machi?
Lakini si wawekezaji wenyewe ni Barrick Gold Mines ambao wapo nchini tayari?
Je, si walikuwa wanajua kuwa serikali inapitia upya taratibu za mikataba? Je, walitaka waingie mkataba mpya kwa utaratibu wa zamani?
Je, hata hii juhudi ya serikali "kuwashawishi" wawekezaji hawa kubadilisha vipengele kadhaa vya mikataba hiyo, si itagonga mwamba?
Kwa nini ripoti ya mazingira haikutiliwa maanani? Je, iwapo ikigundulika baadaye kuwa mradi huo ni hatari kwa mazingira, serikali itajinasua vipi kama siyo kwa gharama kubwa au kushindwa hata kuchukua hatua yoyote?
Je, kwa nini Karamagi hakuweza kutoa taarifa yoyote kwa Kamati ya Buge ya Biashara na Uwekezaji juu ya mradi huo tangu Februari iliposaini mkataba hadi alipobanwa mbavu?
MwanaHALISI linaendelea kufuatilia mfumuko wa taarifa juu ya suala hili nyeti.
 
mzee wa nchi katega kitendawili 4 psychologists to focus what gonna happen, to me this is not a suprise and this does not bar the committee to recommend some this is the way to flash people's injured minds.But we have to wait coz no research no right to speak,lets pray that kabwe may not be eye blinded.
 
Msishangilie kuwekwa kwa Zitto humo. Kama mnakumbuka JK alivyosema, tatizo sio mikataba ya madini, tatizo ni sheria zetu tulizojiwekea, HIZI SHERIA ZIMEPITWA NA WAKATI.

..mkuu FD,

..kwahiyo unaniambia pamoja na kujua kwamba nyama imeoza bado tumeenda jikoni na kutengeneza supu? yaani,hatukuwa na subra kabisaa!kuona kwamba tunasuburi hadi nyama fresh ije ili tujinome?

..ama kweli,ukitaka kula na kipofu,usimguse mkono!
 
Kwa mtaji huo, anapewa immunity! I am sure she was the designer if not the endorser of Buzwagi contract itself.

Mwambieni Mnyika na Zitto waliongelee hili kwenye chama chao. Hamna haja ya kuona aibu au kuogopa. Zitto should not set his foot into the kamati if any of the members appointed has been associated with any Ufisadi issue or a Fisadi.

Hivyo on the List we have Maria Kejo, I hear Mwakyembe (give us extensive details MK) and someone who was employed by Karamagi!

Let's discect each member, including Zitto if we are to get anywhere and let us make these people and their laundry public and let the Wapiga Kura wa taifa waamue je ni mazingaombwe au ni wivu wa kike wa wapinzani!

This time around, we should not allow JK and his cronies fool us again.


Rev Kishoka:

I have read you loud and clear. Some people can be fooled for some time but not all the people all the time. Msimamo wangu kuhusu JK kuhusisha wapinzani kwenye hii kamati nilishautoa mara baada ya Kikwete kuzungumza kwenye mkutano mkuu wa chama chake. Na wapo walionipinga, nikautolea ufafanuzi zaidi mahali pengine, baadhi ya niliyoyasema yameanza kusemwa sasa baada ya Zitto kuteuliwa na wasifu wa wajumbe wengine kwenye kamati kuanza kujadiliwa. Ukipenda naweza kuweka hapa nini nilisema huko nyuma na nadhani chombo kimoja cha habari kilinukuu kidogo sehemu ndogo ya maoni yangu. Natofautiana na wanaopinga Zitto kushiriki kwenye kamati; ni vyema akashiriki ili kuthibitisha USANII wao akiwa ndani, cha msingi ni yeye kuendelea kuwa na msimamo. Binafsi naamini huu ni usanii mwingine tu, kwa nje ni sifa kuwa Rais amekuchukua hatua lakini kwa mlolongo wa matukio hiki ni kiini macho kingine. Ni kweli sisi kama chama tunapaswa kujadili. Nimevutiwa na uchambuzi wako kuhusu wajumbe walioteuliwe, na uchambuzi wa Mwafrika wa Kike, DUA na wengineo. Sina wasaa wa kuchukua michango yote na kuichambua kuiweka kama dossier moja kuhusu background ya wajumbe wote wa tume hii. Ningefurahi sana kama Mwafrika wa Kike akiniwekea muktasari wa hoja zote za msingi zilizotolewa kuhusiana na wajumbe wa Kamati na kutunitumia kwenye mnyika@yahoo.com ili tuifanyie kazi.

At the same time, ukirejea hotuba ya Rais Dodoma makundi mbalimbali aliyoahidi kuyashirikisha kwenye kamati mathalani wasomi(kwa maana ya kutoka academic institututions) na asasi za Kijamii(mathalani LEAT, LHRC nk) hazikushirikishwa. Hii ina maana ahadi yake hajaitimiza kwa ukamilifu wake.

Wakati huo huo kwenye hadidu rejea masuala ya haki za binadamu na mazingira katika maeneo yenye migodi hayajaguswa kwa ukamilifu wake.

Kuna haja pia ya kuhakikisha ripoti ya kamati hii inakuwa public, miezi mitatu si mingi sana. Ni vyema mjadala wa umma ukaendelea kwa kishindo.

Kamati ifanye kazi yake kwa uwazi, na ni vyema ikaanzia kwanza kwa kupitia kamati za nyuma kuhusu madini kama ile ya Mboma, ya Mang'enya, Kipokola, Masha nk- jambo hili nililisisitiza siku kadhaa nyuma nalirudia tena. It is a waste of resources kwamba ndani ya miaka isiyozidi sita tumeunda kamati nne katika suala hilo hilo.

Masuala ya msingi yanajulikana kwa kweli- ushiriki katika umiliki, uboreshaji wa mfumo wa kodi nk; kinachokosekana ni nia ya kisiasa. Na kinachochangia hali hii kwa kweli nadiriki kusema ni UFISADI! Lakini kila wakati tunakwepa chanzo cha msingi tunakimbilia kukabiliana na matokeo na tunakimbilia kufunika mijadala ya umma. Tunasahau kwamba kufukapo moshi ndipo moto utakapowaka

JJ
 
Dar Si Lamu

tumia uhuru wako babu !

ntakupeleka Kantucornia, uliza popyulesheni yake ni ngapi ? Moja.
uliza nani atakuwa mwenzako huko ?.............
 
Back
Top Bottom