John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Rais wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Wallace Karia amezungumzia matumizi ya VAR wakati wa kufunga semina ya siku tatu ya Waamuzi wa Ligi Kuu ya NBC iliyomalizika jana Februari 17, 2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Haya hapa ndiyo aliyoyasema Karia: “Unajua gharama za VAR? Sawa najua Serikali wanaliangaia hilo.
“Ili kupata ile VAR seti nzima ni karibu Sh bilioni 14.5, mbali ya kamera za Azam TV, VAR nao wanatakiwa kuwa na kamera zao kuanzia 33 hadi 38.
“Na tukiamua kuweka lazima tupate kibali kutoka kwao kwa kuwa siyo mali yetu, pia kila mechi klabu zinatakiwa kushea gharama ya kutumia hiyo VAR ambayo ni kama Sh milioni 7 hivi.”
Hatua hiyo inakuja kutokana na presha kubwa ambayo imekuwa ikiendelea hivi karibuni kutokana na waamuzi kadhaa wa soka kufanya makosa katika Ligi Kuu Bara msimu huu unaoendelea wa 2021/22.
Karia akaongeza kwa kusema: “Kuna mambo mengi yanazungumzwa, mengine kwa wadau kutojua sheria na mengine nayafanya makosa kweli.
“Mnafanya makosa nyie lawama zinakuja kwangu, sijawahi kutoa maelekezo kwa waamuzi hata mara moja.”