Huu uteuzi wa Siyani umekuja kimkakati au ni mpango uliokuwepo?
Hasa wakati huu ambao hukumu ya kesi ndogo ilikuwa inasubiriwa tar 19.10.2021, napata mashaka.
Nilimkubali sana alivyosikiliza kesi ndogo ya Mbowe, alikuwa kama refarii haswa, upande mmoja ukiweka objection anauliza upande wa pili wanaonaje, then wakijibu anarudi kwa upande wa waliotoa objection kama wanakubaliana na hoja ya upande wa pili, wakikataa, jaji anaangalia sheria inasemaje, then anaupa haki upande unaostahili kesi inaendelea kusikilizwa.
Sijui kama wataipangia kesi jaji mwingine, if yes, napata ukakasi na huu uteuzi kama sio wa kimkakati, kumuondoa huyu aliekuwa anaenda na sheria halafu wamrudishe kama yule wa mwanzo kuwafundisha jamhuri nini cha kufanya, fingers crossed.