TFF: Bei ya VAR ni Sh Bilioni 14.5, kamera ziwe 38, kila mechi timu zinalipia Sh milioni 7

TFF: Bei ya VAR ni Sh Bilioni 14.5, kamera ziwe 38, kila mechi timu zinalipia Sh milioni 7

Lupweko amekariri standard za FIFA halafu hajui ukomo wa standards za FIFA zinahusika katika ngazi zipi. Standard za FIFA zinafanya kazi kwa ngazi za kimataifa pekee.

Rais wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Wallace Karia amezungumzia matumizi ya VAR wakati wa kufunga semina ya siku tatu ya Waamuzi wa Ligi Kuu ya NBC iliyomalizika jana Februari 17, 2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Haya hapa ndiyo aliyoyasema Karia: “Unajua gharama za VAR? Sawa najua Serikali wanaliangaia hilo.

“Ili kupata ile VAR seti nzima ni karibu Sh bilioni 14.5, mbali ya kamera za Azam TV, VAR nao wanatakiwa kuwa na kamera zao kuanzia 33 hadi 38.

“Na tukiamua kuweka lazima tupate kibali kutoka kwao kwa kuwa siyo mali yetu, pia kila mechi klabu zinatakiwa kushea gharama ya kutumia hiyo VAR ambayo ni kama Sh milioni 7 hivi.”

Hatua hiyo inakuja kutokana na presha kubwa ambayo imekuwa ikiendelea hivi karibuni kutokana na waamuzi kadhaa wa soka kufanya makosa katika Ligi Kuu Bara msimu huu unaoendelea wa 2021/22.

Karia akaongeza kwa kusema: “Kuna mambo mengi yanazungumzwa, mengine kwa wadau kutojua sheria na mengine nayafanya makosa kweli.

“Mnafanya makosa nyie lawama zinakuja kwangu, sijawahi kutoa maelekezo kwa waamuzi hata mara moja.”

Kariaa.jpg

Kwa mashindano ya ndani kinachoangaliwa ni namna ya kufuata zile sheria za FIFA, kama ingekuwa kunakufuata standards za FIFA basi tungeona FIFA wanaingilia kati juu ya viwanja vyetu vibovu tunavyotumia kwenye ligi yet
 
Hatutaki VAR kama za ulaya bali replay za Azam pekee zinatosha kwa mwamuzi kuangalia tukio uwanjani na kujiridhisha kama sisi tunaoangalia kwenye luninga tunavyopata wasaa kujiridhisha. Gharama hapo ni kununua tv na ving'amuzi vya Azam tu na kuviweka viwanjani. Na azam pia waongeze idadi za camera zao
Azam mvua ikinyesha inakuaje
 
Kwanza wakarabati viwanja kwa hizo pesa, hizi kelele za VAR ni mihemko tu ya Mwigulu na timu yake utopolo, siku utopolo nao wakifaidika na maamuzi ya refa kelele zao zote za VAR zitakwisha, nasisitiza hiyo pesa kwanza ikaboresha viwanja (pitch).
 
Kwa mashindano ya ndani kinachoangaliwa ni namna ya kufuata zile sheria za FIFA, kama ingekuwa kunakufuata standards za FIFA basi tungeona FIFA wanaingilia kati juu ya viwanja vyetu vibovu tunavyotumia kwenye ligi yet au unataka kusema kiwanja kama cha Manungu kipo kwenye standard ya FIFA? Lakini hawawezi kuingilia kati kwasababu ni mashindano ya ndani ila inapotokea mashindano ya kimataifa hapo ndipo kitu kinachoitwa standard hutumika. Halafu pili toa kichwani kwako dhana ya V.A.R kama limtambo likubwa kama la wazungu bali sisi tutumie tu replay inatosha sana na hakuna kosa litakalokuwa limekiukwa ndani ya sheria za FIFA eti kisa waamuzi kupitia replay kwenye mashindano yetu ya ndani
Bila shaka TFF wameona ushauri wako tusubiri utekelezaji
 
Karia anachanganya mambo makusudi, makosa ya marefa tunayaona kupitia replay za Azam tv. Siyo kosa replay tunazo ziona sisi na wao marefa wawekewe pale uwanjani walau kwa kuanzia. Implementation ya VAR hata huko Ulaya inatofautiana kwa baadhi ya nchi.
 
Karia anachanganya mambo makusudi, makosa ya marefa tunayaona kupitia replay za Azam tv. Siyo kosa replay tunazo ziona sisi na wao marefa wawekewe pale uwanjani walau kwa kuanzia. Implementation ya VAR hata huko Ulaya inatofautiana kwa baadhi ya nchi.
Ni kweli mkuu
 
V.A.R (Video assistance Refaree) kwani hizo replays za Azam nazo si ni Video? Au mpaka kutumia kamera za wazungu ndo zitaitwa Video
 
Ukitaka uone TFF hawapo serious na mpira wa bongo angalia hiyo nembo ya GSM bado hadi leo inadisplay kama moja ya wadhamini wa Ligi kuu pamoja na mkataba kusitishwa wiki sasa.

Kila mwaka kuna fungu linatoka FIFA kwa ajili ya maendeleo ya soka kwa mashirikishi ya mpira lakini sioni TFF wanatumia vp fungu hilo ni bors wanunue hizo VAR tu
Uweke VAR kwenye viwanja kama madimbwi ya Samaki hebu tuwe serious kidogo.

Billion 14 itahudumia viwaja vingapi kuweka nyasi bandia na taa za usiku ?
 
Back
Top Bottom