Kesi ya uhujumu uchumi / ugaidi namba 16 /2021 ya Mbowe na wenzie 3
Jaji M. Siyani ataachiwa asikilize kesi ya Mbowe na wenzie 3 mpaka mwisho au ndiyo kesi atapangiwa jaji mpya?
Toka maktaba:
6 Sept 2021
Mahakama Kuu
Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi
Dar es Salaam, Tanzania
Wakili Peter Kibatala azungumza baada ya Jaji Luvanda kujiengua
Habari kubwa iliyojitokeza Leo ni Jaji Luvanda ajitoa kesi ya Mbowe na wenzake.
Jaji Elinaza Luvanda wa Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa na aliyekuwa anaisikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya Ugaidi, amejitoa kusikikiza kesi hiyo.
Sababu ya kujitoa katika kesi hiyo ni kutokana na mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuieleza mahakama hiyo kuwa yeye na washtakiwa wenzake watatu hawana imani na Jaji huyo katika kutenda haki dhidi ya kesi yao.
Kesi imehairishwa mpaka jaji mwingine atakapopatikana. Pia awali Jaji Elinaza Benjamin Luvanda alikataa kutoa uamuzi wake leo juu ya mapingamizi ya upande wa utetetezi mpaka atapopata hansard / kumbukumbu za majadiliano ya Bunge kuhusu sheria ya ugaidi.
Wote walikubaliana kuwa kesi hii ina masilahi mapana kwa umma wote waliopo ndani ya Mahakama na nje.
Hoja 3 za upande za upande wa utetezi zilikuwa zinashambulia madhaifu na kasoro ya hati ya mashtaka. Hoja ya kwanza ilikubaliwa na jaji wakati hoja ya pili ilikubaliwa kwa nusu yake na jaji wakati hoja ya tatu ya kutupiliwa mbali au kufutwa kesi, jaji aliikataa.
Na kwa msingi huo mtuhumiwa Freeman Mbowe kwa niaba ya wenzake akasimama na kusema hawana imani na Jaji Elinaza Benjamin Luvanda kuendelea kusikiliza kesi hiyo, na mheshimiwa Jaji E.B Luvanda akaafiki ombi hilo na kujiengua kusikiliza kesi hii.
Source : Mwananchi Digital
Kutoka maktaba :
10 September 2021
MAHAKAMA KUU DIVISHENI MAALUM KUSIKILIZA KESI YA FREEMAN MBOWE NA WENZIWE 3, MFULULIZO KUANZIA TAREHE 15 SEPTEMBER 2021
Jaji Mustapher Siyani ameanza jukumu lake na kupanga kuanza kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi / ugaidi namba 16 /2021 ya Mbowe na wenzie 3 ambao kwa pamoja wa wakabiliwa na tuhuma za ugaidi kwa mujibu wa upande wa mashtaka wa serikali.
Mahakama hiyo chini ya jaji Mustapher Siyani imekubali pia ombi la upande wa utetezi unaoongozwa na wakili Peter Kibatala kuwa upande wa utetezi una mashahidi wake kadhaa na kuiomba Mahakama Kuu kuwa miongoni mwao mashahidi hao, wapo mashahidi 4 walindwe na Mahakama wasitangazwe anuani zao wala majina yao kwa kuhofia kufuatwa na vyombo vya serikali.