Teuzi ya Maxence Melo, ina maana gani kwa JF na wanachama wake?

Teuzi ya Maxence Melo, ina maana gani kwa JF na wanachama wake?

Ina maana mtabaki yatima, kule kuna mpunga hatari. Faragha nayo inaleta mashaka kama jamaa ataendelea kutulinda
 
Nashangaa sana kwa namna watu wanavyodhani Melo amewekwa mfukoni kisa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Watu wanasahau mapema sana

Melo ndio amekuwa mstari wa mbele kabisa kupigania Ulinzi wa Taarifa Binafsi hadi kuwepo kwa sheria na Kanuni zake, kwa nafasi hiyo naamini anaenda kusimamia haki kwa Wananchi kama alivyopigania Ulinzi wa taarifa zetu na faragha yetu kidijitali

Halafu kwa wengine humu mtakuwa hamumjui Melo, ni mtu amenyooka sana hawezi kuweka mfukoni kwa uteuzi kama huo
 
Ingekuwa kheri kwake kama angekabidhi ukurugenzi wa JF Kwa mtu mwingine.
 
Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums ameteuliwa kuwa mmjoa wa wajumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa muda wa miaka mitatu. Suala hili limezuia mijadala hata kwa wanachama wa JamiiForums wakidhani uhuru wao utakuwa umeminywa.

Unayopaswa kujua.
Bodi inayoundwa ni kwa ajili ya kuisimamia Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Kwa mujibu wa Kifungu cha 9 cha Sheria ya Ulinzi wa taarifa binafsi, bodi ina majukumu haya,

9.-(1) Bodi itasimamia utendaji wa Tume ilikuhakikisha kuwa utendaji huo unazingatia sheria nataratibu zinazosimamia Tume.
(2) Bila kuathiri ujumla wa kifungu kidogo cha (1),Bodi itakuwa na wajibu wa-
(a) kutoa miongozo ya kimkakati na kuunda seraza uendeshaji na usimamizi wa Tume;​
(b) kusimamia shughuli na utendaji kazi wamenejimenti ya Tume;​
(c) kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali,ikijumuisha kuidhinishwa kwa mpango kazi wamwaka, bajeti ya mwaka na bajeti ya nyongeza;​
(d) kuidhinisha mipango ya uwekezaji ya Tume;​
(e) kuidhinisha ripoti za utendaji kazi wa Tume;​
(f) kuidhinisha kanuni za maadili kwa watumishiwa Tume;​
(g) kuidhinisha na kusimamia taratibu zausimamizi wa fedha na kanuni za utumishi waTume;​
(h) kuidhinisha uondoshaji wa mali za Tume; na​
(i) kutekeleza wajibu mwingine wowote kwa kadriTume itakavyoona inafaa kwa ajili ya kutimizamalengo yake kwa mujibu wa Sheria hii.​
10. Bodi inaweza, kwa madhumuni ya kutekelezamajukumu yake kwa ufanisi, kuunda na kuteua kutokamiongoni mwa wajumbe wake, kamati zozote kadriitakavyoona inafaa.

Kutokana na majukumu hayo msingi ya Bodi, JamiiForums haitaathirika kwa teuzi hii bali itakuwa katika nafasi ya kuhakikisha yanayosemwa na wananchi yanafika kwenye tume ya ulinzi wa taarifa binafsi

Aidha, Maxence Melo hajateuliwa kutokana na UCHAWA bali kutokana na mchango wake katika Ulinzi wa Taarifa binafsi. Mimi naona anaenda kuwa kama mwalimu kwa wengine ambao wapo ambao uelewa wao ni finyu kwenye masuala ya taarifa binafsi.

Aidha kwa sababu sio chawa, sidhani kama atashindwa kujiuzulu ikiwa atakutana na mambo ambayo hakubaliani nayo. Ikumbukwe mjumbe wa bodi anaruhusiwa kujiuzulu kwa kifungu cha 1(1)(3), kama ambavyo amekuwa akitetea suala la haki na faragha za watu, uteuzi huu hauko katika nafasi ya kumtoa katika kitu amesimamia miaka yote.

