Mkuu zandrano umekuwa mzalendo wa kukipigania kiswahili kuliko hata wenye dhamana kama vile BAKITA au TUKI.
Nakuunga mkono, Matumizi ya Lugha ya kiswahili ni Muhimu sana ktk kutoa haki za watanzania.
Sheria ilipitishwa Na Bunge kuwa Ruksa sasa Kwa Majaji wetu Na mahakimu wetu kuandika Na kutoa hukumu Kwa lugha ya kiswahili lkn cha kushangaza ukifika mahakamani hadi leo bado hukumu zinatolewa Kwa lugha ya kiingereza!! Kweli wananchi wengi wanakerwa sana Na hali hii!!
Inaonekana wazi Muhimili wa Mahakama hauko tayari kutumia lugha ya kiswahili kutoa haki ZA wananchi, kinacho fanyika ni kuwahadaa tu, sielewi kwa nini Na Kwa masilahi ya nani?!
Wananchi wanaomba Lugha ya kiswahili itumiwe Na Majaji Na mahakimu ktk kutoa haki zao.