Teuzi ya Maxence Melo, ina maana gani kwa JF na wanachama wake?

Ina maana mtabaki yatima, kule kuna mpunga hatari. Faragha nayo inaleta mashaka kama jamaa ataendelea kutulinda
 
Nashangaa sana kwa namna watu wanavyodhani Melo amewekwa mfukoni kisa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Watu wanasahau mapema sana

Melo ndio amekuwa mstari wa mbele kabisa kupigania Ulinzi wa Taarifa Binafsi hadi kuwepo kwa sheria na Kanuni zake, kwa nafasi hiyo naamini anaenda kusimamia haki kwa Wananchi kama alivyopigania Ulinzi wa taarifa zetu na faragha yetu kidijitali

Halafu kwa wengine humu mtakuwa hamumjui Melo, ni mtu amenyooka sana hawezi kuweka mfukoni kwa uteuzi kama huo
 
Ingekuwa kheri kwake kama angekabidhi ukurugenzi wa JF Kwa mtu mwingine.
 
We mwenyewe ni chawa, acha kujipendekeza kwa huyo Mello
 
Kitu kidogo km hicho ndiyo mhangaike na upambe
 
Umeongea kwa uchache, ila umeongea kitu kikubwa na kizito sana. Mwenye masikio na asikie.
 
Dare to talk openly with caution
Well.said.
Miaka ya karibuni kuna trend imeanza humu ndani admin wanachomoa thread zingine zikipostiwa bila kutoa justification..hii inaleta feedback kua usiamini mtu kwa kila jambo na wakati wote.
 
Tatizo ni kwamba atalambishwa asali tu,
 
Mfumo ni mfumo tuu...maxence melo mtani wangu na boss wangu hapa lazima akubali kuingia kwenye mfumo wa kidola. Hakuna atakachosaidia na ameshaingia kwenye mfumo. In short ameyatimba kiaina.
Ukweli ndo huu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwani hata sasa taarifa zetu za hapa Jf unafikiri hawana? Au unafikiri kwamba wanashindwa kuzipata bila hata kuwasiliana na Uongozi wa Jf?
Tambueni tu kwamba hakuna Siri yoyote ile hapa, kila kitu wanakifahamu.
Watazipatajee? Hukumbuki mello jinsi alivyokuwa na seke seke kule rumande, lakini hakutajaa kamweee.

Sahivi inatujia uoga, mmmh
 
Watazipatajee? Hukumbuki mello jinsi alivyokuwa na seke seke kule rumande, lakini hakutajaa kamweee.

Sahivi inatujia uoga, mmmh
Je. Unaelewa lengo la zoezi la usajili tena wa hao watoa huduma za mitandaoni lililofanyika miaka Michache iliyopita??Do you know the reasons???
 
Kwani hata sasa taarifa zetu za hapa Jf unafikiri hawana? Au unafikiri kwamba wanashindwa kuzipata bila hata kuwasiliana na Uongozi wa Jf?
Tambueni tu kwamba hakuna Siri yoyote ile hapa, kila kitu wanakifahamu.
Hamna kitu Kama hicho ,usitishe watu .. nadhani wewe Ni mgeni mengi huuafahamu ya Jf!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…