KWA WANA JF
Baada ya kujua kuwa mkurugenzi ni mjumbe wa bodi, WanaJF wanakuwa na nafasi ya moja kwa moja ya kuishauri bodi kwa kuwa wakiweka mawazo yao hapa yana nafasi ya kuonekana na watu kuchukua hatua. Maana yake ni kuwa, kama Maxence anaenda kushauri jambo anajua kutoka kwa wananchama anaweza kuthibitsha kwamba wananchi wanapitia hiki au kile. Hii maana yake wanachama wana nafasi kubwa ya kushiriki mchakato huu kwa uzuri.
We mwenyewe ni chawa, acha kujipendekeza kwa huyo Mello
 
Tatizo moja la middle class ni UOGA TU, wanafikiri kuwa Mr. Melo kuwemo kwenye bodi ile itamfanya anunulike kirahisi na kutoa informations kuhusiana na IDs za humu ndani! ninaweka kichwa changu kwenye chopping block ,Mr. Melo hawezi kufanya hili, welldone kwako Mr. Melo kwa uteuzi wako, your a great man
Kitu kidogo km hicho ndiyo mhangaike na upambe
 
Sijui hata umeandika nini....
Jf ya 2015 kurudi nyuma sio JF ya 2015 kusonga mbele....hii inatokana na mfumo kupenyeza mods ndani ya hili jukwaa.
Mods wamechangia sana jf kukosa flavour kabisa....sembuse boss kaenda kitengo si ndo itageuka jukwaa la kampeni ya ccm ya tuvuke na mama 2025
Umeongea kwa uchache, ila umeongea kitu kikubwa na kizito sana. Mwenye masikio na asikie.
 
Dare to talk openly with caution
Well.said.
Miaka ya karibuni kuna trend imeanza humu ndani admin wanachomoa thread zingine zikipostiwa bila kutoa justification..hii inaleta feedback kua usiamini mtu kwa kila jambo na wakati wote.
 
Tatizo moja la middle class ni UOGA TU, wanafikiri kuwa Mr. Melo kuwemo kwenye bodi ile itamfanya anunulike kirahisi na kutoa informations kuhusiana na IDs za humu ndani! ninaweka kichwa changu kwenye chopping block ,Mr. Melo hawezi kufanya hili, welldone kwako Mr. Melo kwa uteuzi wako, your a great man
Tatizo ni kwamba atalambishwa asali tu,
 
Mfumo ni mfumo tuu...maxence melo mtani wangu na boss wangu hapa lazima akubali kuingia kwenye mfumo wa kidola. Hakuna atakachosaidia na ameshaingia kwenye mfumo. In short ameyatimba kiaina.
Ukweli ndo huu.
 
Sijui hata umeandika nini....
Jf ya 2015 kurudi nyuma sio JF ya 2015 kusonga mbele....hii inatokana na mfumo kupenyeza mods ndani ya hili jukwaa.
Mods wamechangia sana jf kukosa flavour kabisa....sembuse boss kaenda kitengo si ndo itageuka jukwaa la kampeni ya ccm ya tuvuke na mama 2025
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwani hata sasa taarifa zetu za hapa Jf unafikiri hawana? Au unafikiri kwamba wanashindwa kuzipata bila hata kuwasiliana na Uongozi wa Jf?
Tambueni tu kwamba hakuna Siri yoyote ile hapa, kila kitu wanakifahamu.
Watazipatajee? Hukumbuki mello jinsi alivyokuwa na seke seke kule rumande, lakini hakutajaa kamweee.

Sahivi inatujia uoga, mmmh
 
Watazipatajee? Hukumbuki mello jinsi alivyokuwa na seke seke kule rumande, lakini hakutajaa kamweee.

Sahivi inatujia uoga, mmmh
Je. Unaelewa lengo la zoezi la usajili tena wa hao watoa huduma za mitandaoni lililofanyika miaka Michache iliyopita??Do you know the reasons???
 
Kwani hata sasa taarifa zetu za hapa Jf unafikiri hawana? Au unafikiri kwamba wanashindwa kuzipata bila hata kuwasiliana na Uongozi wa Jf?
Tambueni tu kwamba hakuna Siri yoyote ile hapa, kila kitu wanakifahamu.
Hamna kitu Kama hicho ,usitishe watu .. nadhani wewe Ni mgeni mengi huuafahamu ya Jf!
 
Back
Top Bottom