Wakuu wote;
Nimesoma mpaka page 8 ya thread hii; nilichoona ni kwamba kuna uelewa tofauti wa madhumuni ya kuunda tume kama nilvyomsikia mh. Rais, nilivyomsikia Rais wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM, ni kwamba ataunda tume nyingine ya Madini [ku-replace ile ya mheshimiwa Masha ambayo ilikuwa tume ya Serikali] nia ikiwa kuangalia wapi kuna mapungufu kwenye sheria ya 1998 ya madini kiasi kwamba tunakosa kama nchi maslahi stahiki.
Kwangu mimi naiona Tume hii, kama tume ya kuangalia tunatoka wapi tuko wapi, na tufanye nini ili tuweze kufaidika na madini yetu.
Tume hii sio kwa ajili ya kumchunguza Mh. Karamagi na Wizara yake...
Tume hii sio kuchunguza kwa nini mkapa ulisainiwa London,
In short tume hii sio ya kuchunguza mkataba mmoja specific, lakini tume inaweza chunguza mkataba mmoja au michache kama case studies.
Hivyo ndivyo nilivyoelewa!!!
Ndio maana Mh. Rais akasema "sisi kama serikali tulikuwa tunaendelea na Mh. Masha nadhani bado anaendelea hata baada ya kuwa naibu waziri wizara ya mambo ya ndani, lakini wenzetu naona hawatuamini, sasa tumeamua kuenda tume ambayo itawakuwa inajumuisha watu wengine zaidi ikiwepo upinzani, ... au hata dini kama nili lazima", ila la dini tone yake ilikuwa ya utani)
Quote hiyo ya mh. Rais, sio exact kama alivyosema lakini content ilikuwa similar na hiyo.
So sio jambo jipya, ni wajumbe wapya!!! na Terms of Reference Pana zaidi, ambazo expected output ni utungaji wa sheria mpya ya madini kama ... tume hii itagundua kwamba loyalt ya sasa ya 3.0% ni ndogo, inatakiwa say 10%, na vingine na vingine etc...