Teuzi ya Maxence Melo, ina maana gani kwa JF na wanachama wake?

Ukiishateuliwa na ukakubali uteuzi, ahahahahaha!!!
 
Kilichonishangaza umetuuliza Sisi Maswali ili tukujibu lakini nawe tena kwa Kiherere chako umejijubu katika baadhi ya Aya zako za huu Uzi hivyo ni kama tu Unatuchanganya na Kutusanifu kimtindo vile vile.

Asante Onana, Lakred na Benchika!!!
 
Wasiwasi ambao wewe umeuita uoga ni akili pia, nchi hii tumeshuhudia mengi, ikiwemo watu kupotea, kutekwa na kudhuriwa...
 
[emoji1666][emoji1666][emoji1666] tena mada/issue nzito nzito zilitupwa humu unashangaa hazifunguki au kufutwa...
 
Well.said.
Miaka ya karibuni kuna trend imeanza humu ndani admin wanachomoa thread zingine zikipostiwa bila kutoa justification..hii inaleta feedback kua usiamini mtu kwa kila jambo na wakati wote.
Jf imepoteza ubora.... 2011 nlikua napita humu kama guest naogopa hata kucomment sina content..
2013 nikajiunga (id yangu ya zamani ina tabu kidogo) JF ilikua nzuri kweli, ukiwa na jambo lako chap haraka unapata majibu,
Madudu ya kwenye jamii mtu unakuja kuyamwaga humu bila hofu lakini sahizi ubabaifu umekua mwingi sana.
Hii futa futa ya thread mara comment yako ikipitiwa na mods ndo itaruhusiwa ni upuuzi.
Kama vipi wafute baadhi ya majukwaa
 
Yawezekana ni woga tu usio na msingi, lakini tahadhari ni muhimu sana maishani.

Ni ukweli kuwa USIRI Ndio nguzo kubwa ya Mtandao wetu huu. CONFIDENTIALITY/ANONYMITY. Serikali yetu, toka enzi za JK, haiipendi JF. Utawala wa JPM ulitumia mbinu za kibabe dhidi ya JF, zikashindwa.

Kuwa karibu na adui yako, ni moja ya mbinu za kupambana nae. Wanawake ni mafundi sana wa mbinu hii.

Bwana Melo ameanza kuwa karibu sana na Gavoo. Ameanza kupata 'mashavu'.

Mimi ninaanza sana kupata wasiwasi na hatma ya huu mtandao.
 
Naamini uzi huu haujakiuka sheria ya mijadala hapa JF naamini badala ya kufutwa JamiiForums inapaswa kujibu.

Miongoni mwa taarifa zilizo gonga vichwa vya habari ni ile ya uteuzi wa Mkurugenzi wa JF ndugu Maxence Melo rejea uzi huu Maxence Melo ateuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Kwa upande wangu uteuzi huu ni kiashiria kwamba JamiiForums si jukwaa salama tena. Siamini kama privacy yangu itaendelea kuwa stable maana mmiliki wa jukwaa ambaye ana access ya taarifa zangu binafsi ni mteule wa waziri, waziri ambaye ni mteule wa Rais.

Sidhani kama Max anaweza kuwanyima hawa watu taarifa zako hivyo ukiwa na issue sensitive nakushauri utafakari mara 2 kabla ya kuiweka hapa.

Pia nashauri ndugu Maxence Melo either aachie ngazi hapa JF na kumkabidhi mikoba Mike Mushi au akatae uteuzi tata aliopata vinginevyo sioni mwanga wa usiri wa taarifa binafsi hapa jukwaani.

Mods badala ya kukimbilia kufuta, jibuni tuambieni boss wenu ambaye ni mteule serikalini akiwaomba taarifa zangu hamta mtumia ili aziwasilishe kwa boss wake?
 
Kwa jambo gani sensitive ulilonalo uhofie kujulikana? Ni hizi chit chat tuu?
 
Max aliwahi kusema kuwa huwa anawanyima polisi access pale wanapotaka kujua taarifa zetu binafsi.
Polisi!...tiss wanakujua vizuri tu,mimi nilishaona mtu ananiripoti akitaja kuna langu la ukoo hapa,nadhani alikosea badala ya kutuma huko anakotakiwa kutuma akareply,tena yuko bize humu acha tu
 
Huyu anakwenda kuwa kuwadi wa CCM tu,, hakuna lingine.....tujiandae kutekwa sasa na kuuliwa kwa kusema ukweli.
 
Maxence kishaoza tayari, anakwenda kuwa chawa tu wa CCM, sina kabisa imani naye hata kidogo. Never deal na viongozi incompetent kwani hawapendi kukosolewa hata kidogo, wao wanawaza kuua tu na kuiba.
 
inafikirisha sana, mero kuwa pamoja na serikali....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…