JK amteua Zitto kamati ya madini
Hivi mbona nimeona huyo Mwakyembe kateuliwa tena kuchunguza RDC sasa atapata muda kweli? hakuna watu wengine?
Hapo ndiyo inashangaza tena kwani jana hiyo hiyo ametajwa tena kamati ya richmond.There is no coordination between executive and parliament.Kila mmoja anapiga tiktaka kivyake.
Hapo ndiyo inashangaza tena kwani jana hiyo hiyo ametajwa tena kamati ya richmond.There is no coordination between executive and parliament.Kila mmoja anapiga tiktaka kivyake.
Na wewe umezidi mno kushangaa. Ikipita siku hujashangaa kwa nini unashangaa sote humu hukushangaa
i) Mpaka kieleweka et al.: Si kweli kwamba Issa Shivji na Tundu Lissu ndio watu pekee wanaoijua mikataba ya madini au wenye uchungu na Tanzania. Kwa hiyo mimi kutukuwepo hawa katika kamati sioni tatizo kabisa. Tuache kasumba ya kufikiri kwamba ni watu fulani katika jamii yetu wenye uwezo wa kufanya mambo, huo na ni utegemezi! Ile nchi ina watu mil 36 wenye vipaji mbalimbali. Watu wakipewa kazi, tuwasukumu na kuwatia moyo kuhakikisha wanafanya kazi ya vizuri.
ii) Ndio nasema kila siku kuwa nchi yetu ina uhaba wa mafanikio kiasi kwamba hata likitokea jambo dogo inabidi tushangilie kama mazuzu. Ndiyo tuliweza kubagawa hata Rashid kushinda mashindano ya BBA. Sasa na hili nalo sishangai. Lakini binaafsi, at the risk of being seen cynical, sioni cha kushangilia. Yaani mafanikio hapa ni nini hasa hadi tumsifu JK? Huyu mtu kuna siku tutamsifia hata atakapoamka mapema. Kosa la mikataba mibovu walifanya wao, sasa wanapochukua hatua za kurekebisha tena kwa shinikizo, sisi tunachosifia hapa ni kitu gani hasa? Tunamsifia baba kununua nepi za mwanae? Ndio kusema siku JK atakapoamua kuwatoa akina Karamagi itabidi tufanye maandamana ya kumpongeza, tuna wazimu au nini?
Tunaelekea kuwa Taifa la walalamikaji au namna gani?
Pia amezidisha maafisa wa serikalini. Badala yake angeongeza wajumbe utoka nje ya serikali. Naunga mkono kumshirikisha Prof. Shifji. Hata mimi simuamini bwana Mapesa. Dr. Mwakyembe pia anaonekana kuwa kigeugeu (kumbukeni alivyokuwa akitetea matatizo ya CUF na CCM kwenye muafaka aliposhirikishwa kwenye kamati ya muafaka wakati wa Mhes. Mkapa.
Tundu Lisu si muhimu kwani ataweza kumpatia ushauri bwana mdogo Zito. Ila, pia Mzee Mark Bomani sina uhakika naye sana kuendesha kamati hii. Bi Simba Kijo angefaa kushirikishwa pia.
Kama kuna watu wa karibu na Mheshimiwa Kikwete, basi watufikishie ujumbe.