TEUZI: Rais Samia Suluhu ateua Majaji wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu. DPP Mganga ateuliwa kuwa Jaji

Bi Mkubwa ndiyo kazi pekee anaweza labda na kusafirisafiri -- ila kwenda kukagua miradi ya maendeleo anaona karaha. ^Ilikuwa Dkt Mwinyi ndiye awe Makamo wangu^ JPM
Wacha ujinga mwamba! Mama ndiye Rais wetu utake usitake! Yaani kwenda kukagua miradi nayo ni kazi hiyo?
 
Samia haaminiki, katika majaji nilitegemea angalau mawakili wa kujitegemea wateuliwe maana kuna walio wazuri sana. Kinyume hakuna hata mmoja. Huyu mama twendeni tu mtaona huko mbele
one thing i am sure of kuhusu Samia ni kuwa hatakuwa Rais hayawani kama Jiwe, anawea asitende haki,akaboronga sana lakini Jiwe atashikilia rekodi kwa miaka mingi sana. Labda Mwigulu akija kuwa Rais anaweza kumfikia jiwe
 
One remarkable thing, hakuna aliyeteuliwa kutoka Principal and Senior Magistrate's court kuwa Jaji. Mbonà amewapiga chini kiasi hicho. Mashauri alipanda baada ya kuwafunga Mbowe.
Naona wametelekezwa, WHY?
uwezo mkuu, hawana uwezo hao mahakimu. walioteuliwa ni Wasajili ambao kicheo ni Mahakimu (Senior or principle), ambao at least wamekuwepo High Court, imagine unamteua hakimu hajawahi fika mahakama kuu ili akaendeshe kesi za mahakama kuu. si bora kumteua msajili ambaye kicheo ni hakimu na amekuwepo High court kwa muda akiona majaji wanafanya nini? hakimu akitoka moja kwa moja wengi huwa weupe hawajui procedure. hao mawakili wengine wa kujitegemea na mawakili wa serikali huwa wameshafanya kesi za mahakama kuu hadi mahakama ya rufaa ambako mahakimu hawajawahi gusa.
 
Hoja yako ina nguvu, lkn Hakimu, Principal one ambaye ana miaka kama 20 kweye bar anakuwa na ujuzi wa sheria mkubwa...., nafikiri hivyo anyway. Lakini zamani kawaida ni kuwa walikuwa wanatokea huko kwa kupewa Magistrates with Extended jurisdiction, then they are there! Basi mashauri alibahatika kuwafunga Mbowe na kuukwaa Ujaji!
 
one thing i am sure of kuhusu Samia ni kuwa hatakuwa Rais hayawani kama Jiwe, anawea asitende haki,akaboronga sana lakini Jiwe atashikilia rekodi kwa miaka mingi sana. Labda Mwigulu akija kuwa Rais anaweza kumfikia jiwe
This is the post of the day. Umehitimisha siku ya leo kwa post yako. Ukweli ambao utadumu millele JF kwa post yako.

Mwigulu ni fashist kuliko mtu anvyoweza kufikiri....
 
Mkikazana anaweza akarudi, maana wapo walioomba aondolewe wakasikiwa.
Ombeni bila kukoma atarudi
Hongera mama kwa kazi njema lilikuwa jambo la aiby na ukatili mkubwa kuwatesa watu magerezani kwae kisingizio cha upelelezi haujakamilika mwisho wa siku unawaambia mwende mkakiri makosa yenu kwa DPP atakayekataa akae rumande hata miaka ishirini. Mpaka CAG anakuta akaunti ya DPP Ina mabilioni yaliyopatikana nje ya utaratibu mpaka wanaogopa kuzitumia.
 
Huyu Dpp wa Zamani alipaswa kuwekwa pembeni kabisa,yule siyo binadamu yule ni jambazi tu. Mfano case za uhujumu uchumi,ameshiriki sana kuwafirisi.
Amevionea sana vyama vya siasa na amekuwa akijifanya Mungu kwenye hii nchi.
 
DPP ni mtu mkubwa hivyo kimajukumu ...?
 
nimekuwepo Mahakamani muda mrefu, amini usiamini, mahakimu hao wakianza kuwa majaji wanafundishwa na makarani procedure. nilishawahi shuhudia kabisa hapahapa dsm. hajui chochote kwasababu maisha yake yote amezoea kesi za kuku huku chini, wakati mawakili wa kujitegemea na mawakili wa serikali akifikisha miaka 5 tu anaanza mahakama za rufaa kwahiyo anakuwa na uzoefu mkubwa sana wa high court, na baadaye court of appeal, wakati hakimu muda huo anatumia karibia mwaka kujifunza procedure za huko.
 
Bi Mkubwa ndiyo kazi pekee anaweza labda na kusafirisafiri -- ila kwenda kukagua miradi ya maendeleo anaona karaha. ^Ilikuwa Dkt Mwinyi ndiye awe Makamo wangu^ JPM
Hizo chuki zako mpaka sasa anafanya kai nzuri sana ya kupanga upya serikali ambayo ilikuwa ikiendeshwa kwa amri ya mtu mmoja ambaye yeye alikuwa serikali, mahakama na bunge. Hongera mama safisha safisha nyumba kwanza kabla ya kuanza kutembelea hiyo miradi.
 
Najua kiroho kinawauma ,hamkutaka apate teuzi ,mungu si athumani ,huyo ni jaji kwa sasa na majaji Serikali inawajali sana ,wewe endelea kusugua gaga
Mimi huko sipo kabisa!!ila ninachoshukuru nauona mwanga mpya kwenye ofisi ya mwendesha mashitaka, kama tunavyouona huko TCRA, yaani li jitu linajifanya kama MUNGU!!ngoja uone sasa watu wenye makosa ya kubambakiwa wanavyoanza kutoka mahabusu!!kwani majukumu yote ya mahakama alikuwa amejipa yeye?!!kule atapata stahiki ambazo majaji wanazipata kisheria sio huku ambako alikuwa anajiamlia tu , nimbambikie nani kesi!!gang lote la meko lazima litoke kwenye nafasi walizokuwa nazo, hadi sasa top 4 wote wameshafyekwa!!kwani walisumbua sana jamii huko walikofichwa hawana madhara tena kwetu
 
umeniacha hoi, kuku? nakumbuka akina Rugazia RIP wametokea kisutu.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…