TEUZI: Rais Samia Suluhu ateua Majaji wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu. DPP Mganga ateuliwa kuwa Jaji

TEUZI: Rais Samia Suluhu ateua Majaji wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu. DPP Mganga ateuliwa kuwa Jaji

Siku moja walionyesha mijinoti imekaribia kujaa chumba , eti wale waliokubali makosa na kuingia makubaliano ya kulipa!!pale kuna nini?waezipiga sana!!lakini kwenye ujaji , hakuna ubabe, ukimuonea mtu anakata rufaa, au ana kukataa!!!jamaa ni pigo sana kwake, ila kwa wapenda haki ni furaha!!
Najua kiroho kinawauma ,hamkutaka apate teuzi ,mungu si athumani ,huyo ni jaji kwa sasa na majaji Serikali inawajali sana ,wewe endelea kusugua gaga
 
Hayo ni mabadiliko ya kawaida kabisa kwenye mifumo ya serikali

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote
 
Bi Mkubwa ndiyo kazi pekee anaweza labda na kusafirisafiri -- ila kwenda kukagua miradi ya maendeleo anaona karaha. ^Ilikuwa Dkt Mwinyi ndiye awe Makamo wangu^ JPM
We nae...hebu mwache mama yetu.

Kila bandiko lako ni kimkandia mama yetu tu... kakukosea nini?
 
BADO Kichele

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Weeee koma
IMG_20210412_105955_511.JPG
 
Una maana ileee safari ya kwa M7 na kwa Mr Freedom juzi, nyumba ya Jamaa wa Msoga na Benzi ya Mzee Ruksa vimekomba ^killer-key-2^ pale hazinani. Kumbe ndiyo maana waliharakisha sanaaa kumpandisha cheo Dkt Mpango ili atoke kule wafanye yao!??? Hii ni hatari na robo ^tar-two^¡¡¡ Nahisi kufikia mwisho wa mwaka Bi Mkubwa lazima atatembeza bakuli la michango huku mtaani, kama ndio mwendo huu.
We kenge umetuchokesha na maujinga yako!

Stop your nonsense!
 
Mi nilisema mapema huyu mama siyo
Una taka aendelee na Sukuma gang kama Maganga alie kalia mafaili ya watu miaka mitano sasa? Yaani watu wako mahabusu hawajui wata toka lini kisa Dpp? Kweli?
 

Toka maktaba mwaka 2014​

DPP ateuliwa kuwa jaji​

By France

August 15, 2014

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer FeleshiAliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi
NA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM

RAIS Jakaya Kikwete leo anatarajia kuwaapisha majaji wapya wa Mahakama Kuu, akiwamo Dk. Eliezer Feleshi ambaye awali alikuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Uteuzi huo umewajumuisha watumishi wa mahakama na mawakili wa Serikali wa kujitegemea pamoja na watumishi wa taasisi mbalimbali za serikali.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) juzi, inaeleza kuwa uteuzi huo umefanywa baada ya Rais Kikwete kushauriana na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo umeanza Agosti 13, mwaka huu na wateuliwa wote wataapishwa leo saa 5:00 asubuhi katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

Watumishi wa mahakama walioteuliwa ni Penterine Kente ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, Dar es Salaam, Benedict Mwingwa aliyekuwa Msajili wa Mahakama Kuu Dar es Salaam na Edson Mkasimongwa ambaye awali alikuwa Katibu wa Jaji Mkuu.

Wengine ni David Mrango aliyekuwa Msajili Baraza la Ushindani, Dar es Salaam, Mohamed Rashid Gwae aliyekuwa Msajili Mahakama Kuu, Kitengo cha Kazi, Dar es Salaam, Dk. John Ruhangisa ambaye kabla alikuwa Msajili Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha na Firmin Matogoro aliyekuwa Naibu Mwenyekiti Baraza la Rufaa la Kodi, Dar es Salaam.

Mawakili wa Serikali na taasisi mbalimbali za serikali ni pamoja na Dk. Feleshi ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi wa Mashtaka, Dar es Salaam, Barke Mbaraka Aboud Sehel ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.

Wengine ni Winfrida Beatrice Korosso aliyekuwa Katibu Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria, Dar es Salaam, Lilian Mashaka ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (Takukuru), Dar es Salaam.

Uteuzi huo pia umewajumuisha Leila Edith Mgonya ambaye alikuwa Msaidizi wa Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dar es Salaam, Awadhi Mohamed aliyekuwa Mchunguzi Mkuu Takukuru, Dar es Salaam.

Kwa upande wa mawakili wa kujitegemea, walioteuliwa ni Lugano mwandambo kutoka REX Attorneys, Dar es Salaam, Amour Khamisi kutoka AKSA Attorneys, Dar es Salaam.

Wengine ni Paul Kihwelu aliyekuwa wakili wa kujitegemea na Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu Huria (OUT) Dar es Salaam, Rose Ebrahimu ambaye alikuwa wakili wa kujitegemea, Bulyankulu Gold Mine Ltd, Shinyanga na Salma Maghimbi, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mjumbe, Tume ya Ushindani, (FCC), Dar es Salaam.

Uteuzi huo pia umewahusisha watumishi wa vyuo vikuu, akiwamo Dk. Mary Caroline Levira, ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha na Modesta Opiyo Makopolo aliyekuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu, Mzumbe, Morogoro SOMA ZAIDI Source DPP ateuliwa kuwa jaji | Mtanzania
 
Atuwekee na Rcs, Dcs, makatibu tawala safu iapishwe siku moja.
 
Lakini wait...Mama alisema atachagua Watu bila kujali itikadi zao na Vyama vyao au Mataga ndio wamempiga Biti.

Hii Nchi inaangamizwa na ccm.
 
Ni mchakato mrefu pia katiba inamlinda DPP. Hivyo mfano DPP angetofautiana na utashi wa mwendazake dawa ni kumpandisha cheo.

Pia rais ukiona huridhishwi na mwenendo wa DPP pia njia rahisi ni kumpandisha cheo.

Kwa nchi za Madola wadhifa huu wa DPP ni wenye nguvu sana kikatiba ktk nchi za Jumuiya za Madola / Commonwealth.
Acheni ujinga Biswalo kaula ,nafasi ya DPP huteuliwa na Rais ,hivyo akizingua anafukuzwa tu kazi ,na si kupandishwa cheo ,hii mnayofanya ni propaganda mfu,
Biswalo kaitendea haki ofisi ya DPP kwa kuwatemesha pesa za umma vibaka wote akiwemo na baba yako mzazi
 
Samia haaminiki, katika majaji nilitegemea angalau mawakili wa kujitegemea wateuliwe maana kuna walio wazuri sana. Kinyume hakuna hata mmoja. Huyu mama twendeni tu mtaona huko mbele
Kawatosa kabisa mawakili wa kujitegemea
 
Back
Top Bottom